Kwa utaratibu huu, tufunge safari kumuona DG wa NSSF?

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,263
Reaction score
1,753
Mzee wangu amemaliza utumishi. Kafungua madai ya kukosa ajira NSSF Mwanza, june 01, 2026. Danadana zinazoendelea hapo, hata Pele hakuwahi zicheza. Hadi leo hajalipwa.

Majibu ya mwisho yalikuwa kuwa asubiri mfumo wa NMB, umeleta usumbufu na hata jana ameelezwa hivyo na waheshimiwa sana ambao pekee ndio wanatumia NMB ambayo wengine hawaitumii.

HAkuna ofisi hajaingia hapo NSSF Mwanza, lakini bila mafanikio. Kimbembe kipo kwenye msingi wa uzi huu,kumfikia DG.

Kuna utaratibu wa kufuata, kuwasiliana, [email protected] au [email protected]., hizi email ni kama namba za chasis. Haziendi.

Pia kuna ile namba ya 0800116773, jana ilipatikana lakini kwa zaidi ya nus saa, ulikuwa ukitolewa ujumbe wa kusubiri , mhudumu anaongea na mteja mwingine. Leo hiyo namba haipatikani kabisa.

Mkurugenzi mkuu anapaswa kufikishiwa suala kama hili ikiwa halitakuwa limepata ufumbuzi ndani ya siku 11 na kuendelea. mawasiliano yake ni, [email protected], kama kawaida hii nayo mail haziendi.

Najiuliza, tutumie njia gani kukufikia? Na au nini kifanyike ili "waheshimiwa" ninyi mtoe malipo ya mzee huyu. Naimani njia zipo.
 
Asubiri mfu

Asubiri mfumo wa NMB ili alipwe au
 
Hakuna taarifa za kueleweka kila siku kuna jiipya. Mara anayefuatilia suala hilo ana week ni mgonjwa! Kana kwamba kuna ofisi inafubgwa kwa mtu kuugua, kisha watumishi wengi wako nje ya ofisi kikazi!, mara faili limewekwa mhuri kimakosa limepelekwa uchunguzi, kabla ya kuambiwa liko kwa watu wa IT.

Kumbuka hapo, umetakiwa kufika ofisini kupata taarifa hizo. Msoto kama unaomba msaada.
 
Pale unapodai chako baada ya kustaafu, ndipo shida huanza! 😊
Lazima mvutane na watu aisee!
Hii ni mitazami ya kale, dunia inabadilika lakini kuna watu hawataki kubadilika.
Vipi wao kuwafuata waajiri na kuwapiga faini kwa kuchelewa kuwasilisha michango ya wanachama?
 
Kasheshe.
Kuna watu wako ofisi hiyo, nafikiri walipaswa kuwa katika jeshi la KAR kwani kwa zama hizi, wamepitwa na wakati.

Wiki tatu zilizopita Dada mmoja mweusi mwenye kuvaa hijabu hapo ofisi ya mapokezi, ampatie namba yake, atalishuguulikia suala hilo, hadi leo naona salio lake halitoshelezi kupiga simu.
 
Mwambie akomae mkuu Watampa sema kwa mbinde sana. Binafsi niliwahi kuwekwa pending na PSSSF miaka 2 wanakupiga danadana tu washenzi wale siku waliyoingiza mzigo wangu hata nyuma sikugeuka kuwaangalia!
Sasa hili la kusubiri kwa muda usioeleweka ndo janga. Kwaji huyo DG yuko hapo kumwakilisha nani?
 
Nilimshuhudia mzee mmoja katokea kigoma huko alikuja hapo dodoma kufwatilia hayo maswala yake baada ya mawasiliano kutoleta maelewano. Yule mzee aliongea kwa uchungu na alikuwa mgonjwa wala hakuna aliyekuwa anajali haya mambo yanasikitisha Haiwezekani Jasho Lako Uteswe nalo Kiasi kile. Washenzi wale tuliwagomea kutoka ofisini ndio poneaponea yetu Just imagine nilikuwa natoka mbeya to dodoma kulala hoteli siku kadhaa na bado hawakufanikishii jambo lako Wehu sana wale
 
Mlikuwa sahihi. Mlifunga ofisi kwa muda gani?

