Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Mkuu, wanasema swali kabla hujaswaliwa. Huyu mwache apambane na mabaya yake maana yamezidi mzani wa mazuri. Alijiona yeye ni jiwe akajiita Hadi malaika na wengine wakadiriki kumuita Mungu. Sasa akapambane na Mungu mwenzie ndio atajua yupi ni Mungu wa kweli.

Nachosema ni heri Mungu akuchukie na ukiomba msamaha atakusamehe Ila sio mimi mwanadamu niliyezaliwa na mwanamke mwenye damu na nyama. NEVER
 
Kama ulikuwa haujamsamehe ni shida yako tuu. Tangu day one mpaka 21, watanzania tulimlilia kwa kujipiga vifuani kwa kumuomba mwenyezi mungu amasamehe yale yote ambayo alitenda kwa bahati mbaya au makusudi ila kwa lengo la kuinyosha nchi. Kati ya watanzania mil60 na hao wa vijiweni kwako wasiozidi watu50 haina athari hata kwa mwenyezi mungu. Mwenyezi mungu mwenyewe ni Baba wa Vita ana wapigania watu wake, na hata aliruhusu watu wauwawe kwa sababu ya kukiuka matakwa yeke. So, HAYATI JEMEDARI JPM pumzika kwa amani, watz tutazidi kukuombea hadi mwisho wa dahali.
Haya ndio makosa ya kiufundi... endeleeni kuchochea moto...
 
Kwani yeye mwenyewe anasemaje juu ya msamaha?
Sidhani kama huu Upuuzi wenu wa hii Kauli inafaa katika Uzi huu sana sana unaweza kujikuta Unadharaulika tu.

Unaposema ( tena Kuhoji ) kuwa kwani Yeye anasemaje wakati unajua kuwa hatunae tena duniani ( amefariki ) unakuwa unamaanisha nini labda kwa Great Thinkers hapa?

Huwa mnanilazimisha niwajibuni hovyo.
 
wewe mtu huwa ni mwungana sana, ubarikiwe...
Asante Mkuu. Kuna Watu hapa JF wanadhani kuwa labda ni Wao tu pekee ndiyo walioumizwa, ila kuna Wengine wangeyasema yao huenda wangejiona wana afadhali.

Taifa haliwezi kuwa na Harmony kama Wananchi wake 24/7 Wana Visununu ( Vinyongo ) Mioyoni mwao lakini nyote mkijitambua ni Wanadamu na hatujakamilika basi Kusameheana na kuombeana Rehema ni Jambo la Kheri mno.

Bado nawaombeni kuwa tumsameheni.
 
Pole sana mkuu,,yule kiumbe hakuna ambae hajapitia madhila yake, nahisi yule hakuwa binadamu
Hasa wapiga ma deal aliwabana sana! Hadi Ndama Mutoto ya Ngombe na genge lake nao walibanwa na bwana yule Mwenda zake!!
 
Mwendazake safari yetu ya maisha aliifanya kuwa ni ya taabu Sana na mateso Tena KWA kipindi kifupi,alipotufikisha kimasafa palikuwa ni mbali ikatuchosha kufikiria kurudi,na tulivyovipoteza ni vingi hatuwez kuvihesabu,bora tuhesabu tulivyovibakiza
Tatizo mnapenda sana kuendesha Maisha yenu kupitia shot cut! Ndiyo maana mnamchukia sana Mwenda zake!!
 
Sidhani kama huu Upuuzi wenu wa hii Kauli inafaa katika Uzi huu sana sana unaweza kujikuta Unadharaulika tu.

Unaposema ( tena Kuhoji ) kuwa kwani Yeye anasemaje wakati unajua kuwa hatunae tena duniani ( amefariki ) unakuwa unamaanisha nini labda kwa Great Thinkers hapa?

Huwa mnanilazimisha niwajibuni hovyo.
Siku hizi Vitoto vingi humu,baada ya kua Tanzania ndiyo Nchi pekee bando ziko chini sana kwa bei!!
 
