Kwa shangwe za wafuasi wa CHADEMA jana Rais Samia njia ni nyeupe 2025

Kwa shangwe za wafuasi wa CHADEMA jana Rais Samia njia ni nyeupe 2025

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2019
Posts
222
Reaction score
202
Siku ya jana inamwingiza tena kwenye historia ya Tanzania na Dunia Mama yetu kipenzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kudhihirisha ujasiri, utu na upendo wake kwa Watanzania wote kwa kile kitendo cha kuhudhuria kama Mgeni Rasmi sherehe za Siku ya Wanawake Duniani zilizo adhimishwa Kitaifa na Baraza la Wwanawake wa CHADEMA huko Kilimanjaro tarehe 08/03/2023 pamoja na hotuba aliyotoa.

Tukio hili linaturejesha kwenye historia ya nchi ya Marekani kipindi cha Rais wa 16 Hayati Abraham Lincon. Rais huyu anakumbukwa kwenye historia ya Marekani kwa ile adhma yake na matendo yake ya kuwaunganisha Wamarekani bila kujali rangi zao, imani, jinsia na hali zao.

Rais huyu alifanikiwa kuiokoa Marekani na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kukomesha ubaguzi wa rangi, na kuwajengea watu weusi uwezekano wa kujiendeleza na kupata fursa mbalimbali.

Sote tunakiri kuwa, Rais Samia ameipokea nchi ikiwa katika hali ya sintofahamu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ni kweli vyama vya siasa vimekuwa na misuguano mingi katika vipindi vya nyuma, lakini katika kipindi cha 2015-2020 kiwango cha msuguano kilikuwa kikubwa.

Kwa mara ya kwanza idadi kubwa ya wanasiasa wa vyama vya upinzani walikua wamekimbia nchi kwa sababu mbalimbali. Kesi za kisiasa zilikuwa nyngi mahakamni, wafanyabiashara kufunga biashara zao na kukimbia pamoja na mambo mengine mengi ambayo yaliwarudisha nyuma Watanzania.

Kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Raisi Samia, vyama vyote vya upinzani vinampokea kwa shangwe, vilio na nderemo kama mkombozi wao. Ndani ya CCM, CHADEMA, ACT-Wazalendo na vyama vingine viongozi wa juu na wanachama wao wanakiri hadharani kuwa Uongozi wa Rais Samia umetukuka.

Nikisikiliza baadhi ya viongozi walioongea kwenye mkutano wa jana, ni wazi kuwa mkakati wa vyama vya upinzani Tanzania hasa CHADEMA ni kumpa nafasi tena Rais Samia 2025 na wao kupambania viti vya Ubunge na Madiwani ili mchakato wa Katiba utakapoanza 2026 uwe na ushirikishwaji mzuri wa Bunge ambalo litakuwa na idadi nzuri ya Wabunge kutoka katika vyama vyote.
 
Mwananchi ni sawa na Mwanaume aliyeoa wake wengi.

Mke mkubwa ni CCM, mke mdogo pendwa ni CHADEMA na vyama vingine ni wake na masuria nk nk.

Mume huyu huwapambanisha wake zake ipi apikiwe chakula kizuri kulingana na Kodi ya meza atoayo.

Ugomvi kati ya wake Hawa, huleta manufaa makubwa sababu wake hupambana kuhakikisha wanapika chakula kizuri kumvutia mume aje kulala ktk nyumba zao.

Hivi karibuni, mume ametaharuki baada ya Kupata habari kuwa WAKE zake wote, masuria na mahawara WAMEUNGANA na Wana AGENDA ya SIRI Kwa Mume wao huyo.

Nini mume atafanya kuhakikisha hapati madhara?

HAPPY women's day.😃😃😃😃😃
 
Hakuna aliyelala Chadema.

FqtCSZoXwAAiYYk.jpg
 
Back
Top Bottom