Kwa sifa hizi; Mabasi ya Shabiby Line Toleo Jipya ndiyo bora zaidi.

Huwa nikitaka kwenda Kaskazini navizia Tahmeed bus, nikichelewa kubook basi ndo napanda gari nyingine kama hizo Shabiby nk. Nishazoea utamu wa Scania.
 
Wamenikosha hiyo Tv ya futi 24! Ni zaidi ya uwanja wa Mkapa.
 
Mbona hakuna socket za kuchaji simu na laptop yangu?
 
"pia ndani ya basi kuna runinga za futi 24 kwa kila baada ya siti nne:! Upana na urefu wa ndani ya basi ni futi ngapi? Shule ni muhimu.
 
Siti za ndani zinaachana kwa futi 3. Kwa hiyo kila urefu wa futi hizo zimewekwa siti mbili kwa mfuatano. Hii inasaidia abiria kunyoosha miguu kwa uhuru mkubwa akiwa safarini.
Naomba ufafanuzi
 
Naomba ufafanuzi
Hajui vipimo huyo, yeye inchi anaita futi, hata hivyo baadhi ya basi Scania Marcopolo za zamani siti zilikuwa zinatanuliwa kama abiria ni mnene. Fikiria anasema sikirini ya tv ina futi 24! Wakati hakuna gari duniani yenye upana zaidi ya futi 10.
Shida ya machawa ni watu wasio na elimu.
 
Nimejikuta nacheka bila maandalizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…