Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaua kabisa nafas za watu kufanya kazi. Watu wanazaana sana katika kipindi ambacho Fursa zinazid kuwa finyu.

Leo hii wabeba mizigo hawana ishu sabab ya fokolift. Nyumba zinaprintiwa siku hizi, fundi ujenzi tafuteni chaka mapema. Majiko ya gesi na umeme yanaua sido.

Hii veta pamoja na teknolojia duni Leo inaonekana valid & tentative solution. Miaka yake mitano mbele tu kama haijabadili focus ya teknolojia za kisasa mtaikataa au itabase rural areas tu
 
Mkuu hakuna degree nzuri au mbaya. Hata medicine wapo kitaa wanaendesha bodaboda.

Tatizo kubwa in lipo kwenye mtazamo (mindset) wa wasomi. Wengi mmejengwa na kuandaliwa kupewa ajira. Hapa ndipo penye kosa kubwa.

Lengo la degree siyo kuajiriwa kwenye fani uliyosomea kama mleta mada unavyotaka kutuaminisha. Lengo la degree ni kupanua mawanda ya kufikiri ili msomi aweze kuyakabili mazingira yake kwa namna toauti na asiyesoma.

Kwahiyo ktk nchi kama Tanzania iliyobarikiwa ardhi kubwa yenye rutuba na imezungukwa na mito, maziwa na bahati ni aibu kwa wasomi kuleta mada za kulalamikikia kukosa kuajiriwa. Mlienda chuo kudanga, kubet na kuvuta shisha badala ya kujielimisha. Shubamiti, ndengeleki ninyi!
Kwel nimeamin wew ni sexless. Suala la nchi kuwa na mito na maziwa linahusiana vip na mtu aliyesoma sociology?
 
Enzi nasoma udsm B.A Education nilikua na masomo ya Linguistics & Literature. Kuna washikaji zangu nilikua na share nao course za linguistics wao wakisoma B.A Language studies, nilikua najiuliza hawa jamaa kwa nini wasisome tu education wakatembea tu na masomo ya Linguistics & Literature na ajira ni uhakika mbona ni kitu kile kile na ninachosoma mm. Sasa miaka imeenda utakuka mwingine yuko anapgwa tu maisha shida amezitaka mwenyewe.
Kabisa kabisa..na hii ni kwasababu vyuo haviko serious juu ya hatima ya wanafunzi.

Wao nikukusanya watoto madamu wawe na kakitengo kao basi!

They don't care!
 
Ungekuwa mhitimu wa fani yoyote ya uhandisi ungeamini vizuri mbona ?
Ungekula msoto na kupata first hand experience soon baada ya kugraduate
Hali ni mbaya kwa fani zote ,ni kama soko la ajira lipo kwenye" standstill "mode
Mimi ni mhandisi wa fani moja wapo ya uhandisi ,ila ninafanya issue tofauti kabisa na fani yangu
Pole braza
 
Hivi mfano wa karibu. Watu wanaopelekwa Israel,kujifunza mambo ya kilimo,
1. Hawa watu hawaendi tu hivi hivi. Wanalipwa.
2. Watu hawa hawa, ukija kuangalia,si kwamba kuna vigezo vya kwenda huko,bali connection tu. Ndugu yangu akaonje hela ya serikali.
3. Wakirudi, nani anajua wanakopotelea?
4. Sasa kama wamepelekwa kujiendeleza, af hawana mchango wowote, unategemea huyu huyu ambaye hajafika hata Dar atadai ana uwezo wa kuendelea kilimo?
5. Kwa nini hao wa Israel wasiletwe wakawafikie wenye uhitaji?
6. Ikiwa mifumo ya kiAfrika bado ya kimagumashi,ni ngumu sana.
7. Leo hii Israel inadai inahitaji nguvu kazi kutoka Afrika. Hasa kwenye sekta ya kilimo. Wanalima wakauze nje.
Ni kwamba hayo masoko wanayouza,hayapokei mazao kutoka Afrika?
Je, Israel ina ardhi kubwa na nzuli kuliko ya TZ?
Mfumo wa maisha ndo ulivyo bila kushikana mkono, ni ngumu. Sasa wenye nafasi za kuwapa maisha vijana, wasipotaka, miaka ijayo mtakuta vibaka ni wasomi. Sasa hivi wanaojiuza si wasomi?
Hao wanao enda Israel, Wanakwenda kufanyishwa kazi mashambani kama vibarua cheap labourers, Wakidanganywa kwamba wanaenda field.
 
Hivi mfano wa karibu. Watu wanaopelekwa Israel,kujifunza mambo ya kilimo,
1. Hawa watu hawaendi tu hivi hivi. Wanalipwa.
2. Watu hawa hawa, ukija kuangalia,si kwamba kuna vigezo vya kwenda huko,bali connection tu. Ndugu yangu akaonje hela ya serikali.
3. Wakirudi, nani anajua wanakopotelea?
4. Sasa kama wamepelekwa kujiendeleza, af hawana mchango wowote, unategemea huyu huyu ambaye hajafika hata Dar atadai ana uwezo wa kuendelea kilimo?
5. Kwa nini hao wa Israel wasiletwe wakawafikie wenye uhitaji?
6. Ikiwa mifumo ya kiAfrika bado ya kimagumashi,ni ngumu sana.
7. Leo hii Israel inadai inahitaji nguvu kazi kutoka Afrika. Hasa kwenye sekta ya kilimo. Wanalima wakauze nje.
Ni kwamba hayo masoko wanayouza,hayapokei mazao kutoka Afrika?
Je, Israel ina ardhi kubwa na nzuli kuliko ya TZ?
Mfumo wa maisha ndo ulivyo bila kushikana mkono, ni ngumu. Sasa wenye nafasi za kuwapa maisha vijana, wasipotaka, miaka ijayo mtakuta vibaka ni wasomi. Sasa hivi wanaojiuza si wasomi?
Dah! Umeandika Kwa uchungu sana Mkuu!
 
Ndo maana hatufai kumlaum mtu. Mwalimu anaekufundisha hizo Maths na Physics,mwenyewe ukute hata Airport hajawahi kuiona. Huyo huyo,ndo anaekuaminisha kuwa unaenda kuwa rubani miaka 6 au kumi badae. Akili ya kujiuluza kwa nini yeye hajaenda kuwa rubani,ndo zero. Unategemea nini?
Sasa mwisho wa siku unaamua usepe kijijini ukawaache walime, vijana wanajenga,wanaoa,unabaki mjini kuwa tapeli
Kuna Prof. Mmoja R.I.P tukiwa Darasani UDSM pale nikiwa mwaka wa pili, nilimuuliza kuwa sisi wanafunzi wako tunalalamikia mfumo, na wewe unalalamikia mfumo tena unawalalamikia vijana uliowafundisha ambao Leo ni mawaziri; je nani wa kutusaidia?

Akaniangaliaaaaa, akanambia kua uyaone mwanangu!

Kafa akiwa na kigari Cha hovyo na nyumba haijaisha kisa anasomesha ndugu!
 
Back
Top Bottom