Kwa umahiri mkubwa wa Makomandoo wetu ilikuwaje wale wa Kesi ya Mbowe wakateswa na Jeshi la Polisi kama walivyodai?


Achana na movie za Rambo njoo kwenye uhalisia.
 
Hata uwe special force kutoka SEAL TEAM huwezi kupambana na system.. polisi wakija kukukamata wawili ukiwapiga wanakuja wanatano , ukiwapiga watakuja 10 na bunduki bora zaidi , ukifanikiwa kuwapiga watakuja 30 na vifaa bora zaidi.
Kwa mtu mwenye akili kama hana complete plan ya kutoroka ni bora utii mamlaka na ukubali kukamatwa..

Labda pale vita iwe kati ya macomando wote vs polisi kwamba hata wale makomando wanaweza kuita reinforcements
 
Hao jamaa kuwa hai hadi leo ni ukomandoo tosha. Maana walitumia akili kudeal na watu waliokua tayari kuua na kukupoteza. Sasa kwa akili ndogo unadhani kwamba kila komandoo anapokamatwa basi mbinu yake ni moja tu kupambana kwa mabavu kijinga jinga. Kutumia akili hadi ukawa hai kwenye mazingira ya kuuawa ni ukomandoo wa hali ya juu sana. Hao sio akina ziro wenye akili mbili akiambiwa piga risasi pale yeye anapiga tu na kudai amri imetoka juu. Hao wamepikwa kiakili pia.
 
Komando wa ukweli yuko tayari kufa kuliko kudhalilishwa
 
Nani kakwambia hawaumii?

Tofautisha kati ya kujikaza (uwezo wa kustahimili maumivu bila kulia) na kutoumia

Hao hadi mapenzi yanawaumiza sa sembuse mateso,?

yani uchukue prise ubinye zile efu moja mia mbili afu na mchizi akavunga kama hakuna kitu umemfanyia....hiyo kitu haiwezekani

Ni kweli commando anaweza kupigana na idadi hiyo ya watu lakini endapo hao watu watakuwa unarmed, nani atakuwa na muda wa kupoteza kuangalia sarakasi zako wakati mkononi ana Glock 19 na iko loaded?

Huyo commando aliyekuambia hivyo alikua ana malengo yake, pengine alitaka akuogopeshe ili hata siku akikukopa ushindwe kumdai

Umahiri wa commando haupimwi kwenye maonyesho, ni sawa na mtu aseme bondia wa ulimwengu apimwe kwa kuzingatia idadi ya makonde anayopiga kwenye punch bag

Umahiri wa komando upimwe kuzingatia opponent aliyekutana naye, akutane na komando mwenzie wa nchi nyingine wazichape tuone who deserves to be commando and who should be recognized as sungusungu
 
Wew ni mpumbavu wa akili na ufaham wako umelala fofofo. Walikamatwa na police , kua komando ni pamoja na kujua kutii mamlaka ya serikali. Ndio maana hawakuweka resistance ktk kukamatwa. Wew ushatoka kuangalia muvi zako za kutafsiriwa unaleta uzi wa kiboya. Unauliza maswali unajijibu
 

nakukumbusha komandoo ni mtu kama wewe,ndio maana alilia wakati fulani.

hata yeye mahakamani alijibu,"labda komando wa kwenye movie"mbona hata polisi wawili wanamshika vizuri tu!!!

ishu ya kufanya vurugu hata wewe unaweza muhimu ushibe vizuri tu.ila uwe tayari kwa matokeo baada ya hapo.
 
Vitengo walivyokuwa wanafanyia kazi walivitaja na kueleza kila kinachohitajika kwenye maswali waliokuwa wanaulizwa na kujibu kiufasaha kama wako huko.

Mazingira waliokamatiwa kwanza ujue hayakuwa wafanye kama unavyotaka.

Hawakufanya vurugu wamepewa kesi isiyoyakweli je wangelifanya si mlikuwa mje na hoja nyengine za kusema ni magaidi kweli kwanini hawakutii kukamatwa.

Sasa mlichokuwa mnatarajia ili wafanye kwa vitendo hawakufanya na kama kweli hawo policcm ni mabingwa wawekeni uwanjani tujue nani comando.
 
Mleta mada unamaanisha akija polisi dogo dogo unayemzidi kimo na mafunzo ya kimapigano kwa ajili ya kuku arrest utakataa.
Afu kingine unachopaswa kujua hao makomandoo usidhani walienda kukamatwa kizembe hata hao waliowakamata walijua fika wanaenda kukamata makomandoo kwa maana hiyo walikua wamejiandaa vya kutosha usikute nyuma yao walikuwepo makomandoo zaidi ya kumi wakisubiri jamaa walete nyenyenye af waingie.
Afu kama umemsikiliza Ling'wenya anasema ye kama Askari anajua katika ukamaataji kunakua na in and out yani manake, kuna wale Askari wanaoonekana kuja kukukamata, lakini kuna wale ambao huwaoni Ila wanakuwa around in case ukileta ubishi.
 
Kuna wanajeshi Fulani walikuja kukamata masela waliokuwa wanavuta kijiti karibu na kambi ya jeshi.Walikuja MP wawili na Komandoo mmoja.Kisa ilikuwa mwenzao(mwanajeshi) kuwazingua masela.Sasa akaja huyo komandoo kama chambo,na anajulikana kuwa yeye ni nani mtaani.Basi kaenda maskani katoa elfu 5 anataka kijiti,akawa analazimisha arudishiwe chenji hapo hapo.Ndipo msela mmoja akamuuliza kwani vipi!?Ndipo huyo komandoo akamvamia msela na kuanza kumpa kipigo.Jamaa nae Yuko fiti akajibu mapigo na kumzidi komandoo.Ikabidi Yule komandoo ajikinge uso wake na kung'ang'ania fulana ya msela.Msela akajivua fulana na kukimbia.Wale wanajeshi wengine(MP) waliokuwa wamewazuia masela wengine.Ikabidi yule komandoo awaambie wenzie wawaachie wale masela.
 
Aisee.

Natamani kuelewa ila nimeshindwa.

Kwamba Komandoo alinunua kijiti akanyimwa chenji yake? Afu akapigana akaishia kupigwa? Afu Jamaa aliyempiga akakimbia? Afu Komandoo akawaambia Ma-MP wawaachie Masela?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…