Kwa Tanzania/Dunia ya leo Katiba kuruhusu Darasa la Saba kuwa Mbunge ni aibu kwa Taifa

Kwa Tanzania/Dunia ya leo Katiba kuruhusu Darasa la Saba kuwa Mbunge ni aibu kwa Taifa

Kama Msukuma Kuna mda anakuwa na logic kuliko Kabudi, Lipumba na huyu utopolo Dr Abbas Kwa nini tusichague darasa la saba?????

Mleta mada!! Kwa taarifa yako Darasa la saba wengi ndo werevu kuliko hao wenye madegree! Hili ndo ajabu kuu la Tanzania!

Hivi wewe kati ya Mfanyabiashara wa madini Laizer na Mwakyembe wakiongea, Nani unamuelewa kwa haraka na vizuri????
Itategemeana na uwezo wako wa kuelewa
 
Kama Msukuma Kuna muda anakuwa na logic kuliko Kabudi, Lipumba na huyu utopolo Dr Abbas Kwa nini tusichague darasa la saba?

Mleta mada!! Kwa taarifa yako Darasa la saba wengi ndo werevu kuliko hao wenye madegree! Hili ndo ajabu kuu la Tanzania!

Hivi wewe kati ya Mfanyabiashara wa madini Laizer na Mwakyembe wakiongea, Nani unamuelewa kwa haraka na vizuri?
Tz ni nchi ya ajabu sana. Mtu kama Msukuma & Lusinde wanasifa ya kuwa wabunge lakini hawana sifa za kuwa wenyeviti wa kamati ya shule!!! Hivi unajua kama sifa mojawapo ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya shule ni kuhitimu kidato cha 4? Sasa kama kigezo chako sometimes Msukuma anaongea point kuliko Kalamagamba basi hata Wehu pia sometimes huwa wanakuwa poa ndiyo maana huwa wanakula na kunywa maji nao tuwape ubunge?
 
Basi ili lifanyike kisheria kwamba huyo mbunge wa darasa la saba lazima awe na wataalamu wenye ubobezi na elimu zaidi yake ili wamsaidie

Je hao wabunge wanafanya hivyo?
Bila hata kisheria,kila mbunge ana karibu yupo permanent kwenye ofisi ya mbunge
 
Sina nia ya kuwadharau wale wenye elimu ya Darasa la Saba ila ninaandika haya kwa kuzingatia nafasi ya uwakilishi wa Jimbo na unyeti wa nafasi hii. Dunia/Tanzania ya leo siyo ile ya miaka ya 60s. Tunahitaji mabadiliko makubwa katika nyanja zote ikiwemo katika nafasi za ubunge.

Mbunge ni mtu muhimu sana katika eneo analoliwakilisha na ndiyo maana anaheshimika na kulipwa mamilioni ya pesa kutoka na unyeti wa kazi anayoifanya au nafasi aliyonayo.

Mbunge anayeongoza Jimbo lenye kata 30 anakuwa na elimu ya Darasa la Saba, ila afisa mtendaji wa kata anayeongoza kata moja anatakiwa angalau awe na Diploma/shahada. Hiki Ni kichekesho sana na Tanzania inatakiwa tubadilike ili kuendana na uhalisia wa sasa. Tumebaki nyuma sana katika mambo mbalimbali likiwemo hili la kuwa na wawakilishi ambao uwezo wao na nafasi zao haviendani.
Umeshaanza kwa dharau japo unatuaminisha kua hujadharau elimu ya wengine,elimu yenyewe hii unayosema iloyojaa misingi ya kigeni isiyo msaidia mTanzania? Ktk nchi za kiafrika huoni wasio na elimu ndiyo wanaoweza kuendesha mambo kwa uzuri na kufuata misingi ya kiafrika, kila mwenye shule huko bungeni huwaoni wanaochemka na PHD zao?

Bure kabisa wewe
 
Kama Msukuma Kuna muda anakuwa na logic kuliko Kabudi, Lipumba na huyu utopolo Dr Abbas Kwa nini tusichague darasa la saba?

Mleta mada!! Kwa taarifa yako Darasa la saba wengi ndo werevu kuliko hao wenye madegree! Hili ndo ajabu kuu la Tanzania!

Hivi wewe kati ya Mfanyabiashara wa madini Laizer na Mwakyembe wakiongea, Nani unamuelewa kwa haraka na vizuri?
Usimshangae huyu..hawa ni wale walioenda vyuoni na baada ya hapo wanazurula na vyeti kwenye makampuni ya watu ambao hawakusoma
 
wengi wanashindwa kutofautisha kati ya elim na akili, elim ni bora bt akili ni bora zaidi coz elim inatokana na akili, hivo tusiwachukulie poa ambao hawakwenda shule coz wana miliki akili ambayo ndo chanzo cha elim inayotufanya tuwaone wajinga.
 
Basi aende Kenya au Uganda akaonyeshe logic yake! Naunga mkono hoja!
 
Back
Top Bottom