Ungekuwa na utulivu kichwani, kamwe usingeandika upuuzi wa namna hii.
Kwa upeo wako, hivi muuaji wa Ali Kibao, akidhalilika, na familia ya Kibao, marafiki wa Kibao, majirani, na wananchi wote wanaothamini utu na uhai wa binadamu, wanadhalilika? Vivyo hivyo kwa Mdude? Seka, na wale waliovunjwa miguu na mikono.
Kwa kweli we hupo sawa sawa kichwani. Hata mtu akikuita mjinga, atakuwa amekupendelea sana.
Hapa anadhalilika yeye na maharamia wake wanaotekeleza uovu ambao ameubariki. Kwa waliodhulumiwa, familia za waliouawa, waliotekwa na walioumizwa, wananyosha mikono juu, kumshukuru MUNGU. Maana anagalao uovu wake sasa unajulikana Dunia nzima, na Dunia inatambua kuwa kuna nchi ambayo wananchi wake wanadhulumiwa haki zao, mpaka haki za kuishi kwa sababu tu ya kumkosoa mtawala.
Jitenge na uovu, thamini uhai wa mwanadamu mwenzako kama ulivyo wa kwako.
Hata mbele za Mungu, hakuna amri iliyo kubwa kama amri ya UPENDO. Ukimpenda mwanadamu mwenzako kamwe huwezi kumwua au kumtia ulemavu eti kwa vile tu amekukosoa.
Tunamshukuru Mungu mpaka hapo hali ilipopofikia, tunaomba mkono wa MUNGU uzidi kuwafikia waovu wote ili siku moja wajutie uovu wao, watubu na kumrudia Mungu wa kweli, MUNGU wa upendo.