Kwa ufaulu huu kidato 6, 2023. Bila upanuzi vyuo vikuu ni Div one tu wataingia vyuo vikuu

Mm baada ya kuona dogo anayeshinda kwenye madubu amepata div 2 ya pcm nikaamua kutafuta papers za mitihani hiyo.

Nikakuta kwamba mwaka huu mtihani wa physics F6, definition tu ilipewa marks 5. Halafu hesabu za kidato cha 3 na 4 zilikuwemo nyingi.
Basi itoshe kusema kuna upanuzi wa goli. UDSM warudishe marticulation paper ili kuchuja watu.
 
Basi itoshe kusema kuna upanuzi wa goli. UDSM warudishe marticulation paper ili kuchuja watu.
Wakiwapa hiyo matriculation wasahihishe NECTA na walimu wao wa sekondari itapigwa tu. Tatizo ni msahihishaji na maelekezo tola kwammikiki.
 
Wanafundishwa kufaulu na sio kitu kingine
 
DR. Msonde enzi zake akiwa Katibu Mtendaji wa NECTA angesema matumizi ya vishikwambi kwa walimu yamechangia matokeo mazuri kwa vijana wetu mwaka huu. Yule alikuwa anajuwa kucheza na furusha akalamba unaibu Katibu Mkuu asubuhi tu mapema.
 
mitihani ilikuwa rahisi sana, ngoja nitafute papers hizo
Mkuu ni siasa chafu.
Watoto wana siri nzito.
Mimi kuna baadhi ya wanafunzi shule tofauti wamefunguka magumu...fanya kautafiti utathibitisha hili
 
Ila imenishangaza kusikia kuwa Hesabu imeongoza kwa ufaulu kidato cha sita au niseme masomo ya saiyansi ndio yameongoza. Nikawa najiuliza, ni ile ile mitihani ya PCB/M tulikuwa tunafanya sisi wahenga au kuna mabadiliko?
Hii nchi haiaminiki[emoji23]
 
Ni kweli, wametengenezewa mazingira ya kufaulu kiurahisi pia NECTA wanalegeza
 
PIA MITIHANI INAVUJA SANA, UNAKUTA HADI GOVERNMENT SCHOOLS soft copy zinawafikia
 
PIA MITIHANI INAVUJA SANA, UNAKUTA HADI GOVERNMENT SCHOOLS soft copy zinawafikia
We hutaki ziwafikie
Acha watoto wafaulu tena wote wangetakiwa wapate div One

Viongozi wenyewe ndiyo hawa tulio nao!!! Acha watoto wafaulu tuu

Maisha ndiyo haya haya mafupiiiiii kama mkia wa mbuzi

Acha tupate raha ya watoto kufaulu tukate na keki huon shilole alivo furahi???

Nasemaje panueni goli zaidi watoto wafaulu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Na hili ndio tatizo kubwa , watu wanajipanga kufaulu tu mitihani sio kuelewa masomo .
 
Siku hizi siasa zimeingia Kwenye elimu.

Walimu wanajazishws mafomu na CCM[emoji28]

Wakuu wa shule wanapigwa biti ole wao wafelishe wanapigwa chini.

Shule za private Wana BAJETI kabisa ya paperz[emoji28]

Cheating inahusika pia.

Mimi Kuna dogo mmoja namjua Wala Hana maajabu ila alipiga wani Kali sana[emoji1787][emoji1787] tena six

Hii nchi Ina vituko Kila kona kumejaa vituko

Mara bandari iuzwe , mara hivi yaani ni shida!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…