Kwa sasa kuna kila dalili Kamala Harris huenda atamshinda Trump kirahisi kabisa!

Kwa sasa kuna kila dalili Kamala Harris huenda atamshinda Trump kirahisi kabisa!

Pamoja na umri wake lakini Trump bado yuko vizuri sana kichwani. Haya uliyoorodhesha ni kujikwaa kunakoweza kufanywa na mtu yeyote hata mwenye umri mdogo. Ukitaka kujua Trump yuko vizuri basi lile jaribio la kutaka kuuawa lilianika kila kitu. Aliweza kufirikiri na ku-react kwa haraka na kwa namna ambayo inatakiwa. Japo marais huwa wanafundishwa wafanye nini linapotokea tukio kama lile, lakini kwa umri wake na kwa namna alivyofikiri kwa haraka, bado yuko vizuri kichwani.
Yuko vizuri kichwani kumshinda nani Sasa? Anamzidi Akili Kamala aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa USA?
 
🤣🤣🤣 we bhn fuatilia siasa zako za bongo.. marekani waachine wenyewe..

Mdahalo mmoja tuu ushatoa mshindi 🤣🤣 hirrary alishinda midahalo yote ila ikulu aliiona kwny picha tuu
 
Kinyang'anyiro cha mbio za urais huko Marekani kimeshika kasi, na upepo wa kisiasa ukibadilika karibu kila wiki. Na sasa habari kubwa ni kuhusu Kamala Harris kuanza kuuvuta upepo wa kisiasa kuibeba Democrat.

Tangu mwanzoni Kamala Harris hakupewa nafasi yoyote ya kuwa mbadala wa Biden. Biden alipoanza kupoteza uungwaji mkono bado Kamala Harris hakupewa faida ya kuwa mbadala wa Biden na hata mara baada ya Biden kuhitimisha mbio zake na kutangaza kuachia ngazi huku akimpendekeza Kamala Harris kuwa mbadala wake bado watu wengi walikuwa na wasiwasi wa Kamala Harris kama ataweza kupambana na Trump na wengi wakisema wanasubiri kwanza kinyang'anyiro cha wagombea wa Democrat kifikie mwisho ili kujua nani ataweza kupitishwa!

Wiki moja tu baada ya Kamala Harris kutangaza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mbio za urais wa Marekani kwa tiketi ya Democrat tayari mawimbi ya bahari kwa upande wa Democrat yameanza kutulia na upepo umeanza kuvuma kwa kasi nzuri kumbeba mwanamama Kamala Harris. Hili halijatokea kwa bahati mbaya, lina sababu zake, na hapa tutalijadili.

Hizi ndio sababu za kwanini Kamala Harris huenda akamshinda Trump kirahisi tofauti na vile isivyotegemewa.

1. Wamerekani wengi bado wana imani kubwa na Democrat na mgombea yoyote kutoka Democrat wangeweza kumuunga mkono. Na huo ni mtaji mzuri wa Kamala Harris. Hali ni tofauti kwa Republican ambapo wanaamini bila Trump huenda republican isiambulie ushindi, hivyo yoyote mwenye nguvu, sifa na uwezo wa kukabiliana na Trump kwenye siasa za majukwaani basi automatically anawashinda Republican, na mwelekeo wa siasa za majukwaani kwa siku hizi chache unaonekana kuwa na neema kwa Kamala Harris.

2. Kamala Harris amepata bahati kubwa ya kuingizwa kwenye kinyang'anyiro kwa lazima na kupewa uungwaji mkono wa moja kwa moja na wademocrat wengi kabla ya kupitishwa kwenye misukosuko ya kuchuana na kuchafuana vilivyo na wagombea wengine wa Democrat katika kinyang'anyiro cha kuteuliwa. Inavyoonekana ni kama wademocrat wote wameamua wambebe Kamala Harris ili washinde. Siku zote umoja ni ushindi.

3. Wapiga kura wazuri na wenye kuamua mshindi wa kiti cha urais wa Marekani ni watu wenye msimamo wa wastani ambao wengi wao hawampendi Trump na walianza kupoteza imani kwa Biden kwa sababu ya matatizo ya uzee wake. Ujio wa Kamala Harris umewaamsha upya na kuwapa nguvu ya kwenda kupiga kura. Hii ndio habari njema kwa Democrat.

4. Wamerekani wengi huwa wanajivunia na kufurahia mnoo kuwa na Rais mwenye sifa, mwelekeo na mvuto katika ulimwengu wa kimataifa, wao huamini Rais wao ndio kioo cha kuwatambulisha wamerekani wote kidunia. Na katika hili wanataka kuthibitisha kwa kuwa na Rais wa kwanza mwanamke tena mwenye asili ya uafrika na uhindi ambaye ni Kamala Harris. Tofauti na hivyo itabidi wampe kura mtu mwenye sifa za utambulisho wa uhalifu na ubaguzi, yaani Trump.

5. Hoja zote za Republican zilizowapa positive political milleage dhidi ya Biden za Uzee, usahaurifu na udhoofu zimekufa kifo cha Mende. Kwa sasa inabidi Trump na Republican watengeneze agenda mpya za kutrend kwa kuwa katikati ya vita wamebadilishiwa adui ambaye yuko tofauti na adui wa mwanzo. Kwa sasa kibao kimebadilika, wamerekani wameanza kuhoji uzee, usafi wa kimaadili na utimamu wa Trump kama unastahili kukalia kiti cha urais wa Marekani.
Muwage na akiba ya maneno,
Leo hii upepo umerud tena kwa trump kwan duru zote za makisio ya uungwaji mkono na kura za kimtandao zinamuweka juu trump dhidi ya harris…

Pili : Usidhani marekani ni Tz, hawana imani kihivyo na jinsia ya kike eti awe kiongozi wa nchi. Rejea uchaguzi wa 2016 highest politician profile ya hillary haikumsaidia kumuangusha huyo unaemuita muhuni na mhalifu…

Hizo n chuku na baguzi za mtu mweusi kumuunga mkono mwny asili yake, eti alipitia misukosuko ya kura za maoni…

Usichokijua n kwamba harris alipita bila kupingwa kwan hakuna aliejitokeza kuchuana nae kwny kinyanganyilo cha kupeperusha bendera ya democratic..

Broo sukuma ndani beyonce, T - swift, cjui adele, niki minaji na bikini nyingine unazo zijua wewe,,, bt Trump atawala kisamvu cha kopo mapema sn…

Cz America need strong leader to make them stay stronger and harris cant fit the position
 
Rais WA USA huchaguliwa na majombo 6 yenye nguvu ya electorate college votes zinazotokana na popular vote na replican hushinda Mara Kwa Mara hayo majimbo.....trump atashindaa
Mwambie huyo mlima mwani…..
Maana anaendeshwa n hisia n sio uhalisia
 
Back
Top Bottom