Hivi karibuni, Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Line iliingiza nchini mabasi mapya yasiyopungua 50 kwa ajili ya matumizi ya barabara za nchi nzima.
Mabasi hayo ni aina ya Yutong D 14 yaliyotengenezwa nchini China yakiwa na Kilomita '0' (zero).
Sifa kubwa ya mabasi ya Yutong D14 inaanzia hapa; Yutong-D14 Model yake ZK6139D. Yutong ni kampuni ya kwanza kwa uzalishaji wa Mabasi ya Kichina yakitengenezwa na Kampuni ya 𝗭ehngzhou 𝗬utong 𝗖o. 𝗟imited.
Mabasi ya Yutong hutumia injini za mafuta ya dizeli yenye 6 silinda (Six Cylinder).
Breki za mabasi haya hutumia mfumo wa 𝗔𝗕𝗦 (kuzuia kuingia kwenye mteremko), uthabiti wa elektroniki (ESC) na mfumo wa kumfanya dereva wa basi asisinzie awapo barabarani.
Mabati ya mabasi haya yametengenezwa kwa 𝗔erodinamiki ili kupunguza matumizi ya mafuta.
Chasis yake ni nyepesi lakini ni imara kwa safari ndefu.
Yana nafasi ya chini ya gari kwa ajili ya kuhifadhia mizigo (buti).
Yutong D14 kwa sasa ndiyo mabasi bora sana katika nchi za Afrika, Asia na Marekani ya Kusini kwa sababu ya uimara wake na abiria wake kuwa comfortable kwenye siti wawapo safarini.
SIFA NYINGINE ZA MABASI YA YUTONG D14.
1. Mabodi yametengenezwa kwa kujaa na kufanya umbo pana na siyo boksi au nusu mkate kama yale mabasi tuliyoyazoea!
2. Siti za ndani zinaachana kwa futi 3. Kwa hiyo kila urefu wa futi hizo zimewekwa siti mbili kwa mfuatano. Hii inasaidia abiria kunyoosha miguu kwa uhuru mkubwa akiwa safarini.
Hivyo kuondoa malalamiko ya miguu kuvimba au kupata ganzi kwa sababu ya damu kushindwa kutembea sawasawa kwa miguu kujikunja kwa muda mrefu.
3. Kila basi lina milango miwili ya abiria kushukia au kupandia. Mlango mmoja upo mbele jirani na dereva. Mlango wa pili upo sehemu ya katikati kabla yanapoanza matairi ya nyuma.
Hii ni kwa sababu basi linaweza kusimama mahali ambapo ni vigumu abiria kupanda au kushuka kwa urahisi.
4. Siti zote ndani zimetengenezwa kwa kuzungushiwa ngozi nene yenye muundo wa mwonekano mzuri.
5. Kila siti kwa nyuma ina meza ndogo ya kukunja na kukunjua. Abiria anaweza kuitumia meza hii kuweka chupa ya soda au ya maji na vyakula vya 'takeaway' na kuanza kula wakati basi linatembea.
6. Chini ya meza kuna mfuko kwa ajili ya kuhifadhia vitu kama; machungwa, ndizi, pakiti za clips n.k.
7. Kila siti, sehemu ya kuegemeza kichwa abiria imeandikwa 'Shabiby Bus'. Ni maandishi ya kutoka kiwandani.
8. Kila siti, kwa nyuma au mgongoni kwa abiria kuna skrini ya tivii ambayo abiria anaiseti mwenyewe na kuanza kuangalia.
9. Mbali na kuwepo kwa skrini kwa kila siti lakini pia ndani ya basi kuna runinga za futi 24 kwa kila baada ya siti nne.
10. Kila siti jna sehemu ya abiria kuegemeza mkono iliyotengenezwa kwa umbo la bapa yenye sponji ndani ya kitambaa. Hivyo si rahisi mkono kupata maumivu au usumbufu unaotokana na kuegemea kwa muda mrefu.
11. Vyoo ni vya kisasa. Vyenye shimo la sinki jeupe kwa ajili ya 'hitaji dogo'.
12. Ndani ya vyoo kuna masinki yenye mabomba kwa ajili ya kunawa baada ya abiria kumaliza 'hitaji dogo'. Pia kuna mabomba ya 'shower' yenye presha kali.
13. Sifa za choo hazijaisha. Kuna 'dustbin' nyeupe inayojifunga yenyewe baada ya kutumbukizwa kitu kama karatasi, ' toilet tissue' n.k.
14. 'Carrier' za ndani zimetengenezwa kwa kuzingatia ulinzi wa mizigo ya abiria kwani zina mifuniko. Hivyo, baada ya mizigo (kama mabegi) kuweka mifuniko inafungwa.
15. 'Roof' (au paa) za ndani zimenakshiwa kwa urembo wa kuvutia machoni huku sehemu za kutolea 'unyunyu' (air condition) zikiwa na matundu ya kutosha kumfanya abiria asikie hali ya ubaridi anaotaka kwa sababu kuna sehemu za 'kuseti' baridi ifikaje kwa abiria.
16. Unapokuwa safarini inaweza kutumia intaneti ya bure (Wireless Fidelity au kwa kifupi, Wi-fi inayotamkwa Wai-Fai). ukiwa umezima bando lako
*Shabiby Line imeamua kutumia mabasi haya kwa safari za nchi nzima ili kuwafanya wasafiri wa Watanzania kuwa katika hali ya kupumzika wakiwa safarini.
Mpaka sasa mabasi ya Shabiby Line yanakamata ruti za Dar-Dodoma, Dodoma-Tanga, Dar-Moshi, Dodoma-Mbeya, Dar-Sumbawanga, Dodoma-Arusha.