Hivi mfano wa karibu. Watu wanaopelekwa Israel,kujifunza mambo ya kilimo,
1. Hawa watu hawaendi tu hivi hivi. Wanalipwa.
2. Watu hawa hawa, ukija kuangalia,si kwamba kuna vigezo vya kwenda huko,bali connection tu. Ndugu yangu akaonje hela ya serikali.
3. Wakirudi, nani anajua wanakopotelea?
4. Sasa kama wamepelekwa kujiendeleza, af hawana mchango wowote, unategemea huyu huyu ambaye hajafika hata Dar atadai ana uwezo wa kuendelea kilimo?
5. Kwa nini hao wa Israel wasiletwe wakawafikie wenye uhitaji?
6. Ikiwa mifumo ya kiAfrika bado ya kimagumashi,ni ngumu sana.
7. Leo hii Israel inadai inahitaji nguvu kazi kutoka Afrika. Hasa kwenye sekta ya kilimo. Wanalima wakauze nje.
Ni kwamba hayo masoko wanayouza,hayapokei mazao kutoka Afrika?
Je, Israel ina ardhi kubwa na nzuli kuliko ya TZ?
Mfumo wa maisha ndo ulivyo bila kushikana mkono, ni ngumu. Sasa wenye nafasi za kuwapa maisha vijana, wasipotaka, miaka ijayo mtakuta vibaka ni wasomi. Sasa hivi wanaojiuza si wasomi?