Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Binafsi nilitegemea wakimaliza warudi vijijini kwao wakaboreshe shughuli zinazofanywa na wazazi wao kwa kutumia degree zao.

Haiwezekani na haiingii akilini wazazi wasio na degree wamekabiliana changamoto zote mpk wakafanikiwa kuwasomesha hao wenye degree halafu waageuka kuwa mzigo.

Wajitambue na wajiamdaye kiakili kutatua changamoto za wazazi wao na kuendeleza pale wazazi wao walipoishia
Wakaboreshe shughuli zinazofanywa na wazazi wao kwa namna ipi?

Kilimo ndio shughuli kubwa vijijini, mhitimu anamaliza chuo hana mtaji wowote, unataka aende vipi kuboresha kilimo cha wazazi? kwa njia zipi? awasaidie kulima kwa jembe la mkono?

Suala la wazazi kuunga unga na kusomesha mtoto haliwezi kuwa kipimo kusema wazazi vijijini wanajiweza, ndio maana mtoto anapelekwa shule ili elimu anayoipata ije kumsaidia kuwakomboa wazazi, lakini sio elimu anayoipata kama ya finace au medicine arudi nayo kijijini kulima!.

Kama ni suala la kurudi kijijini kulima wazazi wasingehangaika kupoteza ada kuwapeleka shule watoto wao, wangetulia nao vijijini wawape jembe walime. Pia suala la shisha usilete hapa, elimu ya chuo sio ya watoto, ni ya watu wazima, usiingilie maisha yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ajira na kipato havimilikiwa na mfumo wa elimu
Sasa kama 100% ya vijana wamepambana kusoma ili kupata degree kwa lengo la kujihakikishia ajira na kipato katika maisha yao yote, halafu mwisho wa siku 90% ya hao vijana wameshindwa kupata ajira na vipato kupitia degree zao.

Sasa kwanini tusiseme kusoma kwa vijana wengi ili kupata degree ni upotezi wa rasimali?
 
Community development atajiajiri wapi?
Nurse atajiajiri wapi?

#YNWA
Nliwahi kufanya kazi katika kitaasisi kimoja njaa hapa mjini. Watu wengi tunachukulia kama kuchukulia changamoto na kuangalia Fursa ndani yake kama mzaha.

Innovation still matter!. Kama una utaalam wa jamii na maendeleo. Kuna maeneo maendeleo hayfikii malengo, na changamoto ni nyingi hasa kwenye SSA. Haya maeneno tunahitaj more than having adopted development projects and so.

Shortcut ya ajira kwa sasa ni uvumbuzi na utatuzi wa changamoto za jamii. Whether una mtaji au huna, wenye mitaji wapi na pambania nafas ya kuwafesi mfanye jambo
 
Haya maisha yana siri nyingi mno.

Sio kila .wanaume au mwanamke anaoa au kuolewa.

Sio kila anayefanya kazi kwa bidii anakuwa tajiri.

Hivyo sio kila anayesoma anapata ajira.

Lakini huwezi sema elimu haina umuhimu.

Bado ina umuhimu kwakua kuna ambao wamesoma na wamepata ajira na zimewanufaisha.
Hakuna aliyesema Elimu haina umuhimu.
Mimi ninasema elimu ya degree kwa sasa haina umuhimu wowote wa kuhakikisha ajira au kipato kwa 90% ya vijana.
 
Hamna haja ya kulalamika wakati mnafurahia kufaulisha 100%. Mitihani inatakiwa iwe migumu ili tupate wahitimu wachache wanaohitajika.

Dunia haihitaji watu wengi wenye degree.. inahitaji watendaji, mafundi wengi ambao ni certificate.. na wasimamizi wachache wa kati ambao ni diploma.. degree holders wanaandaliwa kuwa wasimamizi wakuu.. ambao ni wachache zaidi

Tuamshe veta, tuzisurport na kuzichangamkia tutaongea lugha nyingine kabisa
 
Sasa kama 100% ya vijana wamepambana kusoma ili kupata degree kwa lengo la kujihakikishia ajira na kipato katika maisha yao yote, halafu mwisho wa siku 90% ya hao vijana wameshindwa kupata ajira na vipato kupitia degree zao.

Sasa kwanini tusiseme kusoma kwa vijana wengi ili kupata degree ni upotezi wa rasimali?
Ukisema digrii hazifai sabab hakuna ajira. Umefeli kujenga hoja!. Ajira ni sekta ya uchumi, na pia ni suala linaloathiriwa sana na idadi ya watu na structure ya population na pia maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Elimu ya digrii hii hii ya fani yoyote, wanaopata nafas wapo na wanafanikiwa. Think in broader picture
 
Nliwahi kufanya kazi katika kitaasisi kimoja njaa hapa mjini. Watu wengi tunachukulia kama kuchukulia changamoto na kuangalia Fursa ndani yake kama mzaha.

Innovation still matter!. Kama una utaalam wa jamii na maendeleo. Kuna maeneo maendeleo hayfikii malengo, na changamoto ni nyingi hasa kwenye SSA. Haya maeneno tunahitaj more than having adopted development projects and so.

