Kwa Ulinzi wa Dotto Biteko, Serikali itunge sheria kudhibiti matumizi mabaya ya Ofisi

Kosa la Mh.Biteko ni nini katika huo ulinzi ?!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Nchi yetu imejaa wanafiki na machawa. Ukiwa kiongozi, usipokuwa na hekima, machawa yanaweza kukufanyia vituko vya kila aina ya kukupamba, na ukiwa mjinga utafurahia na kukenua meno.

Kwa hiyo watu wanaokuzunguka wanafanya kwa kuona wewe unapenda nini. Kama wakigundua unapenda sifa, watakupamba kwa sifa, nawe kwa ujinga utaona kama vile tangu Ulimwengu uumbwe, hakukuwahi kuwa na mtu mwema na anayefaa kwa uongozi kama wewe.

Wanayoyatenda wasaidizi wa Biteko au hata walinzi wake yatakuwa yanaashiria hulka yake, ndiyo maana Dr Mpango alipoona ujinga wa askari wa kusimamisha magari zaidi ya masaa mawili ili yeye apite, alikemea kwa nguvu, na ikaisha. Ila kwa huyu nadhani watu wanaweza kusimamishwa hata masaa matano, atabakia anafurahia. Unaibu Waziri Mkuu, ambao haumo hata kwenye katiba ya nchi, na wala hauna mamlaka yoyote ya dola, wala hachaguliwi na wananchi, mtu akamwue kwa nia ya kupata nini?
 
Lazima Serikali ya CCM ifanye hivyo na ukiona hivi ujue hali ya usalama na amani ya Nchi si shwari. Hawa jamaa wanawindana wao kwa wao kama pongo Serengeti. Hali si shwari.
 
Yaah hatari ipo....

Hasa kutoka nje ya nchi.....

Uimara wa ulinzi wa viongozi ni kuiheshimisha DOLA....

Likitokea lolote kufanywa na "intruders" na baadaye kujulikana...huwa ni aibu NDANI NA KIMATAIFA.....

#Karibu Komoni Hapa Kwa Mama Lili Majohe Rada[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sasa nchi ya amani kama hii ulinzi wote huo wa nini hata Rais wa marekani hana ulinzi huo
Kupanda cheo au kuogezewa majukumu kumesababisha maadui wake au wa serikali waongezeke au ni mbwembwe tu za madaraka!
Huyo ni waziri mkuu ajaye na usijeshangaa akawa rais ajaye 2035.
 
Lazima Serikali ya CCM ifanye hivyo na ukiona hivi ujue hali ya usalama na amani ya Nchi si shwari. Hawa jamaa wanawindana wao kwa wao kama pongo Serengeti. Hali si shwari.
Duniani kote hali huwa si shwari...

Wako wanaowatarget viongozi kwa VINYONGO ,WIVU ,HUSDA ,CHUKI...

Wako wanaowatarget viongozi (kutoka ndani na hasa nje) kupima uimara wa dola na hata KUIAIBISHA DOLA kimataifa [emoji1787][emoji1787]

Karibu Wanzuki[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Idadi hubadilika kulingana na mahali na tukio. Lakini kama lilikuwa swala la kawaida, aisee hao ni wengi sana..

Nimeshakutana na VP mara kadhaa, hana walinzi wengi namna hiyo. PM pia hana cycle kubwa ya walinzi kama huyo VPM.

Ni wengi sana aisee!.
 
Mbona walishindwa kumlinda Magufuli asife kizembe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…