Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

... ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu.
Samia kasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja ataendeleza alipoishia mwendazake.
 
Marehemu dikiteta magufuli kama mtz mwenzetu tushamsamehe, lkn maovu yake hatutaacha kuyasema make tunayatumia kama case study kuelimisha jamii ili huko mbeleni asije kutokea rais mwovu kama marehemu dikiteta magufuli.
 
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Huyu hata ukimsamehe, kuna vitu amefanya mwaka 2016-20 lakini madhara yake tutayaona hata baada ya 2035 Mungu akitupa uzima.

Naogopa Rais atakayekuwapo 2035 atalaumiwa kwa PERFORMANCE wakati ni uozo uliosababishwa na Mwendazake.

Hatumpumzishi huyu, spanna mpaka ahera
 
Finnaarrr !!...wa JEHANAMU ..!! hakuna msamaa bila chama chake kuleta katiba mpya.
aliandikiwa motoni mwache akateketee na maccm yote yatawaka mpaka ...
 
Fikiria namna bora ya kuwaomba msamaha hawa:

1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports Kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na niaovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara

Haya maneno yako machache hayatoshi kabisa.Hawa wanataka maridhiano na ukweli na kuhakishiwa hayatajirudia tena.
Daah hii ni hatari
 
Kwani ametukosea nini sisi Watanzania? Kwa level ya Taifa sioni kosa lake labda kwa level ya mtu binafsi. Kama ni hivyo, basi ni jukumu la familia yake. But sisi kama Wananchi, we are proud of him and we would had wished him to live longer.

R.I.P JPM

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Una uhuru wa mawazo kadri ya Katiba. Lakini ukipata muda pita Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili
 
Hivi unamuombea msamaha kwa mapungufu yapi kwa mfano? Ungetaja mapungufu unayoyajua angalau mawili matatu halafu uysombee msamaha. Hii itafungua mlango kwa wengine kumuombea msamaha pia kwa yale watakayoyakumbuka na kuyataja. Naomba tusiongelee msamaha wa jimla jumla wa makosa ambayo hayajaorodheshwa. Let's be more specific. Hayo ndiyo mawazo yangu
mwananchit Kama hujui maovu ya Magufuli na uko Tanzania inawezekana unaumwa magonjwa ya akili. Wahi Muhimbili au Mirembe
 
Ni nani ambaye alipotoka madarakani alisifiwa kuanzia Nyerere, mwinyi, mkapa hadi Jiwe? Watanzania ni wanafiki wanasoma upepo, wanajua vyeo vinapatikanaje, SIFIA ALIEPO TUKANA ALIEPITA... Siri kuu ya wabongo kupata shekeli

Kuna mtu alitukanwa Kama Nyerere, kila Lori jipya walisema ni la Siti Mwinyi, kila uwekezaje wanasema Mkapa ana 10%, kila sheli mpya ni ya Rizimoko. Tumewazoea!!!!
 
Marehemu asemwi vibaya ila jiwe alipokufa watu mioyo yao ilishangilia.

Kufa wote tutakufa ila insue nani anatangulia?

Jiwe kanitesa binafsi ila nishamsamehe muda sana.

Tuseme Amina!!! wengine tuseme Inshaallah!!
Nani alishangalia we fedhuli na baladhuli? Hamkuona walilkuwa wanalia na kugaagaa mabarabarani?
 
Ni nani ambaye alipotoka madarakani alisifiwa kuanzia Nyerere, mwinyi, mkapa hadi Jiwe? Watanzania ni wanafiki wanasoma upepo, wanajua vyeo vinapatikanaje, SIFIA ALIEPO TUKANA ALIEPITA... Siri kuu ya wabongo kupata shekeli

Kuna mtu alitukanwa Kama Nyerere, kila Lori jipya walisema ni la Siti Mwinyi, kila uwekezaje wanasema Mkapa ana 10%, kila sheli mpya ni ya Rizimoko. Tumewazoea!!!!
Upo nje ya mada.
 
Magufuli alikuwa anatia huruma Tu hata alipokuwa Rais.

Alikuwa kama 'mwanaharakati' na sio president.

Wengi tulijua atashindwa na hata mazuri yake yanaweza sahauliwa, ndo kinachatokea.
kweli mkuu alitia huruma Sana.
 
Ongeza na Hitler pamoja na Iddi Amin
Ni nani ambaye alipotoka madarakani alisifiwa kuanzia Nyerere, mwinyi, mkapa hadi Jiwe? Watanzania ni wanafiki wanasoma upepo, wanajua vyeo vinapatikanaje, SIFIA ALIEPO TUKANA ALIEPITA... Siri kuu ya wabongo kupata shekeli

Kuna mtu alitukanwa Kama Nyerere, kila Lori jipya walisema ni la Siti Mwinyi, kila uwekezaje wanasema Mkapa ana 10%, kila sheli mpya ni ya Rizimoko. Tumewazoea!!!!
 
