Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
- Thread starter
- #241
Hakuna ubaya yoyote msomi wa level ya degree kufanya kazi za darasa la saba. Shida ni kule kupoteza rasilimali (muda, pesa, nguvu, akili) za kupata degree wakati hitimisho ni kuja kufanya kazi ambazo hazina huo uhitaji wa degree.Kufanya hizo kazi zinazofanywa na wasio na elimu sio vibaya hata kidogo.
Ila kwa kuwa ni 'msomi' namna atavyozifanya hizo kazi kutakuwa Kuna utofauti na wale wengine, Kama mfano ni Kilimo au biashara huyu 'msomi' akichanganya hiyo shughuli yake na maarifa aliyonayo tegemea matokeo mazuri mno na endelevu kuliko asiye na elimu kabisa.
Upande wa pili, msomi wa degree anakuwa mzito sana kuweza kumudu kuanza au kudumu kufanya kazi za darasa la Saba kwa ufanisi, kwa sababu ya aibu, fedheha, kuchekwa, kudharaulika na kushindwa kuamini, kujiamini na kujikubali kwa sababu ya ndoto na mitizamo iliyojaa akilini mwake. Wengi hujiona hapo sio mahali wanapostahili kuwa, kivuli cha degree huwatesa wengi na kwa muda mrefu.