kuongea jambo hili huku kupaa kwa mafuta, hakuna anayejitokeza kutoa ufafanuzi nasi tupo tu.
Watanzania ni nani aliyewaloga?
Nimekusoma, na nikaona tu nijibu hayo maneno manne tu uliyomalizia mwisho wa andiko lako.
Hayo maneno manne, "WaTanzania ni nani aliyewaloga" limeulizwa mara nyingi sana tokea JF iwepo, na pengine hata huko kwingineko kunakojadiliwa maswala kama haya.
Hakuna mchawi wa muda wote. Sasa hivi mchawi ni kundi la watu ambao wameamua kuwatumia watu kama akina Camillius, Mombo, ****** na wengineo.
Hakuna mchawi mmoja wa kudumu; na hakuna aina moja ya matokeo ya uchawi.
Nyerere aliwaloga waTanzania kutambua heshima ya utu wao na wa binaadam kwa ujumla. Ndiyo maana waTanzania wa wakati huo walikuwa tayari kutoa damu yao kuwasaidia wenzao waliohitaji katika mapambano yao.
WaTanzania wakajuwa thamani ya kujiletea maendeleo kwa kutegemea raslimali zao zilizopo, kama watu, ardhi, elimu.
Watu walilogwa kwelikweli kuhusu hayo, licha ya matatizo yaliyokuwepo wakati huo, mengi yakiwa ni kutokana na hali ya kidunia kwa ujumla.
Alipoondoka Mwalimu Nyerere, wakaingia wachawi wengine, na wao wamefanya kivyao kwa kiasi walichoweza kueneza uchawi wao miongoni wa waTanzania; hadi leo hii tukawa katika hali tuliyomo sasa..
Kwa hiyo, ni maoni yangu kwamba hakuna mchawi mmoja wa kudumu anayewaloga waTanzania.
Tukibahatika, tunaweza kumpata mlosi mwingine atakayeleta aina tofauti na huu unaotukabili sasa hivi.
Sali sana na omba kama wewe ni muumini wa chochote chenye nguvu kinachoweza kuleta hali hiyo ya mabadiliko chanya.
Uchawi wa Samia na kundi lake, sidhani kama kutatokea wa kuufikia katika kulididimiza taifa hili na kuwalaza akili waTanzania.