Kwa Tofauti hizi za gharama za uwanja wa Mkapa na Samia, kuna haja ya Maslahi ya Watumishi kuangaliwa upya

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Ni zaidi ya miaka 15 ishapita tangu uwanja wa Mkapa ujengwe lakini tofauti ni kubwa sana mbali na kwamba Uwanja wa Samia ni nusu ya Uwanja wa Mkapa

Hii inaonesha na ni ushahidi piq kuwa mambo mengi yamebadilika na gharama za maisha zimepanda pia hivyo kuna haja ya watumishi kuangaliwa maslahi yao pia

Ingawa pia inawezekana ubora wa uwanja wa Samia uko juu zaidi lakini si kwa Tofauti hii ni lazima gharama za maisha zimebadilika au kuna harufu ya upigaji .
 
Rais ajaye lazima awafunge wote kasoro Samia na chawa wapya
 
Ni sahihi maana hapo sababu kubwa utaambiwa ni gharama
 
Haya sasa yashazoeleka.
Acha wakwibe tu.
Wananchi tujitahidini kuwa wazalendo kwa kulipa kodi.
Mengine tumuachie Mungu
 
Bilioni 280 zinajenga barabara ya moro- dar kilometa 190, kwa gharama ya bilioni kwa kilomita, na chenji inabaki, hakuna haja ya PPP. Hiyo foleni ya ajabu ajabu kwisha kabisa, kwa maslahi ya watu milioni 60, sio kikundi cha watu 30,000 kinachojikusanya kwa mwezi mmoja
 
Wengi wanaolalamikia gharama za huu uwanja wanatumia hisia kuliko factual analysis. 15 years ni muda mrefu kwa teknolojia, standard za uwanja kubadilika.

Mfano, Uwanja Mpya wa Alasaine Ouattara, umejengwa kwa Bilion takribani 600. Hiki ni 60,000 seaters vs Arusha 30,000 seaters. Na kwa kuwa vyote ni AFCON Modern Standards, it's logical hicho cha Arusha, kucost about half of alasaine's.
 
Hii tofauti ni kubwa sana hata kama huu uwanja (Mkapa) ulijengwa miaka 20 ilyopita..

Ingekuwa unagharimu kati ya 100 na 150b ingeweza kueleweka kwa kigezo cha thamani ya fedha yetu kwa kipimo cha dola ya Marekani kushuka sana..

Lakini kwa gharama hii, I doubt kuwa kuna kuongezwa kwa gharama hapa kama walivyofanya kwenye reli ya SGR..
 
Ndio maana anasema ikiwa kila kitu kimepanda bei, basi maslahi ya wafanyakazi yaangaliwe upya!
 
Kama kuna ongezeko la gharama za maisha basi na watumishi wote hayo maongezeko yawe yanaonekana
 
Wakiombwa wajenge scheme ya mashamba kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji,watajivuta sanaaa
Ohh pesa hakuna blah blah kibao
Ila kujenga uwanja sjui arena ilii vijana wakate mauno ni chap chap

Ova
 
Kwenye mipango yao wanasema gharama zimeongezeka ila kwa maslahi ya Wananchi wanasema Pigeni kazi hakuna mwaka maisha yamekuwa rahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…