denoo JG
JF-Expert Member
- Oct 27, 2023
- 2,701
- 9,759
Wakaboreshe shughuli zinazofanywa na wazazi wao kwa namna ipi?Binafsi nilitegemea wakimaliza warudi vijijini kwao wakaboreshe shughuli zinazofanywa na wazazi wao kwa kutumia degree zao.
Haiwezekani na haiingii akilini wazazi wasio na degree wamekabiliana changamoto zote mpk wakafanikiwa kuwasomesha hao wenye degree halafu waageuka kuwa mzigo.
Wajitambue na wajiamdaye kiakili kutatua changamoto za wazazi wao na kuendeleza pale wazazi wao walipoishia
Kilimo ndio shughuli kubwa vijijini, mhitimu anamaliza chuo hana mtaji wowote, unataka aende vipi kuboresha kilimo cha wazazi? kwa njia zipi? awasaidie kulima kwa jembe la mkono?
Suala la wazazi kuunga unga na kusomesha mtoto haliwezi kuwa kipimo kusema wazazi vijijini wanajiweza, ndio maana mtoto anapelekwa shule ili elimu anayoipata ije kumsaidia kuwakomboa wazazi, lakini sio elimu anayoipata kama ya finace au medicine arudi nayo kijijini kulima!.
Kama ni suala la kurudi kijijini kulima wazazi wasingehangaika kupoteza ada kuwapeleka shule watoto wao, wangetulia nao vijijini wawape jembe walime. Pia suala la shisha usilete hapa, elimu ya chuo sio ya watoto, ni ya watu wazima, usiingilie maisha yao.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app