Kwa utaratibu huu, tufunge safari kumuona DG wa NSSF?

NSSF walitoa taarifa wako kwenye marekebisho ya mfumo ijumaa last week.

Hata mimi nilienda kufungua madai, jumatatu wiki hii nikawa nazungushwa zungushwa mara nenda department fulani mara rudi kule. Nikakutana na staff mmoja nikamwambia anielekeze nielekee wapi kwa shida yangu maana nimechoka kuzungushwa.

Yule ndio akanichana live akaniambia mfumo unazingua bado unarekebishwa, ila wanaogopa tu kukwambia ukweli.

Nahisi ndio sababu
 
Mkuu
Hilo nalo tatizo, hizo nyaraka zote zikuwepo kwa ukamilifu hadi wakatoa huo muda wa mwezi mmoja wa kulipwa, lakini imekuwa ndivyo sivyo.

Suala la uvumilivu hili linaweza kikaeleweka kama kuna sababu za msingi, sio za faili lilipelekwa kimakosa IT wiki nzima na halishughulikiwi, au kwamba mhusika ni mgonjwa.

Kwani, kupatikana kwa mawasiliano ya DG kwa urahisi kuna shida gani? Na hizo namba za hudumamkwa wateja zinawahusu kina nani?
 
Kuna mambo huwa yanatengenezwa ili mkate wa mstaafu umegwe.Kuwa makini.
 
Maskini nchi nchi yangu na wwsomi wake. Wanakuachabunataabika badalanya kukwambia ukweli.

Ujinga mwingine huwa wanajifiicha kwenye mfumo umeharibika/ uko down... utafikiri hiyo ni sayansi ya kupasua kichwa, kwamba wewe huwezi kujua, kana kwamba shule walizosoma zilivunjwa baada ya wao kuhitimu.
 
Hukurudi hata kutoa asante
 
Jitieni uchizi na mzee wako.
Kivipi?
Jipangeni, kama inawezekana kesho au Jumanne, muende tena hizo ofisi za NSSF. Mkifika hapo kama kawaida mzee afuatilie, wakitoa majibu yasiyoeleweka tena au kuleta dharau, mzee awaambie nimekuja hapa na kijana wangu, hatutoki hapa ofisini hadi tupate suluhu ya hili suala langu. Tieni presha hapo na muwe tayari kugoma kutoka hapo wakati wanafunga ofisi, hata wakiwaitia security na/au polisi, muwe tayari kwa lolote hata kulala lock up. Mkitia hiyo amsha amsha hapo, nawaahidi kuwa ndani ya masaa 48 (siku 2), mafao ya mzee yatasoma kwenye akaunti yake. Wewe kama kijana shababi inabidi umsapoti sana mzee wako kwenye hii amsha amsha, la sivyo hatapata hayo mafao.
Nakuambia hivi kwa uzoefu, mzee wangu alipigwa mizungusho mwaka mzima, siku hiyo nikawa nipo likizo nikaenda kumcheki, akawa analalamika kuwa mafao yake bado. Nikamwambia mzee nikupe mbinu utakua tayari? Akaniambia nakusikiliza mwanangu. Nikampa mchongo mzima. Akasema mimi niko tayari mwanajeshi wangu. Asubuhi yake tukashindilia chai nzito na kiporo matumbo yakajaa vizuri, mzee hata hakumwambia bi mkubwa kuhusu hii plan ya kimafia, tulipiga kimya kimya. Tukabeba na maji makubwa. Tukatimba NSSF ofisi ya Iringa pale. Kaenda kuulizia, wakamzungusha pale na majibu yasiyoeleweka, wanamwambia arudi baada ya wiki tatu. Akawaambia sasa jamani nimekuja hapa nipo na mwanangu, humu ndani leo hatutoki mkifunga ofisi mtatuacha humu, hadi tupate suluhisho la hili suala. Nikaenda pale dirishani alipokua, kwanza tukazuia yule staff aliekua anamu attend pale asihudumie mtu mwingine lisaa lizima, baadae tukasogea pembeni pale tukasema hatutoki leo humu, kaa pale muda wa kufunga watu wote wameisha tukasema tuambieni suala hili linaisha lini? Wakatutishia polisi, tukawaambia waiteni tu..... Meneja akaja pale anauliza shida nini? Akaelezewa pale, anawauliza wenzake why hadi leo hajalipwa mzee? Hakuna majibu ya kueleweka. Yule meneja akatusihi sana, akasema anaomba hilo suala alifuatilie mwenyewe, na kwamba ndani ya siku 2 mzee atapata mafao labda kuwe na ishu kubwa sana. Baada ya kutusihi sana na kuahidi, tukasepa kwa hiyo ahadi kuwa ndani ya siku 2 mzigo utasoma, na tukamwambia meneja mzigo usiposoma, siku ya tatu tutakuja tena na tutalala hapo ofisini. Tukasepa, hapo tayari kumi na mbili jioni.
Kesho yake tu jioni mida ya saa 10 jioni, muamala ukasoma.
Mzee alifurahi sana, akaniambia kweli wewe jembe mwanangu.
johnmashilatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…