William Mshumbusi
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,761
- 2,391
Tunaomjua Zitto vizuri na Mbowe hawatuchanganyi kabisa.
Mwaka 2010 baada ya UCHAGUZI mkuu wabunge wa upinzani walikusudia kususia bunge kwa sababu kama hizi hizi. Wakati huo Tundu Lissu, Heche na Mdee walikuwa moto kweli. Walilia dhulma dhidi ya wagombea wao wengi sana wa ubunge na kutangazwa kwa shida kama Wenje na yule wa Shinyanga.
Bunge lilipoanza wakasusia hotuba ya Rais Kikwete. Wakakataa kumtambua kama Rais.
Wakati huo Zitto akawa kinara wa usaliti kwa lugha yao. Walitoka wote wakati wa hotuba Ila Zitto akabaki. Wabunge wa CCM wakamshangilia sana Ila waupinzani wakamuona msaliti. Asubuhi yake Zitto akaamkia TBC kuwaponda wenzake. Wabunge wa upinzani wakaazimia Zitto afukuzwe uanachama. Mbowe akamkingia kifua. Baada ya Muda JK akatangaza mchakato katiba mpya Mbowe akamtambua JK kuwa Rais, movie ikaishia hapo.
Kinachousumbua upinzani na uslmi wao wote ni njaa. Wakiwa wabunge wanaishi maisha ya kibepari huku wakifanya harakati uchwara.
Je, Mbowe na Halima Mdee wanaweza kufanya harakati nje ya mishahara na marupurupu ya bunge?
Je, wakati wameamua kurudi bungeni mwaka 2010-2011, hali ya kisiasa ya kisiasa ilibadilika au waliangalia posho zao?
Mpaka sasa kwanini Mbowe na Mdee wapo kimya kutoa mitazamo yao?
Je, wakipitisha majina ya viti maalumu nne ya Mdee na Bulaya je Mdee atawaunga mkono waliopitishwa?
Je, Chadema, ACT na CUF wanauwezo wa kulisusia bunge mazima na kuliacha kuwa la chama kimoja complete.
Je, Chadema inaweza kumfuta uanachama mbunge wao pekee?
Kifupi lazima kila hatua wanayochukua ije na majibu ya namna ya kutibu njaa zao binafsi tofauti na hapo chama kitapasuka.