Finnaarrr !!...wa JEHANAMU ..!! hakuna msamaa bila chama chake kuleta katiba mpya.
aliandikiwa motoni mwache akateketee na maccm yote yatawaka mpaka ...
Au sio unajukita umekua Mungu sasa..unajua aliongea nn na Mungu wake
 
Mimi Sijakamilika sina alichonikosea na nyie mnaomshambulia Mzee ombeni radhi mkiwa hai hakuna mkamilifu chini ya jua ...wengine hata wakizikwa kaburi zao hazitaota majani kinakuwa kijangwa kidogo kwa uovu waliofanya ila kwa kunyoosha vidole hamjambo...Pumzika Mzee wangu damu yako iwasamehe hawa ndio uanadamu...haishangazi..
Damu yake iwasamehe kina nani ssa😂😂😂
 
Mwendazake safari yetu ya maisha aliifanya kuwa ni ya taabu Sana na mateso Tena KWA kipindi kifupi,alipotufikisha kimasafa palikuwa ni mbali ikatuchosha kufikiria kurudi,na tulivyovipoteza ni vingi hatuwez kuvihesabu,bora tuhesabu tulivyovibakiza
Huko ndio kuishi kama mashetani au kubatizwa kwa moto😄
 
Mjadala mpana wa kitaifa unahitajika na kama alivyosema mwenyewe mwendazake hayati John Pombe Joseph Magufuli kuwa historia ya kweli ifundishwe mashuleni.

Basi ktk kumuenzi mwendazake hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli aliyetambulika kupitia propaganda za diaspora ya kiafrika kuwa ni shujaa wa afrika , somo hili la historia tusomeshwe pia ya yaliyofanyika chini ya utawala wa Magufuli na chama chake cha CCM Mpya siyo kwa ajili ya kulipa kisasi bali kutuwezesha kama jamii na wale waliopewa dhamana kama viongozi kutenda mema ili historia isije kutuhukumu siku za usoni.

Kule kwa dikteta Francisco Franco walifikia kwenda kulivamia kanisa wafukue kaburi la mwendazake Francisco Franco .

N.B
Habari zaidi za historia za tawala za mkono wa chuma kandamizi :
24 Apr 2018
Madrid, Spain

Mihimili ya Bunge na Mahakama za afiki kuweka historia sahihi ya dikteta Jenerali Franco wa Uhispania

Diktekta Jenerali Francisco Franco alitawala taifa hilo la Hispania kwa staili ya utawala wa 'mkono wa chuma' kwa muda wa miaka 39 hadi alipofariki dunia kwa afya dhoofu mwaka 1975.

Katika kipindi chake cha utawala wa Jenerali Franco, watu wengi walipotea ktk mazingira ya utatanishi na wengineo maelfu kufungwa jela kutokana na kuwa na itikadi tofauti za kisiasa zilizokwaza utawala wake.

Diktekta Franco alikuwa na mahusiano ya karibu viongozi wa juu wa kanisa, maana kanisa lilikuwa na ushawishi ktk maisha ya raia na pia kuunga mkono utawala wa kifalme ktk Hispania.

Jenerali Franco katika vita (1936-1939) vya wenyewe kwa wenyewe Hispania iliyoisha mwaka 1939 hakutaka kuona nchi hiyo ikiishia kumeguka ktk majimbo ya Catalonia n.k Hivyo alitumia majeshi kuhakikisha nchi inabakia bila mgawanyiko. Ushindi wa majeshi ya Franco, ulishangiliwa na kubatizwa kuwa ni ushindi dhidi ya wapiganaji wasio na imani ktk uwepo wa Mungu, Ufalme , uzalendo na umoja wa taifa.

Vita hivyo vilisababisha maelfu ya vifo na Diktekta Franco kuja na wazo la Kujenga basilica / makumbusho maalum ktk mfano wa kanisa kuwaenzi waliopoteza maisha ktk vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.

Katika wosia wake Dikteta Franco, aliomba kuzikwa ktk basilica hilo na wahanga wengine wa vita ili kujibainisha na wafu wengine waliopigania au kufa kutetea taifa hilo la Hispania lisigawanyike.

Hata hivyo miaka 43 baadaye toka kifo cha diktekta huyo, wananchi, mwanaharakati wa haki za binadamu na wanasiasa wameona kuwa ukatili uliofanyika na utawala wake haustahili kusahauliwa.

Hivyo kupitia Bunge na Mahakama wameona kuweka historia sahihi kuwa ktk utawala wa Franco kuna unyama na ukatili mwingi ulitendeka ktk utawala wake uliodumu miaka 39.

Kuhitimisha hilo, hoja ya kufukuliwa mwili wake imepitishwa Bungeni na kutiliwa uzito mahakamani kisheria kuwa Diktekta huyo hastahili kulala ktk makumbusho hayo kutokana na vitendo viovu vilivyofanyika ktk utawala wake wa kiimla.



Spanish court has for the first time authorised the exhumation of bodies from the Valley of the Fallen. It is a vast mausoleum where the fascist dictator General Franco is buried with thousands of victims of Spain’s 1936 civil war.
 
Marehemu JPM Apumzike kwa Amani.. Nilioata Maisha Katika Awamu yake.
 
Magufuli alikuwa anatia huruma Tu hata alipokuwa Rais.

Alikuwa kama 'mwanaharakati' na sio president.

Wengi tulijua atashindwa na hata mazuri yake yanaweza sahauliwa, ndo kinachatokea.
kwamba mzuri yake yamesahauliwa[emoji23][emoji23]

na nani huyo au nyinyi ambao hamyajui kabisa.
 
Back
Top Bottom