Kwa utaratibu huu, tufunge safari kumuona DG wa NSSF?

Kwa utaratibu huu, tufunge safari kumuona DG wa NSSF?

NSSF walitoa taarifa wako kwenye marekebisho ya mfumo ijumaa last week.

Hata mimi nilienda kufungua madai, jumatatu wiki hii nikawa nazungushwa zungushwa mara nenda department fulani mara rudi kule. Nikakutana na staff mmoja nikamwambia anielekeze nielekee wapi kwa shida yangu maana nimechoka kuzungushwa.

Yule ndio akanichana live akaniambia mfumo unazingua bado unarekebishwa, ila wanaogopa tu kukwambia ukweli.

Nahisi ndio sababu
 
Hayo masuala huwa yanatakiwa kuanza kwa kujaza taarifa na nyaraka atakazopewa kimiongozo na kufuatiliwa kwa karibu miezi hata sita kabla mstaafu mtarajiwa hajaondoka rasmi kwenye UTUMISHI wake.Msikate tamaa.Fuatilieni kwa karibu na inshallah mtafanikiwa.
Mkuu
Hilo nalo tatizo, hizo nyaraka zote zikuwepo kwa ukamilifu hadi wakatoa huo muda wa mwezi mmoja wa kulipwa, lakini imekuwa ndivyo sivyo.

Suala la uvumilivu hili linaweza kikaeleweka kama kuna sababu za msingi, sio za faili lilipelekwa kimakosa IT wiki nzima na halishughulikiwi, au kwamba mhusika ni mgonjwa.

Kwani, kupatikana kwa mawasiliano ya DG kwa urahisi kuna shida gani? Na hizo namba za hudumamkwa wateja zinawahusu kina nani?
 
Mkuu
Hilo nalo tatizo, hizo nyaraka zote zikuwepo kwa ukamilifu hadi wakatoa huo muda wa mwezi mmoja wa kulipwa, lakini imekuwa ndivyo sivyo.

Suala la uvumilivu hili linaweza kikaeleweka kama kuna sababu za msingi, sio za faili lilipelekwa kimakosa IT wiki nzima na halishughulikiwi, au kwamba mhusika ni mgonjwa.

Kwani, kupatikana kwa mawasiliano ya DG kwa urahisi kuna shida gani? Na hizo namba za hudumamkwa wateja zinawahusu kina nani?
Kuna mambo huwa yanatengenezwa ili mkate wa mstaafu umegwe.Kuwa makini.
 
NSSF walitoa taarifa wako kwenye marekebisho ya mfumo ijumaa last week.

Hata mimi nilienda kufungua madai, jumatatu wiki hii nikawa nazungushwa zungushwa mara nenda department fulani mara rudi kule. Nikakutana na staff mmoja nikamwambia anielekeze nielekee wapi kwa shida yangu maana nimechoka kuzungushwa.

Yule ndio akanichana live akaniambia mfumo unazingua bado unarekebishwa, ila wanaogopa tu kukwambia ukweli.

Nahisi ndio sababu
Maskini nchi nchi yangu na wwsomi wake. Wanakuachabunataabika badalanya kukwambia ukweli.

Ujinga mwingine huwa wanajifiicha kwenye mfumo umeharibika/ uko down... utafikiri hiyo ni sayansi ya kupasua kichwa, kwamba wewe huwezi kujua, kana kwamba shule walizosoma zilivunjwa baada ya wao kuhitimu.
 
muda wa kufunga ofisi ulipofika tuligoma kutoka nakumbuka tulikuwa watano hivi. Wazee wanne Chalii nipo mimi tu. Meneja akatupa deadline kesho asubuhi asione mtu ofisini kwake kila kitu kitakuwa tayari Hapo anaongea huku amebetua mdomo kwa dharau😂😂 Hakuna aliyemwamini tukashauriana pale Tukakubaliana Kesho yake asubuhi tuwepo pale. Asubuhi nikapitia ATM kucheki kabla sijaingia huko ofisini kwao. Lahaula nikakuta Akaunti Imecheka Tayari Nikaondoka zangu hata ofisini kwao sikurudi tena
Hukurudi hata kutoa asante
 
Mzee wangu amemaliza utumishi. Kafungua madai ya kukosa ajira NSSF Mwanza, june 01, 2026. Danadana zinazoendelea hapo, hata Pele hakuwahi zicheza. Hadi leo hajalipwa.

