Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kufanya hizo kazi zinazofanywa na wasio na elimu sio vibaya hata kidogo.

Ila kwa kuwa ni 'msomi' namna atavyozifanya hizo kazi kutakuwa Kuna utofauti na wale wengine, Kama mfano ni Kilimo au biashara huyu 'msomi' akichanganya hiyo shughuli yake na maarifa aliyonayo tegemea matokeo mazuri mno na endelevu kuliko asiye na elimu kabisa.
Hakuna ubaya yoyote msomi wa level ya degree kufanya kazi za darasa la saba. Shida ni kule kupoteza rasilimali (muda, pesa, nguvu, akili) za kupata degree wakati hitimisho ni kuja kufanya kazi ambazo hazina huo uhitaji wa degree.

Upande wa pili, msomi wa degree anakuwa mzito sana kuweza kumudu kuanza au kudumu kufanya kazi za darasa la Saba kwa ufanisi, kwa sababu ya aibu, fedheha, kuchekwa, kudharaulika na kushindwa kuamini, kujiamini na kujikubali kwa sababu ya ndoto na mitizamo iliyojaa akilini mwake. Wengi hujiona hapo sio mahali wanapostahili kuwa, kivuli cha degree huwatesa wengi na kwa muda mrefu.
 
Njia pekee ya kutoboa sasa hivi huko vyuoni hakikisha unakuwa kada wa CCM kupitia UVCCM. AIsee ukishaingia huko connection ya kupata kazi ni chapuuuu. Sasa ww jiroge uingie BAVICHA ndio utajua haujui
Msoto wa kukosa ajira na kipato kwa wahitimu kwa 90% uko pale pale haijarishi wewe ni kada wa CCM au CHADEMA.
Yaani CCM awaache vichwa maji kama Bashite kuwapa ajira halafu ikumbatie wasomi?

Ni chawa wachache sana hutoboa, na hao ndio huangukia katika wale 10% ya wahitimu wote.
 
Hakuna ubaya yoyote msomi wa level ya degree kufanya kazi za darasa la saba. Shida ni kule kupoteza rasilimali (muda, pesa, nguvu, akili) za kupata degree wakati hitimisho ni kuja kufanya kazi ambazo hazina huo uhitaji wa degree.

Upande wa pili, msomi wa degree anakuwa mzito sana kuweza kumudu kuanza au kudumu kufanya kazi za darasa la Saba kwa ufanisi, kwa sababu ya aibu, fedheha, kuchekwa, kudharaulika na kushindwa kuamini, kujiamini na kujikubali kwa sababu ya ndoto na mitizamo iliyojaa akilini mwake. Wengi hujiona hapo sio mahali wanapostahili kuwa, kivuli cha degree huwatesa wengi na kwa muda mrefu.
Nimekupata mkuu....

Wasomi wametelekezwa kabisa, tena kuna wengine husema 'elimu' zenu ni mtaji tosha zitumieni kujiajiri....yaani kirahisi tu hivyo, inashangaza sana.

Watunga sera wetu nao wanachangia hili mfano japo halmashauri nyingi zinatoa mikopo ya asilimia 10 ya mapato yao kwa wanawake, vijana na walemavu ila mpaka uzipate hizo hela shughuli yake sio ndogo na huenda hata mkapigwa tarehe tu msipate kabisa.
 
Ninaumia sana nikikumbuka jinsi nilivyokuwa nikiteseka usiku kucha ninasolve hesabu ngumu k.m Laplace transform, abstract algebra, topology, Fourier series, fluid mechanics,rigid body mechanics, advanced complex analysis, data structure, functional analysis e.t.c ili niweze kupata GPA nzuri na nikafanikiwa kuwa na 4.6 ambayo ni first class, lakini nimezunguka mpaka nikanyosha mikono huu ni mwaka wa 10. NINAUMIA SANA MOYONI MWANGU KWA NINI NILIPOTEZA MUDA KIASI HICHO KUHANGAIKIA KUSOMEA DEGREE HII YA .... AMBAYO NINATESEKA KIASI HIKI MTAANI. Hata hivyo Mungu ni mkuu siku Moja serikali watatukumbuka na tutapata ajira
Pole sana mkuu, naelewa vizuri sana unachokipitia.

Mungu ni mwema wakati wako utafika tu haijalishi umesubiri kwa muda gani, amini hilo.
 
Nakuja chumbani kubisha hodi ukisikia hodi fungua,
Ahhhhhh wapi. Na wewe ukileta usenge nakuanika hapa hapa. Mjinga mmoja siku za nyuma amejidai anajua kureply,anajisogezasogeza,anauliza LGBT unawachukuliaje,nkamwambia mi pia huyo huyo,kaingia kichwa kichwa eti anataka picha ya nyeti zangu.

Acha tu tuandike ujinga,JF ilikuwa ya zamani, hapa imehamia ze Comedi.

Sasa na wewe,ukija huko home,njoo kistaarabu
 
Nakuja chumbani kubisha hodi ukisikia hodi fungua,
Sasa iko hivi, hapa kila mtu anaandika utopolo kulingana na mada husika au na wachangiaji. Wahuni wamo sikatai lakini si kila mtu humu ni mhuni. Naomba tuheshimiane, umevuka mipaka.
Kama kusoma na kucomment sawa,huo ubaradhuli hapana usiniletee.
 
Ahhhhhh wapi. Na wewe ukileta usenge nakuanika hapa hapa. Mjinga mmoja siku za nyuma amejidai anajua kureply,anajisogezasogeza,anauliza LGBT unawachukuliaje,nkamwambia mi pia huyo huyo,kaingia kichwa kichwa eti anataka picha ya nyeti zangu.

Acha tu tuandike ujinga,JF ilikuwa ya zamani, hapa imehamia ze Comedi.

Sasa na wewe,ukija huko home,njoo kistaarabu
Mjinga mmoja sio Mimi huyo uminifananisha hivyo haya ingia hivi unaujua ule wimbo wa "hatoki mtu tushaupaka mkongo?"
 
Kuna mbwa na paka wengi mtaani wanazurura.
Wewe Mimi sinaga tabia za kuzunguka mbuyu nimekuja straight to the point km ulivyosema na Mimi nikasema km ulivyosema nini hapo nimekosea?
 
Wanamaliza wahitimu zaidi elfu 20 wa Accounting kwa level ya degree hapa Tanzania kila mwaka, lakini ajira rasmi za kudumu za kuwaajiri (tena za mchongo balaa) hazifiki hata 300 kwa mwaka, hao wengine wanakwenda wapi?

Serikali haajiri wengi na wala haajiri kila mwaka, na taasisi binafsi zenye kuajiri ni chache, kwa uchache sana huajiri, tena huajiri wenye uzoefu mkubwa na mzuri. Sasa mhitimu mpya anavukaje hapo?
Niliona kuna housegirl ana CPA nikashangaa sana kwa kweli.
 
Back
Top Bottom