Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
KWA SISI WATIBELI; JOGOO LA SHAMBA LINAWIKA MJINI VIZURI TUU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Haya sio majivuno. Wala sio matambo. Bali ni ukweli kuhusu sisi Watibeli.
Haijalishi Mtibeli kazaliwa kazuramimba, kazaliwa chini ya mti. Kazaliwa kijumba cha udongo. Kazaliwa ndani ndani huko majoring. Mtibeli Daima ni mtu wa mbele. Mtibeli hiyo haitamzuia kuwika mjini.
Vijana na mabinti, kuzaliwa maisha ya chini, ya dhiki, maisha ya ukiwa sio sababu ya wewe kuishi kinyonge. Sio sababu ya wewe kushindwa kuwika mjini. Kutamba na kuonyesha uwezo wako.
Hiyo misemo waachie watu wajinga. Watu wengine. Hiyo misemo sio yetu. Sisi ni Watibeli. Tuna kanuni zetu. Tuna falsafa zetu.
Wewe zaliwa hata Ikulu.
Zaliwa hata New York au Beijing. Zaliwa hata Kariakoo pale. Lakini utakapokutana na Mtibeli hata kama huyo mtibeli katokeo Turiani Morogoro, au Katokea ushirombo. Hutomuweza. Hutotamba mbele yake. Kwa sababu sisi ni Watibeli.
Wewe soma international school, nenda shule hata ya Elon Musk, lakini utakapokutana na Mtibeli hata kama amesoma kayumba shule isiyo na madarasa. Mkafanya mtihani uleule. Hutochomoka. Kwa sababu sisi ni Watibeli.
Hata uwe na pesa au mwonekano mzuri kama muongoza malaika. Mtibeli awe na sura baya kama kifaru cha Kavita. Hutomshinda mtibeli ushawishi. Na kama ni Demu atamchukua na wewe utaachwa hapo na pesa na uzuri wako.
Ninachotaka kusema nini kwenu vijana.
Maisha yako yapo kwako. Yapo akilini mwako. Yapo moyoni mwako. Ukiweza kujimudu na kujidhibiti maisha yatakuwa chini yako.
Kanuni kuu tunazotumia Watibeli kuwika Mjini hata kama tunatokea ushimbwinde. Kuwika mjini si lazima uwe maarufu kwa kila mtu. Ni uwezo wa kujijenga, kutengeneza thamani, kuelewa watu na mazingira, kutumia fursa na kuacha alama inayotambulika.
Hizi hapa ni kanuni saba zinazoweza kuwa msingi wa falsafa ya Watibeli;
Lakini falsafa ya kitibeli zinakataa kufanya asili kuwa hatima yako. Kijiji ni mahali ulipoanzia, si mwisho wa uwezo wako. Mti mkubwa hauwezi kulaumiwa kwa sababu ulianza kama mbegu ndogo ardhini. Kinachopaswa kutazamwa ni namna ulivyokua.
Hiyo ni falsafa ya kitibeli. Kama msaikolojia; Hii inahusiana na utambulisho binafsi (self-concept). Namna unavyojiona huathiri namna unavyojiendesha.
Ukiamini kwamba wewe ni mtu wa kawaida kwa sababu umetoka familia maskini, unaweza kujizuia hata kabla hujajaribu. Lakini ukijiona kama mtu anayeweza kujifunza, kukua na kutengeneza fursa, utaanza kutenda kwa namna inayolingana na mtazamo huo.
Hata hivyo, kujiamini pekee hakutoshi; lazima kuambatane na uwezo, nidhamu na matokeo.
Lakini kutambulika bila kuwa na thamani ni umaarufu usio na mizizi.
Mtibeli anatakiwa kujiuliza: Ni tatizo gani ninaweza kutatua ambalo watu wako tayari kulipia? Nina ujuzi gani ambao wengine wanaweza kuutegemea?
Ukiwa mfanyabiashara, toa huduma bora. Ukiwa msomi, toa maarifa. Ukiwa kiongozi, leta suluhisho. Ukiwa msanii, tengeneza kazi yenye alama yako. Hapo nimezungumza kifalsafa.
Katika upande wa Saikolojia iko hivi;Katika mahusiano mengi ya kijamii na kibiashara, watu hutathmini manufaa ya kushirikiana na mtu.
Mtu anapogundua kuwa unarahisisha maisha yake, una ujuzi, unatimiza ahadi au unatatua matatizo, anakuwa na sababu ya kukutafuta tena na kukutambulisha kwa wengine.
