Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Enzi nasoma udsm B.A Education nilikua na masomo ya Linguistics & Literature. Kuna washikaji zangu nilikua na share nao course za linguistics wao wakisoma B.A Language studies, nilikua najiuliza hawa jamaa kwa nini wasisome tu education wakatembea tu na masomo ya Linguistics & Literature na ajira ni uhakika mbona ni kitu kile kile na ninachosoma mm. Sasa miaka imeenda utakuka mwingine yuko anapgwa tu maisha shida amezitaka mwenyewe.
Ni vizuri vijana wanapochagua fani za kusoma washauriwe pia maana vyuo vinafanya biashara tu mengine hayawahusu.
 
Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.

Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.

1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16 . Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.

Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada. Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.

Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!
Law Je
 
Kiukweli mm nafanyakaz tofauti na degree niliyosomea na siikumbuki vzr..nikipewa mtihani napata suduria
Ni usenge sana, wanatuchezea tu akili degree degree Sasa hivi wamerudi na six yaan wamekazia six sababu madogo wanaruka hio wanaenda Diploma basi wamebania hapo tunataka walioenda six au wenye vyeti vya six wakaenda degree jinga kabisa ni usenge kwani wote lazima wapite njia moja ndio maana nasema degree ni usenge ni kwa ajili ya watu wachache wanaofanyiwa michongo mtu anaona kazini ili mshahara upande inabidi aongezee degree ndio anaenda kupata degree akirudi mshahara unapanda Sasa huo si usenge hawa wasio na kazi unawafanyaje?
 
Sasa kuna watu ukiwaambia hayo watakwambia wewe ni mzembe, hajajitambua nk ndio maana hujatoboa kwenye ajira kwa kile ulichosomea. Bado hawajajua maisha ni nini.

Mimi huwa nawaambia, waende wasome, wakishahitimu tutakutana mtaani ndio tuongee ukweli.
Na ukikosa kazi dharau kama zote zinakuhusu, kumbe laiti wangejua....

Watu kama hao ni kuwasamehe tu bure maana hawajui wanachokifanya.
 
Elimu ni uwekezaji mzuri sana tu.

Kama una fursa ya kusoma no vyema uitumie vizuri, usiache kwa kigezo kuwa kazi hakuna.

Halafu hiyo elimu pia inapanua ufahamu wako na inaweza kukusaidia pindi utakapoamua kujikita kwenye sekta zingine za uzalishaji.
Ufahamu bila ya pesa ni upotevu wa muda. Una miaka 35 halafu maisha hayaeleweki lazima utajiona mjinga tu
 
20. Mineral processing engr
21. Bachelor of art with education
22. Fine art and design
23. Statistics
24.Mathematics
25.Physics
26. Civil engr
27. Chemistry
28. Agroeconomy
29. Biochemistry
30. French
31. Arabic
32.
33.
34.
Civil Eng imekukosea nn wee?
Itoe hapo haraka sana
 
Ajira zipo kwa fani zote, na hazipo kwa fani zote kutegemeana na mhusika anayeitafuta, una connection?

Kama connection unayo hata kama una ufaulu mbaya ajira utapata, lakini kama una pass mark nzuri connection hauna umeumia.

So hizo kozi ulizoweka hapo zina ajira na hazina ajira pia kutegemeana na situation ya mhitimu na wazazi wake, au kama akiwa mtoto wa kike akakutana na boss anamemuelewa ajira ataipata, bahati mbaya ukiwa wa kiume....

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ukweli ndo huu hapa.
 
Kuna mtu kamaliza 2010 ila hadi leo hajapata ajira na kuna mwingine kutokea course hiyo hiyo wa 2022 kapata kazi mwaka huo huo.

Kwa hiyo nitakachomwambia mtu yoyote ni

1.kuwa nondo kwenye kile anachokisomea kwa sababu competition ipo stiff. Tena kama unaweza piga Gpa ya kushangaza fanya hivyo maana graduated programs za makampuni makubwa zipo nyingi ila exceptional grades zitakubeba
.

2. Connections connections, kupata mtu wa kukuambia "lete cv kuna gap sehemu flani ni muhimu sana"
.

3. Kuijua career yako mapema. Hili kosa mimi nililifanya pia kwa kusubiri nitoke chuo ndio niingie mjini. Haina formular hiyo, kuna watoto wa chuo unakutana nai kwenye hizi private companies wanapiga kazi na wanapendwa haswa kwa sababu hakuna attachment wala kuwalipa pakubwa. Kwa hiyo hizo likizo wanazopata sio za kulegeza mwili, ingia mjini mapema utengeneze cv na connections kabila hujamaliza chuo
.

4. Ukiwa chuo jichanganye kwenye clubs tofauti tofauti AISEC au YUNA, huko napo huwa kuna connections haswa za zile affiliated Org haswa ukiwa kiongozi na peformer
.
5. Develop soft skills, upo chuo na freedom kama yote. Acha kutumia muda wote kuangalia series. Jifunze hata graphic design, photography, videography, social media management, copywriting na vingine ambavyo vingi vipo YouTube
.
6. Online presence haswa twitter na linkedin, kajichanganye huko, post post vitu vyako. Interact na watu vizuri maana huko napo kuna connections za bure haswa kwa msio na powerful surnames. Onesha uwezo sio unakaa unachekacheka tu
.
uliyafanya haya utakuwa ahead of the game mtaani na kwenye career maana ndio dunia inapoelekea ila graduates wachache wanayajua haya. Sijatunga ila nimeviishi na nimeona kwa watu wengine vikifanya kazi 100%, so, silaumu mtu ila nimewapa elimu kiasi
Ahsantee kwa Somo, at least niliyafanya haya kwa kiasi, leo inasaidia kwa kiasi.
 
Njia pekee ya kutoboa sasa hivi huko vyuoni hakikisha unakuwa kada wa CCM kupitia UVCCM. AIsee ukishaingia huko connection ya kupata kazi ni chapuuuu. Sasa ww jiroge uingie BAVICHA ndio utajua haujui
 
Ninaumia sana nikikumbuka jinsi nilivyokuwa nikiteseka usiku kucha ninasolve hesabu ngumu k.m Laplace transform, abstract algebra, topology, Fourier series, fluid mechanics,rigid body mechanics, advanced complex analysis, data structure, functional analysis e.t.c ili niweze kupata GPA nzuri na nikafanikiwa kuwa na 4.6 ambayo ni first class, lakini nimezunguka mpaka nikanyosha mikono huu ni mwaka wa 10. NINAUMIA SANA MOYONI MWANGU KWA NINI NILIPOTEZA MUDA KIASI HICHO KUHANGAIKIA KUSOMEA DEGREE HII YA .... AMBAYO NINATESEKA KIASI HIKI MTAANI. Hata hivyo Mungu ni mkuu siku Moja serikali watatukumbuka na tutapata ajira
Graph theory, Number theory, partial differential equations, statistical inference etc. Ila kusema kweli Kuna Jambo halipo sawa na Elimu yetu.
 
Back
Top Bottom