Kwa Takwimu hizi, nalazimika kuamini Zanzibar hawana tatizo la Ajira

Kwa Takwimu hizi, nalazimika kuamini Zanzibar hawana tatizo la Ajira

KingGuaje

Senior Member
Joined
Dec 30, 2019
Posts
141
Reaction score
249
Poleni na majukumu wakuu na hope mko na afya njema, wanaosumbulia na maradhi namuomba mwenyezi MUNGU awaponye na warudi kwenye hali zao za kawaida.

Basi bhana! Wazo la kuandika uzi huu limekuja baada ya kuingia huko ajira portal nikiwa ninadhumuni la kuangalia matokeo ya written interview ya TRA iliyofanyika hivi karibuni.

Kama tunavofahamu tatizo la ajira linaloikumba nchi sikuona mchangao wa idadi kubwa ya watu ambao wamekua wameitwa na pia kuwa non-selected basi nikapata wazo la kuchungulia ndugu zetu wa ng’ambo kuona nao hali ikoje kule.

Ikilichonishangaza sana ni idadi ndogo sana ya watu waloitwa kwenye written interview ukizingatia hichi ni kipindi ambacho kuna graduates wengi mataani.

Pili, wanaoitwa hawafaulu mitihani yao, imenisikitisha kuona kati ya watu wa tano walioitwa wote wanashindwa kuvuka kwenda hatua inayofuata.

Hizi sababu mbili zinanifanya Niamin visiwani kwa 95% hakuta tatizo la ajira.

Hivyo tunaposema tatizo la ajira tuitaje Tanganyika na sio Tanzania.

Zanz 1.jpg

Zanzi 2.jpg

Zanzi 3.jpg
 
Sio wenzetu hao, wazanzibari ni raia wa daraja la kwanza sisi watanganyika ni raia daraja la pili.

Vuta picha tu, wao wapo milioni 1.5 ila wana mgao wa ajira za muungano asilimia 21 kuanzia jwtz, polisi, tra, bandari, tanesco, n.k na hapo bado huwa hawazijazi.

Mtanganyika ukienda huko kwao hupati ajira kwenye serikali yao ya Zanzibar.

Chao ni chai ila vyetu ni vyao.
 
Wake zetu hao acha tuendelee kuwahonga ili tupate penzi..hujui Tanganyika tunanufaika na mengi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Acha chuki sasa zanzibar kuna wasomi wenyewe wapo bize na mashindano ya Quran hizo nafasi wala hawana mda nazo.
 
Back
Top Bottom