Kitaalamu tunaita social exchange theory
Mtu anaweza kuishi Dar es Salaam miaka ishirini bila kuelewa namna biashara zinavyopata wateja. Mwingine anaweza kufika leo, akachunguza soko kwa makini, akaona tatizo ambalo watu wengine wamelizoea na akalitengenezea suluhisho.
Tofauti si muda waliokaa mjini pekee; ni uwezo wa kusoma mazingira. Watibeli tunafundisha watoto wetu uwezo wa kuona na kuyasoma mazingira.
Mtibeli anatengeneza mahusiano kwa kutoa mchango. Anajenga sifa ya kutimiza ahadi, kutunza siri, kutatua matatizo na kushirikiana na watu bila kujishusha wala kujikweza.
Lengo si kumjua kila mtu. Lengo ni kuwa na mahusiano yenye kuaminiana na yenye manufaa ya pande zote.
Wakati wanalalamika shule haina waalimu na kujipa kisingizio cha kufeli, sisi ndio tunatumia hiyo kama fursa ta kuonyesha uwezo wetu.
Baraka kwetu ndio mtihani. Kwa sababu Watibeli tunaogopa Baraka kuliko changamoto. Unapopewa Baraka fulani labda Kazi, unapaswa ujue ule ni mtihani ambao unatakiwa uufanye na kipimo cha kuonyesha uaminifu wako.
Mtu asiyeweza kusimamia hisia zake anaweza kufanya maamuzi ya kujithibitisha kwa wengine: kununua vitu asivyovimudu, kuingia kwenye migogoro isiyo na faida, kukopa kwa sababu ya mashindano au kuanzisha miradi kwa presha ya marafiki.
Mtibeli anatambua kwamba si lazima ajibu kila kauli, athibitishe kila uwezo au akubali kila mwaliko.
Mtu wa kwanza anaweza kufanya kila kitu mwenyewe. Akiumwa, biashara inasimama. Akikosa fedha, kila kitu kinakwama. Akiondoka, hakuna kinachoendelea.
Mtu wa pili hujenga taratibu, watu, taratibu za kazi, chapa, mahusiano ya wateja na mifumo ya kifedha.
Kijana, Mtibeli anapaswa kuelewa kwamba kutamba mjini si kuvaa vizuri pekee, kuzungumza Kiingereza, kufahamiana na watu maarufu au kuonekana una fedha.
Ni kujenga uwezo ambao hauwezi kufutwa kirahisi na mazingira yako ya zamani; ni kujifunza mifumo ambayo wengine hawaioni, kutengeneza thamani ambayo wengine wanaihitaji, na kujenga nidhamu inayokuwezesha kuendelea hata pale mambo yanapokuwa magumu.
Mtibeli anaweza kutoka Ushimbwinde, lakini hafungwi na Ushimbwinde. Anaweza kuanzia kwenye hali ndogo, lakini hafanyi udogo wa mwanzo kuwa utambulisho wa maisha yake yote.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam

Jamii ina tabia ya kuwahukumu watu kwa asili zao. Mtu akitoka kijijini, anaweza kuonekana hana uwezo, hana exposure au hawezi kuhimili ushindani wa mjini.1. Usijitambulishe kwa Ulipotoka, Jitambulishe kwa Unachoweza Kufanya.
Lakini falsafa ya kitibeli zinakataa kufanya asili kuwa hatima yako. Kijiji ni mahali ulipoanzia, si mwisho wa uwezo wako. Mti mkubwa hauwezi kulaumiwa kwa sababu ulianza kama mbegu ndogo ardhini. Kinachopaswa kutazamwa ni namna ulivyokua.
Hiyo ni falsafa ya kitibeli. Kama msaikolojia; Hii inahusiana na utambulisho binafsi (self-concept). Namna unavyojiona huathiri namna unavyojiendesha.
Ukiamini kwamba wewe ni mtu wa kawaida kwa sababu umetoka familia maskini, unaweza kujizuia hata kabla hujajaribu. Lakini ukijiona kama mtu anayeweza kujifunza, kukua na kutengeneza fursa, utaanza kutenda kwa namna inayolingana na mtazamo huo.
Hata hivyo, kujiamini pekee hakutoshi; lazima kuambatane na uwezo, nidhamu na matokeo.
Niliwahi kukuandikia, lazima ujenge jina lako. Brand yako. Lakini lazima uzingatie thamani ya kweli. Mjini kuna watu wengi wanaotafuta kuonekana. Wanataka kujulikana, kuzungumziwa, kupigiwa simu na kuhusishwa na watu wenye majina makubwa.2. Jenga Thamani Kabla Hujatafuta Umaarufu.
