unaelewa maana ya trade? trade ina pande mbili, data ulizoweka zinaonyesha imports, sasa sisi tunauza nini kwenda kwenye hizo nchi kama exports? nchi huwa zinahangaika kutafuta pa kuuzia bidhaa zao ( exports) na siyo kuwa soko la bidhaa za wengine, kuwa soko ndiyo kitu rahisi kuliko vyote ila wewe kuweza pia kuuza kwao bidhaa ndiyo kitu cha kujisifu, ndiyo maana huona nchi makini kiongozi akifanya ziara anakwenda na wafanyabiashara lengo huwa ni kuangalia jinsi ya kupata soko la bidhaa zao kwenye hiyo nchi, watu makini hawafanyi ziara na bongo movie unless kama unataka kuuza bongo movie kama exports kwenye hizo nchi.
isitoshe ngoja nikusaidie kidogo, ni hivi kila bidhaa unayonunua kariakoo gsm unazalisha ajira kule ilikotengenezwa, umeshawahi kujiuliza au hata tu kulielewa hilo ?