Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Sijafuatilia utekwaji na mauwaji ya huko nyuma. Lakini kwa hili na mauwaji ya Ali Mohamedi Kibao nina uhakika vyombo vya usalama havijahusika.
Waliohusika ni kundi lenye nia ya kuleta fujo nchini na ni wapinzani wa chama tawala.
Waweza kuwa ni wakereketwa wa chama chochote kile cha upinzani na hata Chadema chenyewe.
Kwa maana hiyo hilo kundi halikutumwa na vyombo vya usalama na wala viongozi wa vyama vya upinzani isipokuwa wameona wakiongeza kasi ya matukio ya namna hiyo katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi basi kutatokea sintofahamu na kuitikisa nchi kwa maslahi yao.
Sababu kuu ya kuamini hivyo kwanza ni aina ya mtu waliyemlenga ambaye ana nafasi kubwa kwenye chama cha Chadema na namna walivyoamua kumuua.
Ingekuwa ni ugomvi na visasi vya kawaida basi wangemfuata nyumbani kwake na usiku au akiwa kwenye gari yake au ya ndugu zake ili isiwe rahisi kuleta hisia kwa wananchi.Badala yake wamekwenda kumkamata ndani ya basi na mchana kweupe.Kule walikomtupa ni maeneo yale yale maarufu wanakopatikana watu waliouliwa kiujambazi.
Kwanini wasimzike kwenye kaburi ambalo ingechukua muda kugundulika.Madhumuni yao ni kufanya matangazo kutokana na kifo chake ili kutokee fujo.
Kwa tukio hili sasa ndio uwezekano wa kupatikana waliokuwa wakitenda mauwaji watajulikana na kitendawili kuteguliwa pindi serikali itakapotia nia kulihitimisha.