Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Mnaweza kuwalipa mishahara kwastahiki naambayo inaendelea na hali ya maisha? Serikali hupenda kukimbilia kuajiri graduates wa diploma mfano kwenye afya wana ajiri CO asilimia 60-70 nasio MD kwasababu mishahara yao ni midogo i.e. 650,000/=. Matokeo yake unayajua, hospitaliza wilaya na rufaa kwenda juu zinafurika watu na foleni zisizo na mbele wala nyuma kwasababu zahanati,kituo cha afya na muda mwingine hospitali ya wilaya hazina wataalamu wakufanya procedures na surgeries zinazohitajika kutibu wagonjwa. Naye mwaajiriwa wa diploma haoni kazi yake ya maana bali assurance tu yakupata kitu chakuingiza kinywani kwakuwa anachopewa hakimsaidii kwanjia yeyote ile kufanya maendeleo hivyo hata vituo hubaki empty mchana mpaka usiku na wagonjwa kukosa huduma.
Ukisema unataka hayo unayoyataka hakikisheni pia mpo tayari kupandisha scale ya mishahara yao, hamna mtu anayependa kuitwa cheap labor. Mapinduzi yasiwe kuwafanyisha kazi watu tu bali pia na kuwalipa mishahara inayowatesheleza kulingana na hali ya maisha.
 
Tulikuwa tunajadili masuala ya Elimu na degree we ukakirupuka na upumbavu wako ukatuletea Quran.

Nani kakwambia huu mjadala wa magaidi?
Kwenye mjadala wa elimu unaachaje kuongelea elimu kuu kuliko zote? Elim Akhera?
 
Kwenye mjadala wa elimu unaachaje kuongelea elimu kuu kuliko zote? Elim Akhera?
Tatizo mnatengeneza majini ndomaana mnayajua majina!

Sasa ukiona dini mashekh wake wanatengeneza mpaka majini kama una akili kimbia huko!

Ugaidi lazima upigwe vita!
 
Tatizo mnatengeneza majini ndomaana mnayajua majina!

Sasa ukiona dini mashekh wake wanatengeneza mpaka majini kama una akili kimbia huko!

Ugaidi lazima upigwe vita!
Jini ni kiumbe Cha Allah, mwenye uwezo wa kukitengeneza ni Allah pekee
 
Haya sasa tuambie, inakuwaje karibu 90% ya wahitimu wa degree wako njia panda kusaka ajira na vipato huku wakiambulia patupu?
Ni kwa sababu (kama umenielewa) pamoja na kuwa na technical (hard) skills, hawana soft (21st century) or lifelong skills. Hizi transferrable/employability/soft/21st century skills etc zinazoongeza thamani ya ajira na, hata kama hutaajiriwa kwa sababu watu ni wengi na wanaotakiwa ni wachache, utaweza kujiajiri au kutengeneza ajira. Yaani, mtu mweye skills za aina zote mbili ni marketable zaidi kuliko aliye na aina moja katika dunia ya sasa. Aina hizi za skills ni kama vile critical thinking, communication skills, digital literacy skills, self-management skills, entrepreneurial skills, innovative and creative skills, problem-solving skills, leadership skills, interactive and collaboration skills etc.
 
Bora kusomea kutengeneza simu, au kutengeneza music niwe DJ, kuliko huu upuuzi
 
Jini ni kiumbe Cha Allah, mwenye uwezo wa kukitengeneza ni Allah pekee
Dada usifiche Ukweli! Hapa Magomen, Pale Mywara Kwa Shekh Kingazi majini kama kawaida yanatengenezwa.

Kuna jini Maimuna, jini Makata, jini kibazili n.k usifiche Ukweli! Na majini ni mashetani tu!
 
Dada usifiche Ukweli! Hapa Magomen, Pale Mywara Kwa Shekh Kingazi majini kama kawaida yanatengenezwa.

Kuna jini Maimuna, jini Makata, jini kibazili n.k usifiche Ukweli! Na majini ni mashetani tu!
Kwahyo binaadamu Wana uwezo wa kuumba kiumbe? Una akili kweli wewe
 
Nakazia,
Na mbaya zaidi kama huna wa kukubeba (network) inakuwa shida mno.
Chinua Achebe aliwahi kusema "A common saying in the country after Independence was that it didn’t matter what you knew but who you knew"
 
Njoo nikuoneshe mdogo wangu mmoja mwenye BAF ya IFM na CPA ameamua kufuga ng'ombe wa maziwa Arusha vijijini....lakini ameshajenga na ana maisha tayari

Wenzake bado wanahangaika kusambaza bahasha
 
Elimu ni kutoa ujinga wahitimu waliomaliza wakajiajiri ni tofauti na walio kosa au wenye Elimu ndogo wakajiajiri.
 
ELIMU yetu ilishachezewa sana kitambo lilikuwa suala la muda tu.wahuni walioiharibu Elimu yetu wanaendelea kupeta tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…