Kwa sasa imani, matumaini na mapendo ya watanzania wengi ni CCM pekee

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ndoto, matarajio na matamanio ya Watanzania wengi wa makundi mbalimbali kwa sasa ni katika Chama Imara Sana cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni kutokana na mipango na mikakati yake katika kuwaongoza, kuwatumikia na kuwaletea Watanzania wote maendeleo.

Nchi imefunguka vizuri, biashara imefunguka, kilimo, ufugaji, uvuvi, usafirishaji na miundombinu vimeboreshwa na vimeimarika sana. Upatikanaji wa huduma muhimu kama vile maji, umeme, na afya ni vya uhakika maeneo mengi nchini.

Serikali madhubuti ya CCM inasema na kutenda.

Mambo yanayoendelea ndani ya vyama vingine vya kisiasa nchini, ni aibu na hali ya kukatisha tamaa kabisa.

Hawana hoja tena za kuikosoa au kushauri serikali, hawaeleweki hata wanacholalamikia, hawaelewani wao kwa wao, hawaaminiani wao kwa wao, n.k.

Cha maana zaidi kwao kwa sasa ni kwamba wanajitambulisha vizuri sana kwa migawanyiko baina yao, malumbano na mipasho isiyo na tija kabisa.

Ama kwa hakika, imani na matumaini ya Watanzania yamebaki kwa CCM na serikali sikivu yake, chini ya kiongozi mahiri sana, kipenzi cha Watanzania comrade, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan. πŸ’
 
Unatafuta umaarufu kwa matusi au unajitoa akili? Hii kazi mwachie lucas
kama matusi yanakusaidia yatumie kwa bidii zaidi ili yakusaidie ni uhuru na uamuzi wako πŸ’

ukweli utabaki pale juu bila mbambamba ya mtu yeyote kuhusu CCM πŸ’
 
CCM ndio Chama pekee Cha kitaasisi
 
Mnatumwa?!!
 
WE NI
 
na
Ni wajibu wa chama chochote kilichopo madarakani kuwatumikia wananchi
na ndicho kinafanyika kwa bidii na weledi wa viwango vya juu sana, na ndio maana matumaini na matarajio ya waTanzania ni makubwa mno kwa CCM na kwakweli ni ya uhakika zaid kwa serikali sikivu iliyopo madarakani πŸ’
 
Kukubadili mindset kwako ni ngumu,inaonekana Bado unavaa pekosi na layzon!
muhimu zaid ni kazi ya CCM kwa waTanzania inafanyika vizur sana kupitia serikali yake, na hivi sasa matumaini yao dhidi ya CCM yamekua makubwa kupindukia πŸ’
 
Vijana wengi wenye njaa tz wamegundua chaka la kujipatia umaarufu kuelekea kwenye teuzi, shida ni connection.

Wengine wanapanua midomo usiku na mchana lakini wapi hata ubalozi tu wa nyumba kumi hakuna. Hii yote iinatokana na kukosa kazi muhimu ya kuwaingizia vipato na ndo maan hata kuoa wengi wao wameshindwa sababu hawana nyuma wala mbele maan mwanamke hali wala kuvaa maneno ya siasa uchwara ya kujipendekeza tena kwa mwanaume mwenzio. Poleni sn vijana wa tz.
 
Ha ha ha ha ebu fanya kazi za elimu yako mkuu haya ya siasa waachie MEMKWA wapambane nayo. Au na wewe ni mnafiki mkuu. Km ni ndiyo basi kazi hiyo inakufaa
ile kazi ambayo daima siwezi choka wala kukata Tamaa hata kidogo ni kusema ukweli wa hali halisi ya mambo.....

hii ingine ya porojo na stori za pata potea ni wengine wafanye....

ile ya maana zaid ni waTanzania walio wengi imani na matumaini yao ni kwa CCM, right πŸ’
 
mbona fursa bwerere tu hivi sasa iweje unababaike?

biashara inalipa, kilimo ufugaji kulipa ni uhakika zaid. kwanini usifanye bidii hizo unazosubiri ambazo hazina uhakika zikakukuta uko njema kiuchumi πŸ’

imeandikwa alienacho ataongezewa πŸ’

ama hawakupitia hapa aise
hapahttps://www.jamiiforums.com/threads/kwa-mara-ya-kwanza-nathubutu-kugombea-ubunge.2205618/
 

..hayo unayoyaongelea ni matokeo ya sera mbaya, na uongozi mbovu wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…