Samia kasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja ataendeleza alipoishia mwendazake.... ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu.
Huyu hata ukimsamehe, kuna vitu amefanya mwaka 2016-20 lakini madhara yake tutayaona hata baada ya 2035 Mungu akitupa uzima.Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.
Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.
Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.
Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.
Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.
Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.
Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Yes very true indeedMagufuli alikuwa anatia huruma Tu hata alipokuwa Rais.
Alikuwa kama 'mwanaharakati' na sio president.
Wengi tulijua atashindwa na hata mazuri yake yanaweza sahauliwa, ndo kinachatokea.
Daah hii ni hatariFikiria namna bora ya kuwaomba msamaha hawa:
1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports Kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na niaovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara
Haya maneno yako machache hayatoshi kabisa.Hawa wanataka maridhiano na ukweli na kuhakishiwa hayatajirudia tena.
Una uhuru wa mawazo kadri ya Katiba. Lakini ukipata muda pita Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akiliKwani ametukosea nini sisi Watanzania? Kwa level ya Taifa sioni kosa lake labda kwa level ya mtu binafsi. Kama ni hivyo, basi ni jukumu la familia yake. But sisi kama Wananchi, we are proud of him and we would had wished him to live longer.
R.I.P JPM
Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
mwananchit Kama hujui maovu ya Magufuli na uko Tanzania inawezekana unaumwa magonjwa ya akili. Wahi Muhimbili au MirembeHivi unamuombea msamaha kwa mapungufu yapi kwa mfano? Ungetaja mapungufu unayoyajua angalau mawili matatu halafu uysombee msamaha. Hii itafungua mlango kwa wengine kumuombea msamaha pia kwa yale watakayoyakumbuka na kuyataja. Naomba tusiongelee msamaha wa jimla jumla wa makosa ambayo hayajaorodheshwa. Let's be more specific. Hayo ndiyo mawazo yangu
Nani alishangalia we fedhuli na baladhuli? Hamkuona walilkuwa wanalia na kugaagaa mabarabarani?Marehemu asemwi vibaya ila jiwe alipokufa watu mioyo yao ilishangilia.
Kufa wote tutakufa ila insue nani anatangulia?
Jiwe kanitesa binafsi ila nishamsamehe muda sana.
Tuseme Amina!!! wengine tuseme Inshaallah!!
Maovu gani wewe ni mtu wa chuki.mwananchit Kama hujui maovu ya Magufuli na uko Tanzania inawezekana inaumwa magonjwa ya akili. Wahi Muhimbili au Mirembe
Upo nje ya mada.Ni nani ambaye alipotoka madarakani alisifiwa kuanzia Nyerere, mwinyi, mkapa hadi Jiwe? Watanzania ni wanafiki wanasoma upepo, wanajua vyeo vinapatikanaje, SIFIA ALIEPO TUKANA ALIEPITA... Siri kuu ya wabongo kupata shekeli
Kuna mtu alitukanwa Kama Nyerere, kila Lori jipya walisema ni la Siti Mwinyi, kila uwekezaje wanasema Mkapa ana 10%, kila sheli mpya ni ya Rizimoko. Tumewazoea!!!!
Ni nani ambaye alipotoka madarakani alisifiwa kuanzia Nyerere, mwinyi, mkapa hadi Jiwe? Watanzania ni wanafiki wanasoma upepo, wanajua vyeo vinapatikanaje, SIFIA ALIEPO TUKANA ALIEPITA... Siri kuu ya wabongo kupata shekeli
Kuna mtu alitukanwa Kama Nyerere, kila Lori jipya walisema ni la Siti Mwinyi, kila uwekezaje wanasema Mkapa ana 10%, kila sheli mpya ni ya Rizimoko. Tumewazoea!!!!
Au sio unajukita umekua Mungu sasa..unajua aliongea nn na Mungu wakeFinnaarrr !!...wa JEHANAMU ..!! hakuna msamaa bila chama chake kuleta katiba mpya.
aliandikiwa motoni mwache akateketee na maccm yote yatawaka mpaka ...
Damu yake iwasamehe kina nani ssa😂😂😂Mimi Sijakamilika sina alichonikosea na nyie mnaomshambulia Mzee ombeni radhi mkiwa hai hakuna mkamilifu chini ya jua ...wengine hata wakizikwa kaburi zao hazitaota majani kinakuwa kijangwa kidogo kwa uovu waliofanya ila kwa kunyoosha vidole hamjambo...Pumzika Mzee wangu damu yako iwasamehe hawa ndio uanadamu...haishangazi..
Huko ndio kuishi kama mashetani au kubatizwa kwa moto😄Mwendazake safari yetu ya maisha aliifanya kuwa ni ya taabu Sana na mateso Tena KWA kipindi kifupi,alipotufikisha kimasafa palikuwa ni mbali ikatuchosha kufikiria kurudi,na tulivyovipoteza ni vingi hatuwez kuvihesabu,bora tuhesabu tulivyovibakiza
kwamba mzuri yake yamesahauliwa[emoji23][emoji23]Magufuli alikuwa anatia huruma Tu hata alipokuwa Rais.
Alikuwa kama 'mwanaharakati' na sio president.
Wengi tulijua atashindwa na hata mazuri yake yanaweza sahauliwa, ndo kinachatokea.