Fund man
JF-Expert Member
- Feb 24, 2021
- 3,629
- 4,831
🤣🤣🤣🤣🪑mitihani ilikuwa rahisi sana, ngoja nitafute papers hizo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣🤣🪑mitihani ilikuwa rahisi sana, ngoja nitafute papers hizo
Ndio maana wanafeli sana hata vyuo vya kati.Siku hizi Watoto wa Form I- Form IV hawasomi Supplementary Books kama zamani...
Hata hivi vitabu vya ziada ukivitafuta havipo:
1. Abbot
2. Lambert
3. Tropical Biology
4. Introduction to Biology
Hivi vilikua vinapanua ubongo wa mtoto O- level
Inamuandaa ku solve Complex problem level za juu
Siku hizi ni mwendo wa simple text books+ summary books+ National past papers books
Kuna mabadiliko maku wa sana mkuuIla imenishangaza kusikia kuwa Hesabu imeongoza kwa ufaulu kidato cha sita au niseme masomo ya saiyansi ndio yameongoza. Nikawa najiuliza, ni ile ile mitihani ya PCB/M tulikuwa tunafanya sisi wahenga au kuna mabadiliko?
Sasa mtu kasoma arts wewe unamwuliza maswali ya physics kweli? Kwani wewe ukishtukizwa hapo utaweza? Tuache hizo!Wakati nikiwa likizo nyumbani nilitembelewa na kijana mmoja aliyemaliza Form 6 akiwa na DIV2 akiniomba nimsaidie kupata chuo Marekani ninakofanyia kazi zangu. Nikamfanyia usaili wa haraka haraka wa Calculus na Physics nikamkuta ni mweupe kabisa. Inawezekana mitihani ya siku hizi inahusu maswali basic tu au ni maswali yaliyokwisha jirudia sana kiasi kuwa wanafunzi wanakuwa wanajiandaa kwa kutumia past papers tu bila kuwa na deep understanding ya subject matter.
Enzi ta akina Nape kulikuwa hakuna Civics bali kukikuwa na somo la Siasa! Matokeo ya kutunga haya!
Angekuwa amesopma Arts asingeniomba nimsaidie chuo cha EngineeringSasa mtu kasoma arts wewe unamwuliza maswali ya physics kweli? Kwani wewe ukishtukizwa hapo utaweza? Tuache hizo!
Nafasi za vyuo ni nyingi kuliko waombajiMatokeo ya kidato cha sita 2023. Karibu shule zote daraja lenye idadi kubwa ya waliofanya vizuri ni daraja la kwanza ( Division one). Kwa matiki hiyo mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza;
1. Kama vyuo vikuu vitachukua wanafunzi kulingana na uwezo wake kama miaka ya nyuma ni dhahili kuwa wanafunzi watakao ingia vyuo vikuu vyote vya umma na binafsi watakuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza tu.
2. Kama vyuo vitalazimika kuongeza idadi ya wanafunzi pasipo kwenda sambamba na kuongeza miundo mbinu yake na kuajiri wahadhiri wengine hasa ukizingatia muda haitoshi kulingana na kuanza mwaka wa masomo Oktoba ni dhahili itasababisha kushuka kwa ubora wa elimu itakayotolewa.
3. Tutarajie shule za binafsi kuanza kukosa wanafunzi. Kwani kwa matokeo ya mwaka huu ufaulu umekuwa wa kufanana kwa shule zote, zile za vipaji maalumu, shule za binafsi na hata shule za bweni kawaida na zile za kata Zipo shule za bweni kawaida hazijatoa hata wanafunzi wa daraja la tatu au la pili kabisa. Kwa sababu hiyo wazazi hawataona sababu ya kuwapeleka watoto wao shule za kulipia wakati ufaulu hautofautiani na shule za bure za umma.
Ni wakati wa serikali kujipanga sasa na kukabiliana na ongezeko la ufaulu huu mkubwa kwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Kwa mfano kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha tano kufungua shule Julai kama ilivyozoeleka na kusongeza mpaka Agosti ni ushahidi wa waziri kuwa serikali haina mipango ya muda mrefu. Huu siyo wakati wa kujenga madarasa kwani walitakiwa kuelewa mapema kuhitajika kwa madarasa.
Wataalamu wao wa Chuo cha Mipango Dodoma wanatakiwa kutumika mapema kuepusha uzembe wa aina hii.