Mie binafsi sitaki na sina mpango wa kumsamehe mungu na malaika a.k.a jiwe. Alijiona yeye ataishi milele akataka na kubadili Katiba ili atawale milele so apambane na mzigo wake wa dhambi alizozitenda hapa duniani.
Jamani mnamsingizia Baba Watu,alisema kabisa hataki kuendelea baada ya kumaliza muda wake,ni wale wanafiki tu walikua wanajaribu kujipendekeza kwake kumbe wenyewe ni mahasidi wake na tunawaona Sasa ndimi zao zilivyo badilika ghafla!! Na nakumbuka ujumbe uliletwa kwenye media Polepole!!
 
We unadhani alikuwa hataki kweli? Wakati sukumagang walishaandaa move ya kupeleka muswada bungeni wa kubadili Katiba? Can't you see walivyochanganyikiwa baada ya kufa?

Wao Wana maslahi yao na jamaa sababu ya ukabila walijihakikishia as long atakaa pale juu, then they will be safe. Kuna uhuni mwingi sana ulikuwa unaendelea Mwenyezi Mungu ametuepusha nahisi hata ingeleta machafuko kwenye history ya nchi hii.

Hauoni tafrani iliyojitokeza baada ya Kayafa kufa mpaka ukaona CDF akaamua kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mama anachukua Ile nafasi???

Haya kuna balaa huko kwenye chama maana walitaka nafasi zao mama akawatosa naona wanataka kuleta figisu kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti ndio maana ukaona mzee JK akatoa statement ya kusema hatarajii kuona kiti cha urais kinatenganishwa na uwenyekiti wa chama.

Ofcoz JK huwa anatumia soft language Ila angekuwa Kayafa ungesikia Hadi matusi.

So kwakweli aendelee tu na umalaika wake huko aliko na umungu wake. Katuachia mbegu mbaya sana.
 
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Nakuhakikishia wanaombeza magufuli na kufurahia kifo chake ni wachache saaana (wengi wapo humu mitandaoni) kuliko walioumizwa. Msamaha wako hauna maana, kwasababu unawaomba watu wapumbavu waliojawa na chuki.
 
Kuna waliotumbuliwa kwa vyeti feki
Kuna madanga yamafisadi jiwe kala vichwa
Kuna mtu alikua anakula mishahara yawatumishi hewa
Kuna wale chawa wawale maofisa wa TRA na bandari
Kuna wale chawa wama pedeshee

Hao wote nafamilia zao hawawezi kumsamehe mwendazake mpka dunia inatanduka. Tuwaache wateme nyongo zao maana miaka 6 yamwenda zake kwao ilikua nizaidi yajehanamu.
Umeongea kweli kabisa. Wanahasira za kunyooshwa vilivyo. Mazoea ni mabaya sana.
 
Huyu hata ukimsamehe, kuna vitu amefanya mwaka 2016-20 lakini madhara yake tutayaona hata baada ya 2035 Mungu akitupa uzima.

Naogopa Rais atakayekuwapo 2035 atalaumiwa kwa PERFORMANCE wakati ni uozo uliosababishwa na Mwendazake.

Hatumpumzishi huyu, spanna mpaka ahera
Unampiga spana mtu ambae hakusikii wala hayupo kwenye ulimwengu. Hujioni kama ni mpumbavu.
 
Unampiga spana mtu ambae hakusikii wala hayupo kwenye ulimwengu. Hujioni kama ni mpumbavu.
Vipi mbona kama umepaniki sana kila unachotuma lazima uite watu wapumbavu, kwani marehemu amekuachia ujauzito??

Relax get used to it, kuna mabaya na mazuri, sasa kama wewe uliona mazuri tupu just take it easy, katafute urithi maisha yaendelee.

To some of us he was just another hooligan, it's a bitter sweet you can swallow it or spit it out.
 
Back
Top Bottom