Kwa sasa kuna kila dalili Kamala Harris huenda atamshinda Trump kirahisi kabisa!

Wamarekani wanataka rais wnayeheshimu haki za watu na binadamu mfano ushoga, uhuru wa watu kuishi na kuhamia Marekani, uhuru wa kutoa mimba n.k. Yote haya Trump anayakataa.
Trump ndio Republican nominee wa kwanza kuleta ma-gay kwenye RnC mpaka wenye chama wakamshangaa 2016..jina lake anaitwa Peter Thiel. Rafiki yake Trump mkubwa ni lile transvertite Caitlin Jenner na anacheza naye golf mara kwa mara

Trump ni protectionists not an imperialist na hapo ndipo anapopigwa vita.

Vyama vya Marekani vinakuwa controlled na donors ambao ni ma-CEO wa makampuni makubwa. Wao ndio wanahamasisha uhamiaji in the disguise of free trade because Wanalipa wahamiaji ela ndogo uki-compare na wazawa..Jamaa hataki vita za kijinga ndio maana anapigwa vita,donors wa hivi ni watengeneza silaha za kivita..angalia Lloyd Austin alifanya kazi wapi kabla ya kuwa waziri wa Ulinzi..trade immigration,zimeharibu maisha ya wazawa na hapo ndipo kampeni yake ilipoanzia..haya mambo ya uchoko na utoaji mimba anaji-force kuyabeba ila hayaamini kwasababu anahitaji kura za evangelicals ndio kisa cha kumchagua Mike Pence mara ya kwanza
 
Tatizo jinsia ya 'KE' hawapendanagi na kuwaza kuinuana wao kwa wao.Duru ziliarifu Bi Hillary Clinton aliangushwa na Wanawake wenzie...ila walivyokuwa wana demuka na kujaa kwenye mikutano yake ya kampeni sasa!Kumbe wanamuzodoa rohoni:Kura waka mnyima.Ni kama Tanzania tu,Samia hatapata kura za Wanawake akigombea labda Viongozi wa UWT kama JOKATE na wenzake wa juu huko:Hata JF tu..Mfuatilieni- FAIZAFOX komenti zake pale anapo pandisha nyuzi Waziri DR.DOROTH GWAJIMA,anavyokuja kasi na kumpa makavu......!
 
ni wabaguzi tu wanaomuelewa, kura za maoni zinambeba Kamala. Trump atashindwa ni msela tu hana kaliba wala sifa za kuongoza nchi kubwa, mf kwenda Korea kaskazini na kupokewa na maafisa iliwakera sana raia wake
Kura za maoni zipi? Hizo za CNN?
Hivi kuna watu tangu mdanganywe na mauongo mliyolishwa kuhusu Trump bado mmekwama kwenye hilo tope? Uzuri kila anayetoka kwenye hilo tope hutoka kwa jitihada zake, hakuna wa kukukeamua ni juu yako
 
Usipate tabu mkuu zile katuni maarufu zilishatabiri trump president hawajawahi kukosea walitabiri kifo cha malkia wa uingereza wakatabiri maafa walitabiri corona kiufupi zile katuni ni za watu wa system huyo mama muunga mkono mashoga muache akampikie mumewe kwanza.
Umeongea vizur mkuu. Kamala, hawezi kumshinda mnyama Donald. Labda mtoa mada hapo juu, hajui vision na mission , na pia trend za dunia. Digital currency ndio Donald anatakiwa kuinua na sio huo ushoga.Na jana mnyama alikuwa, kwenye conference ya Bitcoin.
 
Nakumbuka Mtabiri Maarufu wa Bulgaria Baba Vanga ulimtabiria Trump but na kitakachotokea pia alikisema...!
 
Kinyang'anyiro cha mbio za urais huko Marekani kimeshika kasi, na upepo wa kisiasa ukibadilika karibu kila wiki. Na sasa habari kubwa ni kuhusu Kamala Harris kuanza kuuvuta upepo wa kisiasa kuibeba Democrat.

Tangu mwanzoni Kamala Harris hakupewa nafasi yoyote ya kuwa mbadala wa Biden. Biden alipoanza kupoteza uungwaji mkono bado Kamala Harris hakupewa faida ya kuwa mbadala wa Biden na hata mara baada ya Biden kuhitimisha mbio zake na kutangaza kuachia ngazi huku akimpendekeza Kamala Harris kuwa mbadala wake bado watu wengi walikuwa na wasiwasi wa Kamala Harris kama ataweza kupambana na Trump na wengi wakisema wanasubiri kwanza kinyang'anyiro cha wagombea wa Democrat kifikie mwisho ili kujua nani ataweza kupitishwa!

Wiki moja tu baada ya Kamala Harris kutangaza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mbio za urais wa Marekani kwa tiketi ya Democrat tayari mawimbi ya bahari kwa upande wa Democrat yameanza kutulia na upepo umeanza kuvuma kwa kasi nzuri kumbeba mwanamama Kamala Harris. Hili halijatokea kwa bahati mbaya, lina sababu zake, na hapa tutalijadili.

Hizi ndio sababu za kwanini Kamala Harris huenda akamshinda Trump kirahisi tofauti na vile isivyotegemewa.

1. Wamerekani wengi bado wana imani kubwa na Democrat na mgombea yoyote kutoka Democrat wangeweza kumuunga mkono. Na huo ni mtaji mzuri wa Kamala Harris. Hali ni tofauti kwa Republican ambapo wanaamini bila Trump huenda republican isiambulie ushindi, hivyo yoyote mwenye nguvu, sifa na uwezo wa kukabiliana na Trump kwenye siasa za majukwaani basi automatically anawashinda Republican, na mwelekeo wa siasa za majukwaani kwa siku hizi chache unaonekana kuwa na neema kwa Kamala Harris.

