Kwa sasa Tanzania hatuna viongozi bali tuna Wanasiasa

Kwa sasa Tanzania hatuna viongozi bali tuna Wanasiasa

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Habari za saa members wote, leo kwa uchache ningependa kulizungumzia taifa kwa namna linavyo endeshwa.

Mpaka sasa ndani ya taifa letu la Tanzania taaluma nzima ya uongozi imepotea kabisa na siasa za kizandiki zimetamalaki kila pande.

Taifa hili limeshindwa kupata uongozi/viongozi kwa muda sasa toka awamu zilizo pita mpaka hii ya sasa, siasa na kundi kubwa la wanasiasa limetawala kwa kiasi kikubwa hapa nchini.

Ni ngumu kwa wanasiasa kuongoza nchi katika muelekeo ulio bora, kwao chaguzi na marumbano ya majukwaani ndivyo vitu wanaweza na sio swala uongozi wa nchi.

Hii hali ya mataifa kutawaliwa na wanasiasa kwa asilimia kubwa pia yana wakumba mataifa mengi sana hapa Africa na kwa kasi sasa Ulaya na marekani pia.

Mfano wa nchi pekee kwa ninayo ifahamu kwa haraka iliyo na uongozi/viongozi na sio wanasiasa ni China.

Mfumo wa China wa upatikanaji wa Uongozi/uongozi ndicho kitu pekee kinacho wabeba mpaka wao kushindwa kuzama kwenye huu mtego wa siasa na kundi kubwa la wanasiasa.

CASE STUDY:
1. Siasa
2. Wanasiasa
3. Uongozi
4. Viongozi

Napokea maoni yenu nyote
 
Wanasiasa wana ongoza nchi kupitia kelele za majukwaani za miaka mitano mitano hivyo ndivyo wanavyo patikana na ndivyo wanavyo fanya kazi.
 
Back
Top Bottom