Huo ni ufahamu wako, lakini uliyoyasema hayana uhalisia kwani mambo ya mapinduzi na muungano yapo kwenye vitabu na yanasomwa.
Mimi sipo kwenye kumlaumu mtu, nipo kwenye uhalisia wa mambo, ikiwa kudai haki ndiyo hivyo basi hakuna tofauti na mwenye kudhulumu, huwezi choma moto mali za umma au binafsi kwa kuwa unadai haki. Na ukumbuke ajenda ya NRNE ni ajenda yenye msukumo zaidi kutoka CHADEMA si ya watanzania wote, lazima watu waheshimu na fikra za watanzania wengine.
Na pia elewa hakuna mtu anayependa kufa au kuona mtu anakufa, kikubwa tuheshimu mamlaka.
1. Kipi kilianza kwanza kuchoma mali au victimization, hiyo ni consequence iliyosababishwa na watawala, huwezi kuwa na nchi inayotalawa watu wenye njaa na ikawa na amani. Hii nchi ni stable miaka yote 70 baada ya uhuru, lakini ndiyo among masikini duniani. Unemployment above 50%; hiyo ni mijini tu, huko shambani wala serikali hii haijui wananchi wanakula nini. Yule Waziri wa Foreign Affairs anaulizwa swali wamekufa wangapi anasema hata yeye hajui, yaani hii nchi watawala hawajui kazi yao, JK aliulizwa na mwandishi wa Ufaransa kwa Nini Africa haijaendelea hadi leo na Asia kote kushaendelea? Akajibu hata yeye hajui. Usiwalaumu victims, hawa ni victim wa System ya CAUSE, na unayoona hii ndiyo EFFECT, Cause and Effect; Consequences za uzembe, corruption, negligence, nepotism na kuchezea resources kwa CCM na ubinafsi. Usipojenga ufa utajenga ukuta.
2. Msianze kuleta mambo ya Chadema hapa, haya maandamno siyo ya Chadema, haya maandamano yanahusu CCM, pia na wananchi wote ambao hawakubali mambo ya CCM, Polepole ni CCM, Dr Malisa ni CCM, na ahakuna aimpact kubwa iliyofanya watu wengi wajue kuhusu wahuni kama alivyofanya Polepole, in matter of fact, NRE ni moja tu ya catalyst lakini siyo kila kitu. CCM wengi wamegushwa sana na haya maandamano ile nyie die hard hamuwezi kuelewa, kwa sababu mnanufaika. Utekaji, disapperances, uuaji na Rais anakaa kmya unafikiri wanaona ni Chadema tu? Hata wasio CCM wanaona.
3. Yule Rais wa Madagascar kweli hakupenda watu wake wafe, hata maRais wengi wa Asia au Europe hata South America hawapendi watu wao wafe kwa sababu wakiona mambo kama hivi wanapisha njia, ili kuokoa maisha ya wenzao na wananchi. Ni mijitu ya mieusi tu ya Afrika ambayo hugeuza nchi kama mali zao. Angali Haiti ingawa ipo Western sphere ndiyo hutokea yanayotokea huku kwetu, nchi peke yake Western Hemisphere, halafu Papua New Guinea- speaks a lot.