Kama kweli kuna mabaya hayo aliyoyafanya Magufuli, taifa linaweza kunufaika kujifunza, kwa mfano, kuwa na vetting process kali watu wenye rekodi mbaya wasiruhusiwe na vyama vyao kugombea uongozi.
Kuhusu kumuandia Samia, inaonekana wewe mwenyewe hujaelewa maana ya maneno uliyoyaandika.
Umeandika hivi.
"Wapinzani ni kama vile Bado wanaumizwa sana na marehemu kuliko hata mambo yanayoendelea kwenye awamu hii,"
Kama unaona mambo yanayoendelea kwenye awamu hii yana umuhimu zaidi ya kumuandika marehemu, hujakatazwa na wewe kuyaandika, yaandike tu, tutanunua kitabu.
Kwa nini unalazimisha wengine waandike unavyotaka wewe wakati na wewe una uwezo wa kuandika unavyotaka wewe?
This is a false dichotomy fallacy, kwamba ukiandika mabaya ya Magufuli basi hujachukizwa na mabaya ya Samia.
Watanzania wengi wanafanya ujinga huu wa lazima uwe team Magufuli au team Samia, bila kujali kwamba kuna watu wengi wanaona wote wawili ni majanga, tofauti yule alifanya majanga huku akitukana, huyu anafanya majanga huku anarembua macho.
Kabendera kasema kaandika vitabu viwili, kingine kitatoka. Unajuaje hicho cha pili si cha Samia?