Lakini kutambulika bila kuwa na thamani ni umaarufu usio na mizizi.
Mtibeli anatakiwa kujiuliza: Ni tatizo gani ninaweza kutatua ambalo watu wako tayari kulipia? Nina ujuzi gani ambao wengine wanaweza kuutegemea?
Ukiwa mfanyabiashara, toa huduma bora. Ukiwa msomi, toa maarifa. Ukiwa kiongozi, leta suluhisho. Ukiwa msanii, tengeneza kazi yenye alama yako. Hapo nimezungumza kifalsafa.
Katika upande wa Saikolojia iko hivi;Katika mahusiano mengi ya kijamii na kibiashara, watu hutathmini manufaa ya kushirikiana na mtu.
Mtu anapogundua kuwa unarahisisha maisha yake, una ujuzi, unatimiza ahadi au unatatua matatizo, anakuwa na sababu ya kukutafuta tena na kukutambulisha kwa wengine.
Kitaalamu tunaita social exchange theory
Mji si mkusanyiko wa majengo na watu tu. Ni mfumo wa mahitaji, fedha, taarifa, mahusiano, mamlaka, ushindani na fursa.3. Jifunze Mfumo wa Mji Kabla Hujajaribu Kuuingia na kuutawala.
Mtu anaweza kuishi Dar es Salaam miaka ishirini bila kuelewa namna biashara zinavyopata wateja. Mwingine anaweza kufika leo, akachunguza soko kwa makini, akaona tatizo ambalo watu wengine wamelizoea na akalitengenezea suluhisho.
Tofauti si muda waliokaa mjini pekee; ni uwezo wa kusoma mazingira. Watibeli tunafundisha watoto wetu uwezo wa kuona na kuyasoma mazingira.
Moja ya sifa za kipekee ambazo sisi watibeli tunazo ni hii. Wakati wengine wakilalamika kuhusu kukosa connection, kijana wa kitibeli anahangaika yeye kuwa hiyo connection. Ni mchezo fulani hivi kama wa filamu lakini wenye uhalisia.4. Mtibeli Hategemei Connection Pekee; Anakuwa Connection.
Mtibeli anatengeneza mahusiano kwa kutoa mchango. Anajenga sifa ya kutimiza ahadi, kutunza siri, kutatua matatizo na kushirikiana na watu bila kujishusha wala kujikweza.
Lengo si kumjua kila mtu. Lengo ni kuwa na mahusiano yenye kuaminiana na yenye manufaa ya pande zote.
Sisi Watibeli tunapenda changamoto kwa sababu tunapenda kujifunza. Hatukimbii changamoto. Tunazitumia kujifunza na kama ngazi ya kupanda juu. Wakati wengine wakilalamika hakina ajira, hiyo kwetu ni changamoto ya kujifunza namna ya kutatua tatizo la ajira.5. Changamoto ni fursa ya kujifunza. Baraka ni mtihani wa kujipima
Wakati wanalalamika shule haina waalimu na kujipa kisingizio cha kufeli, sisi ndio tunatumia hiyo kama fursa ta kuonyesha uwezo wetu.
Baraka kwetu ndio mtihani. Kwa sababu Watibeli tunaogopa Baraka kuliko changamoto. Unapopewa Baraka fulani labda Kazi, unapaswa ujue ule ni mtihani ambao unatakiwa uufanye na kipimo cha kuonyesha uaminifu wako.
Mjini kuna ushindani, kejeli, watu wenye majivuno, vishawishi vya matumizi na fursa zinazoweza kuonekana za haraka.6. Simamia Hisia Zako; Usiruhusu Mazingira Yakuendeshe.
Mtu asiyeweza kusimamia hisia zake anaweza kufanya maamuzi ya kujithibitisha kwa wengine: kununua vitu asivyovimudu, kuingia kwenye migogoro isiyo na faida, kukopa kwa sababu ya mashindano au kuanzisha miradi kwa presha ya marafiki.
Mtibeli anatambua kwamba si lazima ajibu kila kauli, athibitishe kila uwezo au akubali kila mwaliko.
Kuna tofauti kati ya mtu anayefanya kazi ili apate pesa leo na mtu anayejenga mfumo unaoweza kuzalisha thamani kwa miaka mingi.7. Jenga Mfumo Unaokuzidi Wewe Mwenyewe.