nilijirudia mie na basi la elfu 38,000 /mie natafuta hela kwa tabu then niwape tu alafu huko ndani wanakutembezea vibiscuti ununue tena ,na juice kabox kadigooo 8000/=hahahah nikawaambia mark my face sintapanda hii fast jet tena mimi.bora ndege nyingine ni ghali ila tamu tamu unapewa .jamani kama kuna mtu aliyewahi kupanda hiyo ndege kwa 32+vat isizidi 50,000/= aje atuambie hapa maana nimkwenda mwanza 190,000/=
Kama nina flight ya JRO - JNIA, sina haja ya kutafuna chochote, nitaspend kutafuna kama niko on the road with Dar Express, etc. Kama naweza kulipoa let say 75,000 na nikatumia 50 minutes kufika Dar from Kilimanjaro, kwanini nihangaike na vyakula humo angani, na kama ndo inakufanya uboard precision kisa misosi, pole.
Ni jana tyu nimemfanyia jamaa yangu booking mbili from Mwanza, kuna ya next week bei ni 43,040
ni nyingine ni ya kesho, 75,040. Kazi ni kwako, the earlier the better mzee.
Binafsi sijawahi kukutana na kero kutoka kwa FastJet zaidi ya huduma zao Bora na za gharama nafuu.
Mtoa mada huenda ulikwenda kulipia wakati muda uliopangiwa ukiwa ume-expire,
Juzi tu nimetoka kumnunulia mtu Tiketi kwa Tsh 43,000 JRO-DAR... Fare 32,000 Taxes 11,040
Pia Bei ya Tiketi y ndege siyo Fixed, inabadilika muda wowote, unaweza kuulizia bei sasa hivi na ukitoka kidogo ukarudi ukakuta imeshabadilika.
Hivyo malalamiko yako haya kuna mahali ulishiriki kujikosesha flight (kwa uzembe) au una lengo la kuwaharibia biashara yao.
Pia kuhusu Reporting time, wameonesha kabisa kuwa unatakiwa uripoti 40 minutes before departure. Na kwa msisitizo ukienda kukata tiketi huwa wanakushauri uripoti hata saa moja kabla ya kuondoka, ukizingatia haya, kamwe hutaachwa na Ndege na hutakumbana na unachoita Uhuni wa FastJet...
FastJet - Safiri kwa uhakika na kwa bei nafuu.....
I am glad that you have said it pretty well.
Hapo mtawalaumu fastjet bure,wabongo washaingia kati hapo wanachakachua tkt.ninaamini kabisa kuna staff wakisaidiana na wenzao wanabook tkt zote kisha wanaziuza kwa watu wao wanaowajua huku wakipewa cha juu
Tanzania itajengwa na Watanzania, lakini pia inabomolewa na Watanzania.
...Msiwalaumu sana i love them na ndo wanaleta changamoto kwenye usafiri wa anga maana precision walikua wanajiona babkubwa sana
Na delays zao zilikuwa so noma mpaka zikawa normal. At least upinzni upo, na utazidi kukua, naombea hawa jamaa waanza na hizo route za Entebbe, naskia skia inaweza kuwa kama laki unusu. Ndo upepo wa usafiri utabadilika sasa. Kukaa siku mbili njiani hakuna tena.
Wakuu labda mimi nina bahati au pengine mleta hoja hawakuelewana na muhudumu wa Fastjet.
Binafsi safari zote za kikazi (zinazohusisha Arusha na Dar) nasafiri na fastjet kwa sasa, Precision nimewakimbia kabisa.
Nimeshasafiri na fastjet zaidi ya mara 8 (return tickets) na mara 6 nimelipa nauli ya chini kabisa ya Tsh. 32,000 na mara 2 nimelipa around Tsh. 55,000 hivi.
Nafikiri pengine watu hawazingatii muda wa kwenda kulipia booking zao, binafsi huwa na book safari zangu at least two weeks before na nikiisha book siku hiyo hiyo naenda kulipa pesa yao. Hii inaepusha usumbufu unaoweza kutokea wa bei kubadilika kadiri muda unavyosogea kuelekea siku ya safari.
Nimesikia matangazo yao kuwa unaweza sasa kulipia kwa MPESA, nafikiri hii ndo itaondoa usumbufu wa kubadilishiwa nauli siku ukienda kulipia.
Huo ndo uziefu wangu na Fastjet kwa safari nilizofanya nao.
Ooh nimesahau, faida yao nyingine ni kuwa wanajali sana muda.....on-time departures 100% mpaka raha!!
Mkuu, umenena vyema, I fail to understand shida ambazo baadhi ya watu wanaclaim wame-experience. kwa upoande wangu, kila booking ninafanya na malipo within the specified time, hapo hakuna mhudumu yeyote anayeweza kunibabaisha. Just give then the name na booking reference, off you board.
Na kwenye muda nimewakubali sana, there's no objection kwenye hilo. Naiombea isife tuendelee kunufaika na usafiri huu, time saver.
kaka yagu pole sana kwa yaliyokukuta, mimi naomba niulize je ulifika ofisini fastjet saa ngapi kulipia hiyo tiketi yako? maana kama ulifika muda ambao tiketi yako isha expire utakuwa unalaumu fastjet bure, kwenye story yako hujaandika ulifika ofisini saa ngapi? na ulipata a cheap price maana uliwahi kufanya booking muda wa saa mbili asubuhi mpaka nane mchana wanafanya booking wengi na siti zinajaa ndo maana walikupa hiyo bei ambayo pia ni reasonable and fair, japo aloongea na wewe hakuwa na lugha nzuri, fastjet kwa maoni yangu haina tatizo ni watanzania tu kupata elimu juu ya low cost carrier airline na huduma zake, tutaizoea tu. taratibu ndo mwendo
For sure there is wisdom in your paragraph. Ahsante wa ufafanuzi mzuri sana. i hope mtoa mada atarejea kutueleza alikwenda kulipia booking ndani ya muda gani, vinginevyo this might turn to defamation.