Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Mkuu, wanasema swali kabla hujaswaliwa. Huyu mwache apambane na mabaya yake maana yamezidi mzani wa mazuri. Alijiona yeye ni jiwe akajiita Hadi malaika na wengine wakadiriki kumuita Mungu. Sasa akapambane na Mungu mwenzie ndio atajua yupi ni Mungu wa kweli.

Nachosema ni heri Mungu akuchukie na ukiomba msamaha atakusamehe Ila sio mimi mwanadamu niliyezaliwa na mwanamke mwenye damu na nyama. NEVER
 
Haya ndio makosa ya kiufundi... endeleeni kuchochea moto...
 
Kwani yeye mwenyewe anasemaje juu ya msamaha?
Sidhani kama huu Upuuzi wenu wa hii Kauli inafaa katika Uzi huu sana sana unaweza kujikuta Unadharaulika tu.

Unaposema ( tena Kuhoji ) kuwa kwani Yeye anasemaje wakati unajua kuwa hatunae tena duniani ( amefariki ) unakuwa unamaanisha nini labda kwa Great Thinkers hapa?

Huwa mnanilazimisha niwajibuni hovyo.
 
wewe mtu huwa ni mwungana sana, ubarikiwe...
Asante Mkuu. Kuna Watu hapa JF wanadhani kuwa labda ni Wao tu pekee ndiyo walioumizwa, ila kuna Wengine wangeyasema yao huenda wangejiona wana afadhali.

Taifa haliwezi kuwa na Harmony kama Wananchi wake 24/7 Wana Visununu ( Vinyongo ) Mioyoni mwao lakini nyote mkijitambua ni Wanadamu na hatujakamilika basi Kusameheana na kuombeana Rehema ni Jambo la Kheri mno.

Bado nawaombeni kuwa tumsameheni.
 
Pole sana mkuu,,yule kiumbe hakuna ambae hajapitia madhila yake, nahisi yule hakuwa binadamu
Hasa wapiga ma deal aliwabana sana! Hadi Ndama Mutoto ya Ngombe na genge lake nao walibanwa na bwana yule Mwenda zake!!
 
Mwendazake safari yetu ya maisha aliifanya kuwa ni ya taabu Sana na mateso Tena KWA kipindi kifupi,alipotufikisha kimasafa palikuwa ni mbali ikatuchosha kufikiria kurudi,na tulivyovipoteza ni vingi hatuwez kuvihesabu,bora tuhesabu tulivyovibakiza
Tatizo mnapenda sana kuendesha Maisha yenu kupitia shot cut! Ndiyo maana mnamchukia sana Mwenda zake!!
 
Siku hizi Vitoto vingi humu,baada ya kua Tanzania ndiyo Nchi pekee bando ziko chini sana kwa bei!!
 
Mie binafsi sitaki na sina mpango wa kumsamehe mungu na malaika a.k.a jiwe. Alijiona yeye ataishi milele akataka na kubadili Katiba ili atawale milele so apambane na mzigo wake wa dhambi alizozitenda hapa duniani.
Jamani mnamsingizia Baba Watu,alisema kabisa hataki kuendelea baada ya kumaliza muda wake,ni wale wanafiki tu walikua wanajaribu kujipendekeza kwake kumbe wenyewe ni mahasidi wake na tunawaona Sasa ndimi zao zilivyo badilika ghafla!! Na nakumbuka ujumbe uliletwa kwenye media Polepole!!
 
We unadhani alikuwa hataki kweli? Wakati sukumagang walishaandaa move ya kupeleka muswada bungeni wa kubadili Katiba? Can't you see walivyochanganyikiwa baada ya kufa?

Wao Wana maslahi yao na jamaa sababu ya ukabila walijihakikishia as long atakaa pale juu, then they will be safe. Kuna uhuni mwingi sana ulikuwa unaendelea Mwenyezi Mungu ametuepusha nahisi hata ingeleta machafuko kwenye history ya nchi hii.

Hauoni tafrani iliyojitokeza baada ya Kayafa kufa mpaka ukaona CDF akaamua kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mama anachukua Ile nafasi???

Haya kuna balaa huko kwenye chama maana walitaka nafasi zao mama akawatosa naona wanataka kuleta figisu kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti ndio maana ukaona mzee JK akatoa statement ya kusema hatarajii kuona kiti cha urais kinatenganishwa na uwenyekiti wa chama.

Ofcoz JK huwa anatumia soft language Ila angekuwa Kayafa ungesikia Hadi matusi.

So kwakweli aendelee tu na umalaika wake huko aliko na umungu wake. Katuachia mbegu mbaya sana.
 
Nakuhakikishia wanaombeza magufuli na kufurahia kifo chake ni wachache saaana (wengi wapo humu mitandaoni) kuliko walioumizwa. Msamaha wako hauna maana, kwasababu unawaomba watu wapumbavu waliojawa na chuki.
 
Umeongea kweli kabisa. Wanahasira za kunyooshwa vilivyo. Mazoea ni mabaya sana.
 
Unampiga spana mtu ambae hakusikii wala hayupo kwenye ulimwengu. Hujioni kama ni mpumbavu.
 
Unampiga spana mtu ambae hakusikii wala hayupo kwenye ulimwengu. Hujioni kama ni mpumbavu.
Vipi mbona kama umepaniki sana kila unachotuma lazima uite watu wapumbavu, kwani marehemu amekuachia ujauzito??

Relax get used to it, kuna mabaya na mazuri, sasa kama wewe uliona mazuri tupu just take it easy, katafute urithi maisha yaendelee.

To some of us he was just another hooligan, it's a bitter sweet you can swallow it or spit it out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…