Majibu ya mwisho yalikuwa kuwa asubiri mfumo wa NMB, umeleta usumbufu na hata jana ameelezwa hivyo na waheshimiwa sana ambao pekee ndio wanatumia NMB ambayo wengine hawaitumii.

HAkuna ofisi hajaingia hapo NSSF Mwanza, lakini bila mafanikio. Kimbembe kipo kwenye msingi wa uzi huu,kumfikia DG.

Kuna utaratibu wa kufuata, kuwasiliana, [email protected] au [email protected]., hizi email ni kama namba za chasis. Haziendi.

Pia kuna ile namba ya 0800116773, jana ilipatikana lakini kwa zaidi ya nus saa, ulikuwa ukitolewa ujumbe wa kusubiri , mhudumu anaongea na mteja mwingine. Leo hiyo namba haipatikani kabisa.

Mkurugenzi mkuu anapaswa kufikishiwa suala kama hili ikiwa halitakuwa limepata ufumbuzi ndani ya siku 11 na kuendelea. mawasiliano yake ni, [email protected], kama kawaida hii nayo mail haziendi.

Najiuliza, tutumie njia gani kukufikia? Na au nini kifanyike ili "waheshimiwa" ninyi mtoe malipo ya mzee huyu. Naimani njia zipo.
Jitieni uchizi na mzee wako.
Kivipi?
Jipangeni, kama inawezekana kesho au Jumanne, muende tena hizo ofisi za NSSF. Mkifika hapo kama kawaida mzee afuatilie, wakitoa majibu yasiyoeleweka tena au kuleta dharau, mzee awaambie nimekuja hapa na kijana wangu, hatutoki hapa ofisini hadi tupate suluhu ya hili suala langu. Tieni presha hapo na muwe tayari kugoma kutoka hapo wakati wanafunga ofisi, hata wakiwaitia security na/au polisi, muwe tayari kwa lolote hata kulala lock up. Mkitia hiyo amsha amsha hapo, nawaahidi kuwa ndani ya masaa 48 (siku 2), mafao ya mzee yatasoma kwenye akaunti yake. Wewe kama kijana shababi inabidi umsapoti sana mzee wako kwenye hii amsha amsha, la sivyo hatapata hayo mafao.
Nakuambia hivi kwa uzoefu, mzee wangu alipigwa mizungusho mwaka mzima, siku hiyo nikawa nipo likizo nikaenda kumcheki, akawa analalamika kuwa mafao yake bado. Nikamwambia mzee nikupe mbinu utakua tayari? Akaniambia nakusikiliza mwanangu. Nikampa mchongo mzima. Akasema mimi niko tayari mwanajeshi wangu. Asubuhi yake tukashindilia chai nzito na kiporo matumbo yakajaa vizuri, mzee hata hakumwambia bi mkubwa kuhusu hii plan ya kimafia, tulipiga kimya kimya. Tukabeba na maji makubwa. Tukatimba NSSF ofisi ya Iringa pale. Kaenda kuulizia, wakamzungusha pale na majibu yasiyoeleweka, wanamwambia arudi baada ya wiki tatu. Akawaambia sasa jamani nimekuja hapa nipo na mwanangu, humu ndani leo hatutoki mkifunga ofisi mtatuacha humu, hadi tupate suluhisho la hili suala. Nikaenda pale dirishani alipokua, kwanza tukazuia yule staff aliekua anamu attend pale asihudumie mtu mwingine lisaa lizima, baadae tukasogea pembeni pale tukasema hatutoki leo humu, kaa pale muda wa kufunga watu wote wameisha tukasema tuambieni suala hili linaisha lini? Wakatutishia polisi, tukawaambia waiteni tu..... Meneja akaja pale anauliza shida nini? Akaelezewa pale, anawauliza wenzake why hadi leo hajalipwa mzee? Hakuna majibu ya kueleweka. Yule meneja akatusihi sana, akasema anaomba hilo suala alifuatilie mwenyewe, na kwamba ndani ya siku 2 mzee atapata mafao labda kuwe na ishu kubwa sana. Baada ya kutusihi sana na kuahidi, tukasepa kwa hiyo ahadi kuwa ndani ya siku 2 mzigo utasoma, na tukamwambia meneja mzigo usiposoma, siku ya tatu tutakuja tena na tutalala hapo ofisini. Tukasepa, hapo tayari kumi na mbili jioni.
Kesho yake tu jioni mida ya saa 10 jioni, muamala ukasoma.
Mzee alifurahi sana, akaniambia kweli wewe jembe mwanangu.
johnmashilatu
 
Back
Top Bottom