Kwa Tanzania; Kama Mwanamke hajawahi fika Ukanda wa Pwani ni hakika Hajui Kupika chakula kitamu

Kwa Tanzania; Kama Mwanamke hajawahi fika Ukanda wa Pwani ni hakika Hajui Kupika chakula kitamu

Kujua kupika ndio kukoje

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
  1. Kujua matumizi sahh ya viungo (kujua aina za spices, matumizi yake na jinsi ya kuvibalance).
  2. kujua kiwango sahh Cha joto linalotakiwa kuivishia chakula ili kisipoteze Radha, kujua mchanganyiko sahh wa vitu vinavyoitajika wakati wa upishi(mbali na viungo)
  3. kujua aina mbali mbali za vyakula na namna ya kuvipika na namna ya kuviandaa. Nk
Hapo sijazungumzia nje ya jiko maana upishi hauishi jikon tu.
Kama Kanda ya ziwa wengi hawajui kupika wanajua kuchemsha tu
 
Nakuunga mkono gwiji, ni majority hasa wale waliokulia maisha ya kawaida sio wale waliokua wanpikiwa na house girls
 
Kwema Wakuu!

Kuna watu watabisha Kwa ubishi wao tuu lakini kimsingi na kitaalumuna unapozungumzia mapishi Kwa nchi yetu basi hapo utakuwa unazungumzia ukanda wa Pwani.
Kama unaishi maisha ya kawaida Kurudi ufukara na hujawahi kuishi Maeneo ya Pwani na hapa nazungumzia DAR es salaam, Pwani yenyewe, Tanga, Lindi, Mtwara, na Zanzibar basi kaa ukijua hujawahi Kula chakula kitamu.

Na Kama Mwanamke hajawahi fika na kuishi Pwani basi ni hakika hajui Kupika chakula kitamu.

Wanawake WA Pwani moja ya silaha zao nzito za Masafa mafupi na marefu mbali na kukata mauno pia Upishi WA chakula kitamu wameshindikana.

Kuanzia Chai, Andazi, chapati, wali, pilau, biriani, Makande, Makange, Ndizo, maharage, kunde, mtori, n.k. vyakula hivyo Kama hujawahi kupikiwa na Mwanamke wa Pwani basi jua hujui utamu wake.

Ukiona mtu yeyote anajua Kupika chakula Kwa nchi hii ya TANZANIA, jua Ujuzi huo ameupatia baada ya kuishi aidha ni DAR es salaam, au Pwani, au Tanga.

Kupika Kwa wanawake WA Pwani ni Sanaa, ni ufahari, ni Jadi Yao. Vikorombwezo bila ya bezo, wakiimba Kwa Dezo na michezo ya Ngoma chakula chenyewe kinageuka chocolate.

Mwanamke wa Pwani hahitaji kwenda kujifunza Hotelia ATI ili awe MPISHI mzuri, mapishi matamu kwao ni silaha.

Wengine chakula kitamu ni mpaka siku ya Harusi au sikukuu hasa huko Mikoani.
Ila ukanda wa Pwani kila siku chakula kitamu bila kujali bajeti ni ndogo kiasi gani.

Taikon Leo nipo kwenye Migahawa ya Waswahili huku, kuna watu wanapika bhana, utamu mpaka unafumba macho.

Ooh! Kalogwa! Sijui limbwata! Hivi chakula kitamu unafikiri mchezo!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kwa hilo hujakosea Tycoon wa Fasihi
 
Acha maneno yako wewe, huku kwetu kanda ya ziwa tuna vyakula vyetu vya asili yetu ambavyo wanawake wetu ni mahili sana kuvipika ukilinganisha na hao wa pwani. Mwandishi amebainisha aina ya vyakula ambavyo wapwani ni mahili hapo nimekubali kabisa lakini kwa vile vya asili ya ukanda kila kanda kwa asili yake inafanya vizuri. Mfano ukipikiwa kande na mtoto wa kanda ya ziwa(hasa hasa usukumani) kiukweli "utajua hujui" kama uliwahi kula chakula hicho bila kusahau ugali, wa kwetu huku ni tofauti sana na wa huko pwani. Vile vile ukienda pande za Kagera ukapikiwa ndizi za asili yao kwa kweli ni tamu sana na mapishi yao ni ya tofauti sana ukilinganisha na mahali kwingine.

Naweza kuhitimisha kwa kusema kuwa uzuri wa mapishi ya vyakula mbalimbali hutegemea na asili ya chakula chenyewe ijapokuwa wenzetu wa pwani wanajua kutumia zaidi viungo katika mapishi yao kuliko mahali kwingine popote Tanzania hii.
Mfano wakelewe viazi vinapikwa na maganda yake

Msukuma ukimpatia dagaa huo mchuzi sasa hauna hata ushirikiano na hakunaga dagaa tamu zenye mchuzi

Kanda ziwa nzima hakuna wataalamu wa kupika wali uliochambuka kama huamini tembelea vimigahawa vya kijijini ujionee wali kama ugali

Hivyo vyakula vyote nilivyovisema vipo kanda ya ziwa enzi na enzi

Wasukuma wanachojua ni mrenda tu labda na maharage kidogo kwa vile wanayawekea karanga
 
Upo sahihi kupika nilifunzwa na Dada wa kidigo wakati tuna soma Tanga likizo naenda kwao mie kwetu bara hukoo!
 
Nakubaliana na ww kabsa pwani na watu wa mwambao huo kwel wanajua kupika na sio tu wanajua kupika wanajua pangilia viungo.
Katika mboga nisiyo ipenda ni dagaa ila wacha sku moja nmekutana na dagaa imepikwa na binti wa tanga wacha bana dagaa imewekwa nazi,royco sjui vingne viungo gan dagaa tamu nzuri
Uzuri na utamu wa chakula ni viungo na watu wa pwani ilo wanaliweza huwezilinganisha na watu wa kanda ya Ziwa ambako nmetoka uku kiungo ni Nyanya na kitunguu bas

Tz bana kla mkoa inasifa zake ilo halina ubishi watu wa mwambao wa pwani wanajua kupika iyo ndo moja ya sifa yao
Watu wa mara wanaaminika ni wakorofi ndio ata tanga wapo wakorofi ila sifa ya ukorofi iko Mara
 
Wanawake wa kanda ya ziwa ugali unasongwa na rungu
 
Aisee, huu mwaka tutasikia mambo mengi, watu wana stress ya kupanda bei bidhaa na mafuta
 
Back
Top Bottom