Kwa tuliosoma kayumba: Leo tukumbushane vitu tulivyokuwa tunatumwa na walimu wetu enzi tukiwa shule za msingi

Kwa tuliosoma kayumba: Leo tukumbushane vitu tulivyokuwa tunatumwa na walimu wetu enzi tukiwa shule za msingi

Nimesoma kayumba ya wilayani, haikuwa mjini sana ila sio kijijini kabisa. Fagio za chelewa, majembe, nguzo za kujengea jengea sehemu za nyasi, maua, maji na kuni.

Wasichana ilikua kawaida kuagizwa wakachote maji kupeleka kwa walimu. By the way dingi alikua ticha so nimekula sNa mseleleko wa kudoji kazi sometimes.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alooooo tulikuwa tunawachukia watoto wa walimu maana umbea wote kwa baba au mama zao waalimu ila walikuwepo watoto wa walimu wamepinda mbayaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3] wanalishwa vitu laini laini kwa hiyo hawana nguvu za kutosha, enzi zetu umechumiwa fimbo mzigo wa kuni zote zinakuishia mwilini

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka kwa wiki tulikuwa tunafunga hesbu ya viboko kwamba tumechapwa vingapi, mtu unakuta umepigwa viboko mpaka 200 kwa wiki moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkonge kwaajili ya kutengenezea katani
unachapa mkonge kwenye mti mpaka upate katani
baada ya hapo unasuka kamba ya katani somo la stadi za kazi
unawashwa unavimba maana mkonge unawasha ila unavumilia uondoke na alama

nibu kwa ajili ya kuchorea herufi hii inatokana na fimbo za mianzi unachonga kwa mbele inakuwa na ncha unachovya kwenye wino unachora herufi hiz zilikuwa tofauti sikumbuki

kulima mahindi mwisho wasiku mnavuna yanachemshwa mnakula wenye ubavu walikuwa wanakimbia na sufuria la.mahindi wengine mnakosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakumbuka mwalimu wangu alikuwa anatengeneza kashata, asubuhi akijanazo kiongoz wa darasa anapewa amuuzie,sasa balaa linapotokea usiponunua. ikatokea darasa linasumbua alaf mara paaaap akatokea na majina ya wasumbuf wameandikwa na jina la Call911 lipo kwenye list ya wasumbufu, chakwanza mwalimu anakuambia wewe hununuagi kashata, una fimbo 5 zakashata na 5 za usumbufu. ukipigwa fimbo 10 kesho inabid uje na hela ili kwenye kipind chake ununue kashata ndio idadi ya fimbo unapunguza lasivyo 10 zinakuhusu
 
Back
Top Bottom