Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Hii wiki imekua Ni vilio kwa watu kila mahali,

Wengi wameondolewa tarrif zero, na Hakuna maelezo ya kueleweka.

Tumezoea ukizidisha matumizi ya unit 70 kwa mwezi, automatically system inakuondoa tariff zero (umeme wa 1,000= unit 8.4)
Kwa sasa unaondolewa tu kwa lazima hata Kama ujazidisha.

Mtu Hana tv Wala redio, anatumia balbu 2 tu na simu kaondolewa tarrif zero. Akitaka kununua umeme UNAGOMA afu anaambiwa "unatakiwa upate key change".

Sijajua ndo ukusanyaji mpya wa mapato ya serikali kwa kulazimisha watu wengi watumie tarrif 4 (umeme wa 1000= unit 2.9) au Kuna kitu kingine pembeni kinaendelea TUFAHAMISHWE.

Kwa maana tangu huu mwezi uanze, vijana wa Tanesco wamekuwa wakipita nyumba Hadi nyumba mara kwa mara, wakidai wanakusanya takwimu za mita za luku.
 
Hii wiki imekua Ni vilio kwa watu kila mahali,

Wengi wameondolewa tarrif zero, na Hakuna maelezo ya kueleweka....
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenyw kundi la matumizi ya viwanda.
Je hizi taarifa ni za kweli?
 
kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.
Hapa ndio kuna point ndugu mkata umeme..
Kwahio Yawezekana ukawa unamatumizi madogo yenye kukupa sifa za kua katika zero tarif ila kwa sababu upo katika eneo lililozungukwa na watumiaji wakubwa basi unaondolewa kwenye zero tarif?

Pia naomba kujua, hivi tunavyoita zero tarif ni sahihi?, Nijuavyo ndio ni tarif ila sio ZERO, ninachojua zero halipii chochote ambapo kwenye nchi zetu hio haipo.
 
Hapa ndio kuna point.

Kwa wateja wote wa maeneo ya mijini wanapaswa kuwa Tarifa 1 ambayo ni matumizi ya nyumbani hadi unit 7500 kwa mwezi, wateja wa maeneo ya vijijini wanapaswa kuwa tarif 1 au tarif D1 kutokana na wastani wa matumizi yao wao wanaozidi wastani wa manunuzi ya unit 75 kwa miezi mitatu mfululizo wanakuwa T1 na wale ambao hawazidi na wapo vijijini wanakuwa D1.
 
Mimi mwezi huu nilinunua umeme mara mbili kwa bahati mbaya. Maana niliponunua ule wa units 75 kwa TZS. 9150 system ya bank ilionesha ime-fail hivyo ikabidi nihamie m-pesa.

Kulipa ile ya m-pesa ikaniletea units kidogo, kumbe system ya bank ilikuwa imekata kimya kimya!

Hivyo nasubiri mwezi ujao nione kama watakuwa wameniondoa kwenye hiyo ya TZS. 9150 kwa units 75.
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenyw kundi la matumizi ya viwanda.
Tunaomba kujua utaratibu wa kumuweka mtumiaji hiyo tarrif ya chini.

Eneo namanyere nkasi Rukwa.
Matumizi ni chini ya unit 15 kwa mwezi.

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Kwa wateja wote wa maeneo ya mijini wanapaswa kuwa Tarifa 1 ambayo ni matumizi ya nyumbani hadi unit 7500 kwa mwezi, wateja wa maeneo ya vijijini wanapaswa kuwa tarif 1 au tarif D1 kutokana na wastani wa matumizi yao wao wanaozidi wastani wa manunuzi ya unit 75 kwa miezi mitatu mfululizo wanakuwa T1 na wale ambao hawazidi na wapo vijijini wanakuwa D1.
Ahaa nilikua sijui, kumbe kuondolewa zero tarif ni mpaka uzidishe matumizi miezi 3 mfululizo mi nilijua ni mara moja tuu na ni automatic.

Kwahio kumbe ni kweli tukiita tarif zero tunakosea..

Swali jingine, kwa mtumiaji wa hio tarif 1/D1 je ana limit ya kiwango cha juu cha MANUNUZI ya umeme?

Yaani kimfano yeye anatakiwa asizidishe matumizi ya unit 75 kwa mwezi ambapo lets say ni tsh 9000, Jee akinunua umeme lets say wa 30,000 lakini matumizi bado yakwa chini ya unit 75, Anaweza ondolewa kwenye taarif D1? Kuna mtu tulibishana sana.
 
Elimu bure, flyovers, mishahara, barabara za lami, ndege, SGR, Bwawa la Nyerere, madawa, madaraja, mwendokasi, njia nane e.t.c. vinahitaji kulipiwa na sisi wenyewe.
KULIPA KODI NI WAJIBU WA KILA MWANANCHI.
 
Tanesco kwann msingeset mita zenu ziwe na uwezo wa kutambua matumizi ya umeme kwa kipindi fulani mfano Kama matumiz yake ya umeme kwa miez mitatu mfulizo n chini ya unit 75 bas mita automatic imrudishe kwenye hiyo tarif zero

Na Kama matumizi yanazid kwa unit 75 bas mita impelekee tarif ya juu zaid hii ingepunguza hyo mosongamano ya kuja huko kwenu kijazana maofisin

Inawezekana labda teknolojia yenu ipo chini lakn mnaweza kuanza taratibu had mkamaliza nchi nzima

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom