Uchaguzi 2020 Kwa Umati ule 'Kiduchu' wa kampeni ya Bernard Membe tena 'Kwao' Mkoani Lindi ni bora tu angeungana na Tundu Lissu na awe Mgombea Mwenza wake

Uchaguzi 2020 Kwa Umati ule 'Kiduchu' wa kampeni ya Bernard Membe tena 'Kwao' Mkoani Lindi ni bora tu angeungana na Tundu Lissu na awe Mgombea Mwenza wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mpaka hivi leo nawaza na ninamtafuta huyu Mtu (Mtanzania) aliyemdanganya kabisa wazi wazi Bernard Membe kuwa ana 'Mvuto' wa 'Kisiasa' na kwamba 'akigombea' Urais nchini Tanzania kwa Kushindana na 'Mwamba wa Chato' Rais Dkt. John Magufuli na CCM yake (yangu) anaweza 'Kumshinda' na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama kuna Mtu aliyeona Mkutano wake wa Kampeni Bernard Membe tena Mkoani Kwake kabisa (Chimbukoni) huko Lindi na kwa ule Umati 'Kiduchu' alioupata ni kheri tu angejiunga na CHADEMA au kungekuwa na Makubaliano 'Maalum' baina ya CHADEMA na ACT-Wazalendo ili Yeye ( Membe ) awe Mgombea Mwenza wa Tundu Lissu kidogo kungekuwa na 'Ushindani' wa uhakika wa Kisiasa.

Watanzania siyo Mangumbaru na Mapopoma yaani 'Wamchague' Mtu ambaye hata Kwao tu 'hakubaliki' kivile na wala hana 'Mvuto' ule wa Kisiasa.
 
Membe alituaminisha kuwa kuna makada watano wabobezi from CCM wapo behind the scene, lakn mpak sa hv ni hollaa anafight alone agaist a well organised CCM.

Tatizo la CCM huwa wana umoja Sana linapokuja suala la uchaguz , umoja ni silaha kubwa Sana kweye masuala yyte ya kivita, hii infanya mifumo yote ya nchi inaelekezwa kuifavour CCM , kuanzia vyombo vya usalama, asasi za kiraia , matajiri wakubwa , mashirika binafs na ya uma, katika mazingira haya ni ngumu Sana kutoboa kwa mpinzan.

Kwa sasa mwamko wa upigaji kura ni kama haupo hasa maeneo ya mijini watu kama Wana harakat zao za maisha tofaut na 2015 , hii inaonyesha CCM wanashinda asubhi tuu, ...... Kama ni suala la nyomi hakuna anayeweza vunja rekodi ya Lowassa
 
kwani akipata watu kiduchu wewe inakuuma nini???

sahizi watu wanafuatilia mambo ya kampeni usiku kama huu baada ya pilika za kuusaka uchumi wa kati uliopo ktk makaratasi ya mheshimiwa, kwa hiyo kwenda kwenye hadhara sio tija na kama kweli huyo mwenye kiti wako anawatu wengi wa kumsikiliza basi afuate ushauri wa lissu wa kutopiga kampeni na utitiri wa wasanii..unatakiwa ufahamu kuwa kinachowapeleka watu pale sio kumsikiliza huyo dictator uchwara bali ni kuwaona wasanii ambao wangepaswa kutoa zaidi ya 10k kuwaona ukumbini wakitumbuiza!!
 
Lowasa alishinda, magufuli alitangazwa, Ata mwaka huu, Lissu atashinda, Magu Atatangazwa. #NiyeyE2020.
Tunachosubiri ni maamuzi ya Lissu pale ataposhinda na asitangazwe.
Msimkuze na kumpa kichwa hana ubavu huo nyie, hana la kufanya hata afanyeje na awamu hii wanamlipua kabisaa wasiojulikana,acha atambe akidhani wamemsahau ana maneno ya kilesbian sana...tunza hii comment
 
Mkuu muamko wa siasa umepungua sanaaa mkoa wa Lindi tangu CUF ife hapa, kwaiyo sio kwa Membe tu hata wengine wakija hawatopata nyomi, Lindi kwa sasa kwenye watu 10 ukiwauliza basi 6 au 7 watakuambia hawapigi kura, Mkuu Lowassa kawaumiza watu sanaaaa
 
Membe alituaminisha kuwa kuna makada watano wabobezi from CCM wapo behind the scene, lakn mpak sa hv ni hollaa anafight alone agaist a well organised CCM...

Ni 'Juha / Mpumbavu' tu pekee ndiyo atasema kuwa CCM na Rais Dkt. Magufuli 'hatoshinda' huu Uchaguzi Mkuu. CCM 'itatawala' hadi 'Kristo' akiija.
 
Daaah haya kaka acha nikuache na mtazamo wako lkn

Nadhani Somo langu hilo la 'Kiufafanuzi' limekuingia vyema kabisa na hata wale 'Visokolokwinyo' Wenzako wengine hapa nao wameliewa vile vile.
 
Hao pia Ni CCM ?Acha uduanzi basi!

Kwani wakiwa ni CCM kuna 'tatizo' lolote lile labda? Hivi kwa 'Unafiki' na 'Usaliti' ulioko huko 'Upinzani' kuna Mtanzania 'ataiacha' CCM yangu kweli?
 
Back
Top Bottom