shampondo shila
Member
- Jan 14, 2020
- 19
- 42
Nikiwa zangu nimetulia na familia yangu chini ya mti hapa nyumbani akaja paka na mwanae wakakaa pembeni yetu kama kawaida kwa paka wanaoishi vizuri na binadamu hawaogopi hata wanaweza kukuchezea kama kuku tupia mguu hivi
Basi bhana yule paka mdogo sijui ni shetani gani alimuingia ghafla akakirukia kifaranga cha kuku kilichokuwa kimejikunyata kwa ugonjwa, akakibugia kichwa mdomoni, kifaranga kikaanza kufurukuta,
Nikampigia kelele nikimaanisha amwachie yeye kakimbia nae shambani, nikamfuata huko huko, sikutaka kumuonesha uso wa kukasirika nikambembeleza akamwachia ila amemla kichwa
Nikamwita taratibu mpaka akaingia ndani, nikafunga mlango na dirisha, nikaenda kuchukua kipisi cha nondo, nilichomfanyia Mungu tu anisamehe maana hayupo tena duniani,
Kama umewahi fanya ukatili kwa myama yoyote na wewe tubu hii dhambi kwani ni dhambi kama dhambi zingine.