Si huwa nasikia hawa Jamaa wamekomaa sana, huwa hawaumii hata wateswe vipi, pia wanajua Uchawi ( Mazingaombwe ) na kwamba wanajua Kupigana tena ile Combat Karate / Combat Kung Fu kiasi kwamba Komando Mmoja anaweza Kupigana na Watu kati ya 25 mpaka 50 na Wote akawafletisha / akawashinda hata wakiwa na Silaha na Yeye akiwa hana kutokana na Mafunzo ya hali ya juu aliyonayo?
Sasa hawa wa Kesi ya Mbowe imekuwaje hadi wakaweza Kukamatwa kirahisi kama Panya Buku wa Mtwara, Ruvuma na Lindi mpaka Kuteswa hivyo na wanabaki tu Kulalamika Mahakamani?
Kuna Komando Mmoja aliwahi kuniambia kuwa Makomandoo Wanne tu wakiamua Kukinukisha Dar es Salaam nzima na tuwe tunalala Saa 9 Alasiri au Wote tujifungie ndani kwa Uwoga huku tukijinyea na Familia zetu wanaweza kutokana na Mafunzo yao ya hali ya juu.
Kwa wale Makomandoo niliowaona Juzi uwanja wa Uhuru Siku ya Uhuru na ule Umahiri wao, Ukomavu na Ukakamavu wao wa hali ya juu KEROZENE naanza kuhisi kuwa huenda hawa Makomandoo wa Kesi ya Mbowe siyo Makomandoo kweli bali ni Samjo Samjo / Waongo Waongo tu.