2. Kamala Harris amepata bahati kubwa ya kuingizwa kwenye kinyang'anyiro kwa lazima na kupewa uungwaji mkono wa moja kwa moja na wademocrat wengi kabla ya kupitishwa kwenye misukosuko ya kuchuana na kuchafuana vilivyo na wagombea wengine wa Democrat katika kinyang'anyiro cha kuteuliwa. Inavyoonekana ni kama wademocrat wote wameamua wambebe Kamala Harris ili washinde. Siku zote umoja ni ushindi.

3. Wapiga kura wazuri na wenye kuamua mshindi wa kiti cha urais wa Marekani ni watu wenye msimamo wa wastani ambao wengi wao hawampendi Trump na walianza kupoteza imani kwa Biden kwa sababu ya matatizo ya uzee wake. Ujio wa Kamala Harris umewaamsha upya na kuwapa nguvu ya kwenda kupiga kura. Hii ndio habari njema kwa Democrat.

4. Wamerekani wengi huwa wanajivunia na kufurahia mnoo kuwa na Rais mwenye sifa, mwelekeo na mvuto katika ulimwengu wa kimataifa, wao huamini Rais wao ndio kioo cha kuwatambulisha wamerekani wote kidunia. Na katika hili wanataka kuthibitisha kwa kuwa na Rais wa kwanza mwanamke tena mwenye asili ya uafrika na uhindi ambaye ni Kamala Harris. Tofauti na hivyo itabidi wampe kura mtu mwenye sifa za utambulisho wa uhalifu na ubaguzi, yaani Trump.

5. Hoja zote za Republican zilizowapa positive political milleage dhidi ya Biden za Uzee, usahaurifu na udhoofu zimekufa kifo cha Mende. Kwa sasa inabidi Trump na Republican watengeneze agenda mpya za kutrend kwa kuwa katikati ya vita wamebadilishiwa adui ambaye yuko tofauti na adui wa mwanzo. Kwa sasa kibao kimebadilika, wamerekani wameanza kuhoji uzee, usafi wa kimaadili na utimamu wa Trump kama unastahili kukalia kiti cha urais wa Marekani.
Kamala atashinda Popular votes za Wananchi ila kimbuka tycoons wa USA wana chombo inaitwa Electoral college,hapo ndipo Trump atakapochukua nchi kama ilivyokuwa kwa Hillary Clinton!!
 
Wamarekani watafanya kosa jingine kumweka huyo mwanamke tena kosa kubwa sana ...mwanamke hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi hata akiwa na elimu kiasi gani maana tatizo kuu la mwanamke yoyote ni kukosa AKILI NA ROHO SHUPAVU YA UONGOZI
 
Wamarekani wanataka rais wnayeheshimu haki za watu na binadamu mfano ushoga, uhuru wa watu kuishi na kuhamia Marekani, uhuru wa kutoa mimba n.k. Yote haya Trump anayakataa.
Pamoja na hayo Trump atakuwa raisi wa marekani ila ataongoza kwenye mazingira magumu sanaaaa maana kwanza kuna next pandemic pili kuna global economic crisis vyote hivyo vitamkuta yeye akiwa raisi.
 
Tatizo jinsia ya 'KE' hawapendanagi na kuwaza kuinuana wao kwa wao.Duru ziliarifu Bi Hillary Clinton aliangushwa na Wanawake wenzie...ila walivyokuwa wana demuka na kujaa kwenye mikutano yake ya kampeni sasa!Kumbe wanamuzodoa rohoni:Kura waka mnyima.Ni kama Tanzania tu,Samia hatapata kura za Wanawake akigombea labda Viongozi wa UWT kama JOKATE na wenzake wa juu huko:Hata JF tu..Mfuatilieni- FAIZAFOX komenti zake pale anapo pandisha nyuzi Waziri DR.DOROTH GWAJIMA,anavyokuja kasi na kumpa makavu......!
Huyo mjinga faizafoxy hampendi dr dorothy kwasababu ni mkristo...ashawahi kuandika humu kuwa samia ni muumini mwenzie
 
Umeongea vizur mkuu. Kamala, hawezi kumshinda mnyama Donald. Labda mtoa mada hapo juu, hajui vision na mission , na pia trend za dunia. Digital currency ndio Donald anatakiwa kuinua na sio huo ushoga.Na jana mnyama alikuwa, kwenye conference ya Bitcoin.
Mshikaji wake Roberts Roberts kiyosaki anashangilia tu mdaa mwamba anarudi ili waendelee kupiga ma dili.
 
Trump ndiye m'beba maono ya dunia kwa sasa . Trump ndiye rais ajaye wa marekani.
 
Mkuu pandemic ya nini tena? Korona inarudi?
Mkuu kuna next pandemic inakuja na hata Viongozi wakubwa wa dunia washasema na ndo maana if unafuatilia itakuwa ushasikia kitu inaitwa virus X yaan wanajaribu kuona je itakapokuja next pandemic mifumo yao imejiandaaje kukabiliana na hilo. Na kibaya ni kwamba hiyo next pandemic ni mbaya mnooo corona cha mdoli tu.
Mkuu kuna anguko kubwa mnooo la uchumi pia linakuja.
Najua kuna watu wataniona juha bin hamnazo ila yatakapotukia tutakumbushana
 
Back
Top Bottom