Kwa sasa ni nadra sana kuwakuta hawa viongozi wapo Dodoma Makao Makuu, wote imekuwa ni njia moja Dar

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Yaani kwa sasa ni nadra sana kuwakuta hawa viongozi wapo Dodoma makao makuu - wote imekuwa ni njia moko Dar - Magari yenye bendera za Mawaziri na Watendaji wengine wa Serikali wamerudi Dar kwa kasi kubwa mno. Yaani haipiti saa tatu ukiwa Morogoro kila siku unaona gari la kiongizo liko spidi kutoka au kwenda Dar na Dodoma. Matrafiki siku hizi hawana hata mpango wa kuyasimamisha tena. Wamechoka wanaangalia tu.

Gharama hizo za magari kukimbia njia ya Dar Dom ninaona ni kuwa mno kiasi kwamba angekuwepo Mwendazake isingekuwa hivi - wengine hadi juzi wamediriki kuamua kurudisha Ofisi zao Dar - Waziri yule kaitoa Ofisi Moro kuipeleka Dar badala ya Dodoma. Ninamkumbuka sana Mwendazake jamani!

Hivi leo hii tukiitisha roll call ya Viongozi Dodoma ni Mawaziri na Wanaibu Waziri na Makatibu Wakuu wangapi watakuwepo Dodoma leo?
Kumbuka juzi tu karibu wote walikuwa Dar kwa Sabasaba - leo Ijumaa tayari wanne wamepanga ndege na kuna magari zaidi ya 6 yanaelekea Dar now bila hata sababu yeyote. Pumzika kwa Amani Mwendazake! Tumekumiss sana sana!
 
Tatizo liko kwa msimamizi
 
Dawa ya mambo ya hovyo hovyo katiba mpya na sii mtu au mamlaka ndani ya Katiba ya sasa.Hivyo ikiwa unakereka na haya unga mkono juhudi za kizalendo,mwendo ni katiba mpya dawa ya mambo mbofumbofu.
 
Hayo ni matunda ya utawala wa kiimla ya dikteta Magufuli. Watendaji walijaa unafiki mtupu. Watu waliacha kufanya kazi kufuata miongozo na wakawa busy kumridhisha Magufuli huku wakitesa watanzania.
 
Dawa ya mambo ya hovyo hovyo katiba mpya na sii mtu au mamlaka ndani ya Katiba ya sasa.Hivyo ikiwa unakereka na haya unga mkono juhudi za kizalendo,mwendo ni katiba mpya dawa ya mambo mbofumbofu.
Huwa nawashangaa sana watu wanaodai katiba mpyaa...mnashindwa kujua shida iko wap..hata ukiwa na katiba bora kama nn..bila kuwa na watu wanaoiheshimu ni kaz bure..katiba haijindeshi yenyewwwe..wapo watu wanaisimamia hiyo katiba..kama hao watu ni hovyoo baas wataikanyagaa tu hiyo katibaaa...hivyoo kinatakiwa ni mind set za hao watu zibadilike hapo ndipo katiba itasaidia..la sivyo ni kutwanga maji kwenye kinu..
Hii iliyopo tu inasiginwaa mchana kutwaa..
 
Wewe endelea kuwashangaa ukimaliza utarejea humu.
 

..uamuzi wa kuhamia Dodoma ulikuwa mbaya na wa kulazimisha.

..hatukupaswa kujenga makao makuu mengine wakati tulikuwa na makao makuu yanayojitosheleza hapa Dsm.

..sio kweli kwamba makao makuu ya nchi yanapaswa kuwa katikati ya nchi husika.

..Afrika Kusini kila mhimili una makao yake makuu.

..Executive wako Pretoria, bunge wako Cape Town, na mahakama wako Bloemfontein.

..Fedha tulizotumia kujenga Dodoma zingeweza kuelekezwa ktk sekta ambazo zinagusa maisha ya wananchi kama afya, elimu, maji, etc.
 

..naomba kutofautiana na wewe.

..katiba iliyopo sasa hivi inayo mianya mingi inayotoa fursa kwa viongozi kuikanyaga.

..katiba yetu haiwalindi wale wanaotaka kuitetea. Katiba inalinda wasiofuata sheria.

..vilevile katiba hii ina misingi ya mfumo wa chama kimoja wakati tuko ktk mfumo wa vyama vingi.
 
Wewe endelea kuwashangaa ukimaliza utarejea humu.
kwan unateseka?

Sent using Jamii Forums mobile app
KKa
kwan unateseka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni mnufaika lazima uone mwenye mtazamo tofauti na manufaa uyapatayo kama ni tatizo kwako.
 
LOooo, wewe unasubiri 'mindset' zibadilike, na hata hujisumbui kueleza 'mindset' za nani na zitabadilishwa na nani?
Kama mawazo kama haya siyo maajabu sijui tuyaite ni kitu gani hicho!

Yaani hoja nzima ni ya ajabu kabisa: katiba isibadilishwe, isubiri 'mindset' zibadilishwe!

Kwa nini usiangalie angalao uwezekano wa hiyo katiba mpya ndiyo iwe chachu ya kubadilisha 'mindset' za watu kuithamini hiyo katiba, na kujitahidi kuilinda isikanyagwe hovyo hovyo na watawala?
Hili kwako hulioni kuwa na maana yoyote; umejikita tu kwenye 'mindset'!
 
Magufuli hayupo tena , cha muhimu ni kuipata katiba mpya, msiongee kama kwamba Magufuli na familia yake ndio walikua katiba ya Nchi, HAPANA, Magufuli alikua kiongozi wa nchi na alishaenda zake, tuliobaki ndio inatupasa kuisaka katiba mpya vinginevyo tuna safari ndefu sana.
 
Kama uko makini kwenye siasa za kimataifa unaweza fahamu nani mwenye nguvu kati ya katiba ya nchi na rais alieko madarakan..naomba urejelee utendaji kaz wa trump aliekuwa rais wa marekani..pamoja na kwamba wamarekani wengi wako vzur kichwani haswa kwenye masuala la nchi yao na katiba..lakin kichaa trump aliwatingisha kweli kweli had wakanyoosha mikono..sembuse haka ka nchi kalichojaa mazwazwaa kila kona..nakuhakikishia hata hiyo katiba iwejee rais kama hana heshima na ustaarabu kwenye ubongo wake ataikanyaga mchana kweupe na hatafanywa kitu
 
Nigeria, Malawi wamejenga na kuhamia makao makuu mapya, kama kutaja mifano kunasaidia kuwekea uzito hoja.

Uamzi wa kufanya Dodoma kuwa makao makuu ya serikali haukuwa na hauna ubaya wowote. Dar es Salaam itaendelea kuwa kituo kikuu cha biashara, sioni tatizo liko wapi.

Hawa viongozi inatakiwa watulizane tu wafanye kazi za wananchi hapo hapo Dodoma.

Moja ya historia mbaya inayoweza kumwandama Samia ni huku kuhangaika na safari za kila siku kwenda Dar es Salaam, na atakaporuhusu na mawaziri wake waige tabia hiyo, atajiwekea alama mbaya katika uongozi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…