Kwa suala la ununuzi wa rada nne nitakupongeza daima hayati JPM kazi ya kizalendo sana

Rada haijui hiyo habari ya Osama au beberu. Tambua kuwa nchi yetu inatazamwa yote na mamlaka ya anga TCAA.

JPM alinunua rada nne zenye kumilika kila kona ya TZ, hakuna hata mdudu anayeweza kuruka angani akaingia nchini asionekane.
 
Nenda kazikwe naye
 
Nikweli.. lakini je.. mamlaka zikiona ndege inaingia zitakwambia ?
Ndege ikiingia inaonekana moja kwa moja katika mitambo ya TCAA inayoziongoza hizo rada. Tofauti sana na miaka ya nyuma.

Kuna kaka mmoja alikuwa anataka sana kurudi tena shirika la reli ili aibe mwisho mwisho kabla hajastaafu. Akaja kujua kuwa sasa hivi kuna mfumo wa GPS kila treni inaposimama taarifa zinaifikia ofisi kuu ya TRC, akaja kujua kuwa hawezi tena kufanya maghumashii ya siku za nyuma, unyonge umemuingia na hataki tena kurudi kazini.
 
Rada haijui hiyo habari ya Osama au beberu. Tambua kuwa nchi yetu inatazamwa yote na mamlaka ya anga TCAA.

JPM alinunua rada nne zenye kumilika kila kona ya TZ, hakuna hata mdudu anayeweza kuruka angani akaingia nchini asionekane.

JPM alishakufa hayupo tena. Kuna aliowakwaza sana ndugu. Wengine leo ni wajane na yatima. Ukisikia mapendekezo kwenda kuzikwa naye uwe unaelewa.
 
Tangu lini Awamu za waswahili zikawa na tatizo na waarabu?

Wakipewa zawadi wajomba tatizo liko wapi!!!

Nongwa tu yawasumbua.
 
Mada ya mawazo hasi ni mada mpya,uliyoiibua ww,
Hakuna uwezekano wa ndege kuingia na kuondoka tu, hii ni Tanzania mpya sio ile ya miaka ya nyuma kila Alhamisi ndege zinaingia mgodini na kuchukua vipande vya dhahabu na kuondoka.
 
JPM alishakufa hayupo tena. Kuna aliowakwaza sana ndugu. Wengine leo ni wajane na yatima. Ukisikia mapendekezo kwenda kuzikwa naye uwe unaelewa.
Samia atawakwaza wengi na wataumia wengi na atakapoondoka ikulu madhambi mengi tutayajua, hivyo hao wa kuzikwa nae watakuwepo tu.

Ndio maana ya majukumu ya urais, huwezi kuwakera wote na kuwafurahisha wote. Wapo wenye akili watakaokukumbuka.
 
Hakuna kinachoingia ndani ya anga la TZ kisionwe na rada hizo, hakipo kwa sasa na siku zijazo
Bila shaka siyo kuonywa tu bali pia kuongea na rubani wa chombo hiko. Akileta fyoko fyoko jeshi letu la wananchi linamshughulikia huko huko angani. Hivyo nchi iko salaama maeneo yote ie ardhini, majini na angani. JPM kweli alikuwa anapaisha Tanzania.

Zipo nne zilinunuliwa shilingi bilioni 67 zote kwa pamoja.
Yaani shillingi billioni 67 ni chini ya bei ya aliyokodi January kwa mwaka ile software ya tekohama ya Mahindra kwenye grid yetu ya umeme ambayo wala haifanyi kazi.
 
Hakuna uwezekano wa ndege kuingia na kuondoka tu, hii ni Tanzania mpya sio ile ya miaka ya nyuma kila Alhamisi ndege zinaingia mgodini na kuchukua vipande vya dhahabu na kuondoka.
Kuna kutumia elimu nakutumia akili, akili inakufanya kuwa na ujasiri wa kuhoji kila unachokiona ,na elimu ni formula fulani hv, wsemavyo "elimu isipotosha ongezea akili"
 
Amefanya baadhi mazuri ila mengi kaboronga sana!! Penye ukweli pasemwe tu bila kubwabwaja!!

Nahisi angekuwa na viongozi washauri wazuri angefanya vizuri sana!! Ila viongozi aina ya makonda na sabaya ndo walikuwa washauri wakuu lazima aboronge tu!!
Huko kuboronga ni mtaji wa poor minds. Aliofanya ni makubwa kuliko huko kuboronga mnakomkandia hebu oneni aibu dili, wizi, ujanja janja, vyeti feki na ukwepaji kodi sio sifa kwa taifa.
 
Amefanya baadhi mazuri ila mengi kaboronga sana!! Penye ukweli pasemwe tu bila kubwabwaja!!

Nahisi angekuwa na viongozi washauri wazuri angefanya vizuri sana!! Ila viongozi aina ya makonda na sabaya ndo walikuwa washauri wakuu lazima aboronge tu!!
Yana ukweli kwa % kubwa
Ila nae alikuwa na ubabe wa kij... hakutaka ushauri bali kila kitu alitaka aamue yeye hapo ndipo alipoboronga

Hao kina sabaya hawakuwa washauri bali watekaji tu na walikuwa wanamfurahisha kwa kumpelekea Habari za uongo
 
Malengo ya hizo ni mazuri ila haimaanishi hatutoibiwa! Kwa maana wanaoiba ni viongozi wakuu ambao wana mamlaka ya moja kwa moja yakutoa oda kuwa ao wanaokuja wasikaguliwe.

2013 Twiga wanapandishwa kwenye ndege na kuondoka haikufanyika hivo sababu hatuna Rada za kumulika nchi nzima, maana Rada ilikuwepo kwa upande wa KIA ikipiga kazi maeneo yote ya ARUSHA, MWANZA, KIRIMANJARO mpaka Tanga, tuseme tu wenye mamlaka walilidhia sisi tuibiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…