Shortcut ya ajira kwa sasa ni uvumbuzi na utatuzi wa changamoto za jamii. Whether una mtaji au huna, wenye mitaji wapi na pambania nafas ya kuwafesi mfanye jambo
Sasa kwa 90% ya wahitimu wetu wa degree hiyo innovation skill hawana. Kwanini?
Hakuwaandaliwa hivyo vyuoni na hawakusetiwa hivyo kabla ya kwenda vyuoni. Kwa 100% waliaminishwa wanakwenda kusoma degree ili waje kuajiriwa moja kwa moja huku wakipiga pesa kiulaini kwa kutumia vyeti vyao.
 
Ukisema digrii hazifai sabab hakuna ajira. Umefeli kujenga hoja!. Ajira ni sekta ya uchumi, na pia ni suala linaloathiriwa sana na idadi ya watu na structure ya population na pia maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Elimu ya digrii hii hii ya fani yoyote, wanaopata nafas wapo na wanafanikiwa. Think in broader picture
Mimi nimesema, usomi wa degree kwa sasa 90% umeshindwa kufikia malengo (ajira au kipato).

Kama kwa 100% ya vijana walikwenda kusoma degree ili ziwasaidie kirahisi kupata ajira na kipato cha uhakika, halafu baada ya wao kuhitimu 90% wameshindwa kupata ajira au kipato kupitia degree zao, hapo utasemaje?
 
Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.

Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.

1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16. Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.

Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada. Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.

Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!
Mm nashangaa sana mzazi anapambana na kupeleka mtoto akasome degree analipa juu ya 12milion kama ada na cost nyinginezo za maisha harafu badae anashidwa kumwezesha ajiajiri, wazazi niwashauri na vijana ukimaliza certificate au diploma inatosha sana tafta ela kama unataka iyo degree utaipata ukiwa na kipato chako na wazazi wapeni watoto mitaji tuachane na huu ujinga wa urithi wa mtoto ni elimu , kumbuka elimu siyo urithi ni haki ya mtoto hakuna sehemu Duniani elimu ishawahi kuwa urithi Mpe elimu kidogo Mpe na urithi uliomwandalia kama ww mkulima mpeleke huko akapambane nayo tuache ulimbukeni na kuingia kwenye mipango ya wazungu kutufanya tegemezi miaka yote
 
Watu Hawa Somi ili Waajiriwe,
Watu wana fundishwa Kupata Maarifa
Una uhakika na hilo kwa wasomi wa degree?
Okay, sawa wanasoma ili kupata maarifa, sasa inakuwaje baada ya kumaliza wako busy kusaka ajira?
Vipi sasa baada ya kukosa ajira wanarejea kufanya kazi za darasa la saba badala ya kutumia hayo maarifa ya degree zao?
 
Wakaboreshe shughuli zinazofanywa na wazazi wao kwa namna ipi?

Kilimo ndio shughuli kubwa vijijini, mhitimu anamaliza chuo hana mtaji wowote, unataka aende vipi kuboresha kilimo cha wazazi? kwa njia zipi? awasaidie kulima kwa jembe la mkono?

Suala la wazazi kuunga unga na kusomesha mtoto haliwezi kuwa kipimo kusema wazazi vijijini wanajiweza, ndio maana mtoto anapelekwa shule ili elimu anayoipata ije kumsaidia kuwakomboa wazazi, lakini sio elimu anayoipata kama ya finace au medicine arudi nayo kijijini kulima!.

Kama ni suala la kurudi kijijini kulima wazazi wasingehangaika kupoteza ada kuwapeleka shule watoto wao, wangetulia nao vijijini wawape jembe walime. Pia suala la shisha usilete hapa, elimu ya chuo sio ya watoto, ni ya watu wazima, usiingilie maisha yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Umemjibu vizuri sana watu wanaandika andika tu.
 
Sasa kama 100% ya vijana wamepambana kusoma ili kupata degree kwa lengo la kujihakikishia ajira na kipato katika maisha yao yote, halafu mwisho wa siku 90% ya hao vijana wameshindwa kupata ajira na vipato kupitia degree zao.

Sasa kwanini tusiseme kusoma kwa vijana wengi ili kupata degree ni upotezi wa rasimali?
Most of vijana hawakusoma degree hili wapate ajira bali wamesoma kwasababu walifaulu chini na most ambao hawakusoma hawajasoma kwasababu hawakufaulu nukta.
 
Halafu mwisho wa siku baada ya tuhitimu tukashindwa kupata hiyo ajira ya serikali/umma, maana yake ni kuwa degree imefeli kutuvusha
ndio tulikofika, cha kufanya sasa ni kuwa na altenative ways/plan A, B, C yaani wakati unasomea kuajiriwa pia unasoma na kujifunza mambo mengine mengine interested. Ukifeli kuajiriwa tayari una ujuzi wa kujiajiri na maisha yanaendelea kama kawaida. Tusisahau ukulima, ufugaji, biashara/ujasiriamali na ufundi
 
Back
Top Bottom