Nadhani pia kuna haja watu kujielimisha kuhusu taratibu za kiuchunguzi, haswa linapokuja suala la miamala ya kifedha. Pia ni vyema kujua kama taarifa iliyowasilishwa ni statement ya miamala au ni nakala za risiti anazopewa mteja pindi anapoweka fedha kwenye akaunti yake au ya mtu mwingine.
Mfano, taasisi kama TAKUKURU, Police, Mahakama etc wanaweza itisha nyaraka za kibenki/kifedha kwa utaratibu maalum endapo kuna kesi au tuhuma za kiuchunguzi. Hizi taasisi kama mabenki huwa zina legal departments ambazo hufanya upembuzi wa maombi ya nyaraka kabla hazijatolewa.
Chukua mfano wa kesi ya utapeli wa kimtandao, unaestablish vipi kesi kama hutakuwa na ushahidi wa miamala?.