Uchaguzi 2020 Kwa uelewa wake, Lissu anaamini kabisa kuwa atakuwa Rais wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Kwa uelewa wake, Lissu anaamini kabisa kuwa atakuwa Rais wa Tanzania

Mtu anaweka youtube maelezo kwa kichaga, na kumsifu Lissu wa CHADEMA ya wachaga halafu unaleta tukubaliane naye? Mutahangika sana kutaka kutawala nchi kwa kuungwa mkono kikabila, lakini mutafeli. Population yenu haiwawezeshi kutawala nchi!
Hata mngekuwa mamilioni mangapi majambazi lazima yaachie ofisi ya uma
 
Lissu ana andaa wasifu,pindi akifa lazima waseme kuwa amewahi kugombea urais kwa jamuhuri ya Tanzania na kupata asilimia 15.
Nina wasiwasi na wewe kama ulifanya vizuri kwenye somo la uraia/ civics/general studies/development studies.
 
Nina wasiwasi na wewe kama ulifanya vizuri kwenye somo la uraia/ civics/general studies/development studies.
Nimesoma vizuri sana tu mkuu ndo maana hadi Leo ninao uwezo wa kubaini kuwa lissu hana elimu ya uraia na uzalendo kwa nchi yake ni zero kabisa huyu dubwana
 
Hata mngekuwa mamilioni mangapi majambazi lazima yaachie ofisi ya uma
Tatizo ni mpangilio wa vyama vya upinzani. Viko kama ad abracadabra ya watu wa mazingaombwe. Mi ningefurahi sana CCM wakiachia ofisi na kukabidhi Chama kama ilivyokuwa CUF ya Lipumba na Maalim. Lakini CHADEMA ya vijana wa form 6, nooo!
 
Wakuu habari za Leo?, Nimatumaini yangu kuwa hamjambo.

Naomba kumzungumzia huyu Mgombea wa CHADEMA, mheshimiwa T.A.Lissu, nimejaribu kuhudhuria kampeni zake kama Mara nne hivi lakini hakuna nilichokiambulia tofauti na kusikia habari za risasi kumi na sita kiunoni na mbaya zaidi kampeni nzima unakuta imetawaliwa na neno CCM na Magufuli utadhani kuna vyama viwili tu vinavyoshindana kwenye uchaguzi huu.

Kinacho nifanya niamini kuwa Lissu anapoteza muda wake na itamuwia ngumu kwa chama chake kupata japo wabunge watano ni juu ya tabia yake ya kupinga na kudharau kila kitu kilichofanywa na serikali ya CCM ya awamu ya tano na hivyo kupelekea kukosa muda wa kuinadi ilani ya CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa kudharau juhudi kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano kumekuwa kukiwakera sana wapiga kura na wengi wamekuwa wakisisitiza kuwa huyu bwana (Lissu ) ajikite kwenye kumwaga sela na ilani ya chama chake.

Mwisho lissu atambue kuwa watanzania wengi wameshamshitukia kuwa kuna nguvu nyuma yake ambayo haina nia njema na taifa la Tanzania pamoja na raslimali zake hivyo kumpa kura Lissu ni kuikabidhi Tanzania na raslimali zake mikononi kwa Mabeberu na baadae kupelekea machafuko katika nchi yetu.

Huwezi kuambulia kitu kutoka hotuba za Lisu, mpaka uwe na akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom