Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

Agizo na maelekezo yanayoruhusu kuoa wake mpaka wanne yalipaswa kureflect kwenye idadi ya wanaume na wanawake waliopo duniani
Ningependa kujadiliana nawe zaidi kuhusu dini zetu ila wakati mwingine tafadhali njoo na hoja zenye mantiki na jitahidi uwe ‘objective’ ninakuona unazo akili za kujadili ila kuna mambo machache yanakuangusha.
Hapa unaacha hoja na kuingiza vihoja ili kukimbia kuijibu hoja
Na kwa kuongezea ni wapi kwenye biblia imeamrishwa watu waoe mke mmoja tu? Execute

Nipe nukuu.
Soma Mathayo 19:4-6, biblia inaongelea mke na sio wake:

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
 
Agizo na maelekezo yanayoruhusu kuoa wake mpaka wanne yalipaswa kureflect kwenye idadi ya wanaume na wanawake waliopo duniani
Umeelewa nilichoandika mkuu? Hebu soma tena

Ukisoma Quran vizuri Allah hajalazimisha mtu kuoa wake wanne, na kwakuwa hajalazimishwa mtu hivyo usitarajie kuona kila mtu anaoa wanne.”

Na kwa watakaofanya hivyo wanapewa sharti la kuwa na uwezo wa kufanya uadilifu baina ya wakeze.
Dah, hapo ni wapi tumeambiwa tuoe mke mmoja? Na tusioe wake wengi mkuu?
 
Umeweka nukuu nyingi za mambo ya wayahudi halafu kwa makusudi umeiacha Mathayo 19 ambayo imeelezea nini hasa kilipelekea watu katika agano la kale walipewa ruhusa na Musa kuoa zaidi ya mke mmoja. Sasa soma hapa chini:

Mathayo 19:3-12

3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa sababu yoyote?

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.

12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee
 
Unapata faida gani kuleta takwimu za uongo wewe mvaa rozari ....
Hizo data zako za kuokota Makanyagio Ni fake .
Wewe umekuja kubishana hapa maana hata takwimu ulizonazo hujaziweka hapa.
 
Kumbe quran iliandikwa kwa ajili ya enzi hizo tu? Sasa kwanini watu wanaitumia miaka hii?
 
Ni mbumbumbu tu ndio atakubaliana na mleta mada kuwa wanaume ni wengi kuliko wanawake..nenda hospital au kituo chochote Cha afya kaombe ratio wa watoto wanaozaliwa Kati ya wakike na wakiume then urudi...
Hizo takwimu hapo juu ni rasmi hivyo kama unazipinga tuletee unazoziamini pamoja na chanzo chake.
 
MashaAllah.
 
Wajinga Jf ni wengi mno....
 
Yaani hata tungekuwa sawa bado wanaume ni wachache hapo kuna vichaa hapo na mapadre sijui kuna wengine wapo jela kuna kina juma lokole hapo yaani tabu tupu yaani wanaume waliopo timamu kiakili kiuchumi na waliopo uraiani ni wachache sana .
Kwahiyo hawa ndio wangepunguza nusu ya wanaume ili angalau wanaume wanaobaki wapate angalau watatu?

Halafu hii hoja yako ni dhaifu kwasababu ukichaa haichagui jinsia, jela vivyo hivyo na kuna masista wengi kama walivyo mapadri.
 
Hata huko uarabuni wengi wangekimbia uislamu, Ila ulikimbia uislamu unafungwa au kuuliwa
Una takwimu mkuu?

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na ‘Pew Research Center’ mwaka 2017 iliitaja Uislamu kuwa ni Dini inayokua kwa kasi zaidi.

Mwaka ule waislamu walikadiriwa kuwa Bilioni 1.8 duniani ila inatazamiwa idadi hiyo kuongezeka na kufikia Bilioni 3 ifikapo 2060 ambapo ni ongezeko la zaidi ya 70% Huku wakristo wanatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 34% tu.

Na wakati huo watu watatu kati ya kumi watakuwa ni Waislam duniani.
 
Haya yanahusiana vipi na mada hii?
 
Hilo suala la kuoa wake wengi wanawake wengi hawalikubali, ila wanaume wa kiislamu wanalipenda kuliko hata kuswali..
unakuta mtu hafanyi ibada lakini kwenye kuoa Sasa wa kwanza.utasikia kuoa ni sunna waislam tumeruhusiwa😂😂😂
Bahati mbaya Allah amesahau kuumba angalau wanawake wengi kuliko wanaume ili waweze kuoa zaidi ya mmoja.
 
Halafu hii hoja yako ni dhaifu kwasababu ukichaa haichagui jinsia, jela vivyo hivyo na kuna masista wengi kama walivyo mapadri.
Hivi unakijua unachokisema au unabahatisha?

Kwa Marekani pekee ‘Federal Bureau of Prison’ walitoa ripoti iliyoonesha kuwa 93% ya wafungwa wao ni wanaume na wanawake ni 7% pekee.

Kwa duniani inakadiriwa kuwa (hii ni takwimu ya muda mrefu kidogo lakini itatusaidia walau kupata picha, ni ya 2010) kati ya Wafungwa 16 basi 15 ni wanaume na mwanamke ni mmoja tu, hiyo ni DUNIANI.

Nakuuliza tena unajua unachokisema au unabahatisha? Championship
 
Islam walioingia ukristo ni wengi sema kuna shida ya kuwa huru kusema sababu ya imani ya islam ni hatarishi sana.

Ni sawa na issue ya Ndoa, kinamama wengi wa Islam hawapendi ndoa ya wake wengi ila kwa sababu ya sheria ya dini basi wanaingia tu!.
Uislamu kuingia ni free na kutoka unaacha kichwa 😂. Halafu ukweli kwamba hamna mwanamke anayefurahia kuolewa pamoja na mwingine kwa mwanaume mmoja inathibitisha lile agizo ni feki.

Allah angekuwa ndio muumbaji wa ulimwengu angeweka kukubalika kwa hicho kitu ndani ya mioyo ya wanawake.
 
Mimi siyo muislamu lakini hizo takwimu zisikushitue. Chukua rafiki zako 2 muwe 3 halafu mtangaze mnatafuta wachumba. Siku 2 nyingi watajiyokeza wanawake 20+.
Takwimu ziko wazi kabisa hapo juu. Kuweka tangazo moja hakuleti uhalisia wa kitakwimu.
 
Zipo sawa wakati kuna surplus ya 1.8M au huoni?
Kwahiyo hiyo surplus ndio inatakiwa angalau wanaume laki tano wa kiislamu wajipatie wake wanne halafu wengine wabakie hivyo? Kumbe quran iliandika agizo kwa ajili ya wachache? Na hii ni kwa Tanzania peke yake.

Mbona umeziepuka takwimu za dunia nzima zinazoonesha wanaume ni wengi zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…