Neuro
JF-Expert Member
- May 13, 2017
- 1,551
- 1,721
Mnaweza kuwalipa mishahara kwastahiki naambayo inaendelea na hali ya maisha? Serikali hupenda kukimbilia kuajiri graduates wa diploma mfano kwenye afya wana ajiri CO asilimia 60-70 nasio MD kwasababu mishahara yao ni midogo i.e. 650,000/=. Matokeo yake unayajua, hospitaliza wilaya na rufaa kwenda juu zinafurika watu na foleni zisizo na mbele wala nyuma kwasababu zahanati,kituo cha afya na muda mwingine hospitali ya wilaya hazina wataalamu wakufanya procedures na surgeries zinazohitajika kutibu wagonjwa. Naye mwaajiriwa wa diploma haoni kazi yake ya maana bali assurance tu yakupata kitu chakuingiza kinywani kwakuwa anachopewa hakimsaidii kwanjia yeyote ile kufanya maendeleo hivyo hata vituo hubaki empty mchana mpaka usiku na wagonjwa kukosa huduma.Tunahitaji mapinduzi halisi ya viwanda(industrial revolution), hatuhitaji kuwa na wahitimu wa vyuo vikuu kwa wingi huo, tunahitaji wahitimu wa vyuo vya kati wafanye kazi kwenye viwanda.
Engineer mwenye shahada na mwenye fani yake kwa level ya diploma au cheti, atakayeleta thamani ni mwenye diploma.
Tunahitaji viwanda, otherwise tuna bomb kubwa.
Ukisema unataka hayo unayoyataka hakikisheni pia mpo tayari kupandisha scale ya mishahara yao, hamna mtu anayependa kuitwa cheap labor. Mapinduzi yasiwe kuwafanyisha kazi watu tu bali pia na kuwalipa mishahara inayowatesheleza kulingana na hali ya maisha.