Nimegundua uzenbe na kutowajibikaa huku kunasababishwa na utamaduni wa kitanzania wa kukubali kila unachoambiwa. Jiulize, unaambiwa mhusika ni mgonjwa kwa wiki nzima na unakubali!. Ofisi ya wapi hiyo? Raismwenyewe akutoka kuba mtu mwingine, sembuse ofisi ya wilaya?
 
muda wa kufunga ofisi ulipofika tuligoma kutoka nakumbuka tulikuwa watano hivi. Wazee wanne Chalii nipo mimi tu. Meneja akatupa deadline kesho asubuhi asione mtu ofisini kwake kila kitu kitakuwa tayari Hapo anaongea huku amebetua mdomo kwa dharau😂😂 Hakuna aliyemwamini tukashauriana pale Tukakubaliana Kesho yake asubuhi tuwepo pale. Asubuhi nikapitia ATM kucheki kabla sijaingia huko ofisini kwao. Lahaula nikakuta Akaunti Imecheka Tayari Nikaondoka zangu hata ofisini kwao sikurudi tena
 
Mzee wangu amemaliza utumishi. Kafungua madai ya kukosa ajira NSSF Mwanza, june 01, 2026. Danadana zinazoendelea hapo, hata Pele hakuwahi zicheza. Hadi leo hajalipwa.

Majibu ya mwisho yalikuwa kuwa asubiri mfumo wa NMB, umeleta usumbufu na hata jana ameelezwa hivyo na waheshimiwa sana ambao pekee ndio wanatumia NMB ambayo wengine hawaitumii.

HAkuna ofisi hajaingia hapo NSSF Mwanza, lakini bila mafanikio. Kimbembe kipo kwenye msingi wa uzi huu,kumfikia DG.

Kuna utaratibu wa kufuata, kuwasiliana, [email protected] au [email protected]., hizi email ni kama namba za chasis. Haziendi.

Pia kuna ile namba ya 0800116773, jana ilipatikana lakini kwa zaidi ya nus saa, ulikuwa ukitolewa ujumbe wa kusubiri , mhudumu anaongea na mteja mwingine. Leo hiyo namba haipatikani kabisa.

Mkurugenzi mkuu anapaswa kufikishiwa suala kama hili ikiwa halitakuwa limepata ufumbuzi ndani ya siku 11 na kuendelea. mawasiliano yake ni, [email protected], kama kawaida hii nayo mail haziendi.

Najiuliza, tutumie njia gani kukufikia? Na au nini kifanyike ili "waheshimiwa" ninyi mtoe malipo ya mzee huyu. Naimani njia zipo.
Hayo masuala huwa yanatakiwa kuanza kwa kujaza taarifa na nyaraka atakazopewa kimiongozo na kufuatiliwa kwa karibu miezi hata sita kabla mstaafu mtarajiwa hajaondoka rasmi kwenye UTUMISHI wake.Msikate tamaa.Fuatilieni kwa karibu na inshallah mtafanikiwa.
 
muda wa kufunga ofisi ulipofika tuligoma kutoka nakumbuka tulikuwa watano hivi. Wazee wanne Chalii nipo mimi tu. Meneja akatupa deadline kesho asubuhi asione mtu ofisini kwake kila kitu kitakuwa tayari Hapo anaongea huku amebetua mdomo kwa dharau😂😂 Hakuna aliyemwamini tukashauriana pale Tukakubaliana Kesho yake asubuhi tuwepo pale. Asubuhi nikapitia ATM kucheki kabla sijaingia huko ofisini kwao. Lahaula nikakuta Akaunti Imecheka Tayari Nikaondoka zangu hata ofisini kwao sikurudi tena
Ungerudi uone kama bado kabetua midomo yake umfanyie hata sala ya toba.
 
Back
Top Bottom